Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Haswaaaa.....

Kuna namna flani hivi kama ya kucheza salsa 💃🏽 huwa naipenda sana kucheza na mzee mwenzangu mwenye nguvu zake.....!

Enzi kalabash panabamba nilikuwa nacheza ile live band mtindo wa salsa mwanzo mwisho.

Sasa mpatane mnaenda moves sawa weeweee huku ukimgeukia ukampa mgongo bado steps mnaenda sawa...
Halafu anakushika mkono mmoja juu unazunguka unarudi kwenye kutizamana mnaendelea kucheza weeeweeee aaachaaaaa....!

Sasa hapo kijana wa nini ati, akati hata wallet wanazo hao hao 45 - 60...😋😋😋
Dancing is a vertical expression of the horizontal desire😝
 
Dancing is a vertical expression of the horizontal desire😝

Umemaliza kila kitu....!

Ukipatana na mupenzi wako wote mnapenda mziki, waaaiiiii......

Mnacheza ile mziki unaamsha vimeng’enya vyote mwilini halafu mkitoka hapo......

Ni kusukuma torori hadi gereji (wheel barrow) mnalala wepesiiii usingizi mnonoooo....! 😅😅😅
 

Mambo 10 ambayo huwezi kufanya:​

1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu nywele zako,

3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi;
4. Saivi Unajaribu kufanya namba 3
6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama umbwa😁
7. Unatabasamu !
8. Umeruka namba 5;
9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo.
10. Unatabasamu kwa kuwa umebambwa!
 

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili​

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini huko? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, wife naye kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiria haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi huu…?

 
Back
Top Bottom