kajunjumele
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 2,490
- 1,362
😂😂😂😂Uwoya na Dogo Janja
😂😂😂😂Uwoya na Dogo Janja
Dawa yao ndogo tu,kawasomee albadri hivyo vihela vyao vipukutike,wenyewe watakuangukia"Nimeona story ya jana, jamaa akilalamika kuhusu mama yake. Nahisi watu hatupo tayari kuyasema haya ila kuna muda wazazi wanazingua sana, ila ndio hivyo wamekuwa wazazi.
Mimi nimetoka familia ya watoto tano, kwa bahati mbaya au nzuri mimi ndio mtoto wa kwanza.
Kinachoniumiza ni kuwa sipewi heshima yangu kama mtoto wa kwanza kisa sina hela. Ndani ya familia nimepoteza kabisa kauli, hakuna kitu nitaongea na nitasikilizwa.
Hii yote inatokana na hali yangu ya uchumi. Watoto kwao ni wale wenye uwezo. Ndugu zangu wamenizidi kipato na mmoja wao yule mwenye hela zaidi ni kama ndio amechukua haki ya kuwa mtoto wa kwanza. Siheshimiki kama kaka.
Unaweza dhani nalilia heshima, hapana. Ila kuna mida kuna mambo unatakiwa ushirikishwe kama mtoto wa kwanza tena wa kiume unashangaa maamuzi yameshafanyika, ukiuliza unaambiwa mdogo ameshasema. Nitafanya nini?.
Tena hapo madogo nimewabeba mimi. Ningesema nijipambanie mwenyewe ningekuwa mbali sana. Ila nilijinyima ili wadogo zangu wasome. Na wazee wanalijua hili.
Sasa hivi ndio wananifanyia madharau.
Hakika binadamu tunasahau mapema sana kama kuku". Anonymous, Dar.
#watunistory
Pole!Imenitokea hiyo leo wakati nashindilia uchafu hadi sasa niko na maumivu![]()