Mwanamke akitaka kukufundisha tabia, hata Shetani hukaa chini na kuandika notes
Mume wangu alikuwa mlevi wa kupindukia. Kila mara niliitwa kwenda kumchukua baa akiwa amelewa tirarira.
Familia yangu pamoja na marafiki walinishauri nimwache lakini nilimpenda sana na niliamini kuwa ipo siku nitapata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo lake.
Siku moja nikaamua kupata suluhisho la haraka sana.
Ikatokea nilienda kumchukua akiwa hoi hajiwezi kwa kinywaji.
Badala ya kumpeleka nyumbani, nikaenda naye mortuary. Ndiyo, nilimpeleka chumba cha kuhifadhai maiti na nikafanya mazungunzo na mhudumu ili alale karibu na maiti kwa chini na kuandoka zangu kurudi nyumbani.
Baada ya saa mbili, yule jamaa na lile baridi kule ndani kilevi kikakata kichwani na akili zikarudi.
Akaanza kumuomba mhudumu wa mortuary aruhusiwe kutoka kwani bado hajafa.
Mhudumu akamchapa viboko na kumtaka aendelee kufa na alale pamoja na wenzake akisema "Maiti wewe ulikuja kufanya uchawi humu ndani. Lala chini hapo pamoja na wenzako".
Baada ya kuomba sana, akaruhusiwa kutoka na kurudi nyumbani.
Tangu siku hiyo, mume wangu hanywi pombe kabisa. Hata soda hanywi. Kinywaji chake ni maji na maji yenyewe yasiwe ndani ya chupa.



