Kwa hiyo looking yake mzigo hata kwenye buti siweki bora nipakate tuWw usiwaze wala nini View attachment 2353850

Ha ha ha....Matokeo ya bia ya 1 hadi ya 6..
Chupa ya kwanza, huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anaperuzi simu tuu..
Chupa ya 2, kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, biashara, kazi, nk, na wakati huu hata takwimu hutolewa kwa usahihi….
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Uhispania bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Simba bila kukosea. Kucheua kunatokea kwa wingi..
Chupa ya 3 huanza kuleta furaha na pia huu ni wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…
Bia ya 4 hufanya masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kelele za mziki wa baa utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki..
Bia ya 5 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu. Na kipindi hiki ni changamoto kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalama; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali.....'!!!
Ukifikisha kiwango hiki unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko ma stage show wote!
Kuanzia bia ya 6 na kuendelea.. chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake utajilaumu sana. Wanasema ukilewa ndo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamuelekeza kweli jinsi alivyo fala na kuwa hajui kuendesha kampuni vizuri..
Pia unaweza kusema kweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao uchumba unaweza kuota nyasi fasta tuu…
Ha ha ha....
Vijana tunateseka sana na shimo lisilo mwisho........
View attachment 2351829
View attachment 2351830View attachment 2351831

😂😂😂Matokeo ya bia ya 1 hadi ya 6..