Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Baa​

Jamaa kaingia Bar..

Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji...
Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu.
Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi...

Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili yake, maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake.

Zogo pevu lilianzia hapo....😊
 

Tamaa mbaya..​

Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake:
JAMAA: Shem nakupenda!
MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki
yako akijua? tena ukome
JAMAA: Ntakupa shilingi milioni 1
MKE: Daah! Basi njoo kesho mchana
mume wangu akiwa kazini!

Kesho yake Jamaa kaja
na milioni 1 akamkabidhi..

Akapewa mbususu, akapiga weee shoo ya kufa mtu.. style kibao, tena Kwa kujinafasi.. Wakamalizana, wakaagana na huyo mke wa rafki yake vizuri tu.

Jioni ilipofika, Mume akarudi home..

Mume: Wife, za hapa?
Mke: Nzuri tu mume wangu, sijui wewe, mzima?
Mume: Mie poa tuu..
Mume:, Vipi, rafki yangu SAM ameleta hela yangu milioni 1 hapa?
MKE: (kwa mshtuko mkubwa na mshangao, huku moyo ukienda mbio na presha ikipanda na kushuka).. uuhhh, eeh, aah, ndi ndi ndi, ndi..yooo🙄
MUME: Yeees! Ndio maana nampenda rafiki yangu SAM.. Amekuja ofisini kunikopa asubuhi akaahidi kurudisha hapa home kabla ya jioni, na kweli karejesha.. Saaafi sana.. Big up to my friend SAM!!!!
Mke hooiii……
 

Dawa..​

Dokta: Mama, tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.

Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe, ndiyo, wewe uwe unakunywa vidonge hivi vinne kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona...
 
IMG-20220909-WA0043.jpg
 

Matokeo ya bia ya 1 hadi ya 6..​

Chupa ya kwanza, huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anaperuzi simu tuu..

Chupa ya 2, kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, biashara, kazi, nk, na wakati huu hata takwimu hutolewa kwa usahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Uhispania bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Simba bila kukosea. Kucheua kunatokea kwa wingi..

Chupa ya 3 huanza kuleta furaha na pia huu ni wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…

Bia ya 4 hufanya masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kelele za mziki wa baa utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki..

Bia ya 5 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu. Na kipindi hiki ni changamoto kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalama; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali.....'!!!

Ukifikisha kiwango hiki unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko ma stage show wote!

Kuanzia bia ya 6 na kuendelea.. chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake utajilaumu sana. Wanasema ukilewa ndo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamuelekeza kweli jinsi alivyo fala na kuwa hajui kuendesha kampuni vizuri..

Pia unaweza kusema kweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao uchumba unaweza kuota nyasi fasta tuu…
 

Mume na mkewe?.​

Mume akamwambia mke wake:
“Funga macho yako tufanye maombi”

Akaanza kwa Kimombo:-
“…Ooh Lord, I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith, I pray 4…...”

Mke akadakia, “Unaniringishia unadhani mimi sina eeeh” akaanza:-
I pray 4 Felix, I pray 4 Temu, I pray 4 Rweyemamu, I pray 4 Masawe, I pray 4 Benson, I pray 4 Onyango, I pray 4 Swai, I pray kwa wote niliowasahau!!

Ikawa ni ligi ya michepuko..!!!
 

Mtalii na mbongo..​

Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari..
Akaanza maongezi na kijana anayeongoza boti,

Mtalii: Do you know Biology, Psychology and Anthropology?
Kijana: No
Mtalii: Then you know nothing under the sun.. You are useless, and u’ll die with your illiteracy!”

Baada ya muda boti ikapata hitilafu ikaanza kuzama...
Kijana: Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii: (akajibu huku ametoa macho): No
Kijana: Then you will kufalogy and mambalogy wil eat your makaliology because of your bad-mdomology. 😎
 

Wabongo ni noma!​

Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa wizara moja ilianguka.

Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu.

Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO.

MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Wizara..

MBONGO: “Mi ntajenga kwa milioni 270”

MSIMAMIZI WA WIZARA: “Wee una wazimu nini..!!
Yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”

MBONGO: "Sshhh.. taratiiibu bhasi.. milioni 120 zako, 80 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina kimyakimya”

MBONGO akapewa tenda😊
 

Jamaa bahili kamtoa mke wake out..​

Jamaa: chips kuku bei gani?

Mhudumu: elfu 8
Jamaa: chips yai je?
Mhudumu: elfu 3

Jamaa : ziina kachumbari?

Mhudumu: ndiyo

Jamaa: Kachumbari mnauzaje?

Mhudumu: Kachumbari ni bure.

Jamaa: Eewaaa, ok, basi naomba leta kachumbari sahani mbili, chips ziache tuuu..
 

Zawadi ya nguo za ndani..​

Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazani moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia.

Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.

MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili kila siku?!!!

Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanzia

MUME: Watu gani hao watakaokuambia unachupi moja?
Kumbe kuna watu unawaonyesha kitumbua changu?
Leo utanambia...’

Ungekuwa wewe ungefanya nini?
 
Back
Top Bottom