Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG-20221230-WA0030.jpg
 
Niliwahi kusoma kisa kimoja cha kijana aliyekamatwa na Polisi kwa kosa la uzururaji.Alipofikishwa kitbuo cha Polisi alitakiwa atoe chochote (hongo) ili aachiwe,yule kijana alikataa.Kesho yake alipofikishwa mahakamani yule kijana alisomewa shitaka tofauti kuwa aliendesha baiskeli usiku isiyokuwa na taa na kuhatarisha maisha.Akakiri kosa na kupigwa faini shilingi elfu 20.Akalipa faini na baadaye akaenda kituoni kudai baiskeli yake.Pale kituoni Mkuu wa kituo alimuita askari aliyemkamata na kumwamuru ampe baiskeli yake,askari akakiri kumkamata yule kijana Ila akamwomba Mkuu wa kituo aongee naye pembeni.Askari akamlaumu yule kijana kwa nini anataka kumharibia kazi?kijana naye akakomaa na kudai apewe baiskeli yake aliyokamatwa nayo.Huku na huku ikabidi yule askari akatafute pesa na kununua baiskeli mpya na kumlipa yule kijana.Yule kijana alipokabishiwa baiskeli akafungua taa na kumkabidhi askari na kumwambia "baiskeli yangu haikuwa na taa".Jitahidi kutenda haki bila kujali hali ya unayemtendea haki.
Nawatakia heri ya mwaka mpya 2023 tujitahidi sana kutenda yaliyo mema.
 
Back
Top Bottom