Mamba ya saluni ni shida
SUGAR MUMMY alienda Salon kusuka.. wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati.
SUGAR MUMMY akaona isiwe shida, akaamua kurusha ndoano.
SUGAR MUMMY: Mambo?
KAKA: Poa.
SUGAR MUMMY: Mimi na wewe tunaweza kuongea baadae?
KAKA: Kuhusu nini?
SUGAR MUMMY : Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA: Sawa, ila nitamwambia nini MKE wangu?
SUGAR MUMMY: Aaah ilo sio tatizo, wee mpange tu, mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA: Haya, mwambie mwenyewe, ni huyo hapo anayekusuka..
Mtanange uliojiri baadaye ulihitimishwa Kwa Sugar Mummy kusachiwa pochi na msusi kuchukua malipo yake kamili, na Sugar Mummy kuondoka huku akiwa amesukwa nusu kichwa tuu 😊