Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Kuna siku mzee wangu alikuwa anasinzia sitting room. Nikamwamsha mara ya kwanza akasema sawa ntaenda kulala ndani, nkarudia mara pili akajibu bwana wee kwani mimi nakukera kitu gani nawe sinzia tushindane.

Akakaa kidogo akasinzia nkamwasha tena baba nenda kalale chumbani.. jibu lake ndo mpaka sasa huwa nacheka " nikisinzia hapa nafanya mipango ya kutafuta ada yako, saa niamshe maana yake umejilipia ada yako ya mwakani "

Nkawa mpole. Kumbe mzee naye alikuwa ananisikilizia kama ntamwamsha tena.. mama kaja anasema ona wewe mtoto upo busy humwamshi baba yako analiwa na mbu...

Nkamjibu anatafuta ada kasema... aliamka huku anacheka akasema leo nimekuweza mpuuzi wewe. Akanipa gwara akasepa room kwake kulala
 
nikiwa rais
20220114_123617.jpg
 
Back
Top Bottom