antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 49,678
- 130,554
Mbinu aliyotumia mdada wa kazi kuongezewa mshahara kilainiii:
Mdada: mshahara wangu hautoshi, naomba kuongezewa.Mama mjengo: Una sababu zozote za kustahili kuongezewa?
Mdada: ndiyo
Mama: nipe sababu 3
Mdada: napika vizuri kuliko wewe.
Mama: duh! Nani kakwambia?
Mdada: baba
Mama: sababu ya pili?
Mdada: Mie ni msafi kuliko wewe, nikisafisha nyumba inakuwa nadhifu zaidi.
Mama: nani kasema?
Mdada: baba
Mama: enhee, ya tatu?
Mdada: kitandani najitahidi zaidi ya wewe!
Mama: (huku amefura, akijiandaa kumrukia upesi) - mume wangu ndo kakwambia na hili?!!!
Mdada: HAPANA.. ni shamba boy!
Mama: ssshhhh!!! Shusha sauti baba asisikie, chonde chonde... Ntakuwa mgeni wa nani mie!!! Mwanangu, mdogo wangu, nipo chini ya miguu yako.. mwenzio naomba unitunzie hii siri.. Kuanzia saivi nakupandishia mshahara wako mara TATU😊



