#HADITHI
MWEKANADHIRI NA SHETANI.
Hapokale paliondokea mtu namkewe waliokua na ng'ombe jike ambae walimpenda sana. Wakamtafutia #FAHARI mzuri ili baadae ng'ombe wao awe #MBUGUMA. Basi mke akamwambia mumewe, ng'ombe wetu mara yakwanza akizaa ndama jike nitafanya #KARAMU niwakaribishe mabibi wote wamtaa huu, mume nae akamwambia mkewe ng'ombe wetu mara yakwanza akizaa ndama dume nitatoa pesa kumpa #SHETANI. Basi baada ya mwaka mmoja ng'ombe wao akazaa ndama dume, mke akamwambia mumewe unakumbuka ahadi ukiotoa..? Mume akajibu naikumbuka, mke akamwambia basi ahadi ile #NINADHIRI yapaswa uitimize usipo itimiza ng'ombe wetu wote watapatwa na miosi.
Mume akamwambia mkewe sasa shetani mwenyewe nitamuona wapi..? Katika kijiji kile kulikuwepo na mzee mmoja aliefanya makao yake nje kidogo ya mji, akiitwa #MTABIRI_WA_MALIMWENGU. mke akamwambia mumewe, mwendee mtabiri wa malimwengu huenda atakushauri namna ya kuitoa nadhiri hii.
Mume akakubali, siku iliofuata alifunga safari kummwendea mtabiri wamalimwengu.
Wahenga wenzangu mnaikumbuka hii..? Je niendelee kuwasimulia au inatosha..?
View attachment 2010558
(Sehemu ya pili)
Basi mke akamwambia mumewe mwendee mtabiri wa malimwengu huenda akakupa. msaada wa kuitoa NADHIRI hii. Siku iliofata mume akafunga safari hadi kwa mtabiri wa malimwengu, alimkuta, baada ya kukaribishwa vyema akapewa kigoda akaketi, yule mtabiri wa malimwengu akamuuliza akisema bwana #IMEJIDAWA asubuhi na mapema unashida gani..? Mweka NADHIRI akamjibu akisema, Mimi niliweka NADHIRI kwamba ng'ombe wangu mara yakwanza akizaa ndama dume nitatoa pesa nimpe shetani sasa kwabahati juzi ng'ombe wakazaa ndama dume napesa nilizo ahidi kumpa shetani ninazo, lakini shetani mwenyewe simjui je nifanyeje..?
Matabiri akamwambia nitakufundisha #AYA nawe utaisoma hadi uikariri moyoni kesho asubuhi nenda kwenye ule msitu mkubwa, ukifika katikati ya msitu panda juu ya mti mrefu kuzidi yote kusha mwite shetani kwasauti ya #KUPAZA akiitika mweleze shida yako nae atakukidhia.
Basi mweka NADHIRI akahifunza ile Aya hadi ikamkaa moyoni, siku ilofata akajilawa asubuhi sana akaenda hadi msitu, akauona mti mrefu akaukwea hadi juu, kisha amaanza kuisoma ile Aya kwautulivu sana, kisha akaita "SHETANIIII SHETANIII" akasikia sauti kwambali ikimwitika "UUUUU, UUUU!!!" Mweka NADHIRI akaiambia ile sauti "Niliweka NADHIRI kwamba ng'ombe wangu akizaa ndama dume nitatoa pesa kukupa wewe bahati ng'ombe wangu kazaa dume kwahiyo njoo uchukue pesa zako nilizo kuahidi. Ile sauti ikamjibu ikisema "NENDA KAMPE MKE WANGU MIMI SITUMII PESA" mweka NADHIRI akaiuliza ile sauti "MKEO ANAITWAJE NA ANAKAA WAPI.."? Lakini ile sauti haikujibu japo mweka NADHIRI aliuliza tenanatena,, basi mweka NADHIRI alirudi nyumbani akiwa kachoka kabisa asijue la kufanya.
Je mweka NADHIRI atampata wapi mke wa shetani..? Fatilia simulizi hii hadi ujue kilicho tokea.