Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

[emoji23][emoji23]acha uchoyo n...nambie kazi yake.
Hiyo ni miguu ya binadamu.
Wakazi wa vijijini wakati wa baridi kali kama la sasa miili yao huwa hivyo.


Pole wa kishua[emoji23]
FB_IMG_1626456989901.jpg
 
Aah huyu msukuma wangu alijua kunilaghai tu vizuri, sikumpendea urefu wake hata.
Nakukubali sana Mtumishi. Kama kweli umeolewa na Msukuma basi mhongereshe huyo ngosha kwa kujipatia mke mwema ajabu. Mpendane na maisha yenu yakajae upendo huku mkichukuliana na kuvumiliana. Bagosha [emoji8][emoji8][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Mara ya kwanza simu zilianza zikiwa na kampuni ya mobitel mwaka1998. Nakumbuka ofisini kwangu nilienda kufundishwa jinsi ya kutumia hiyo simu. Mobitel ilianza na tv ya DTV Mwaka 1992 au 93. Mimi nilinunua TV mwaka 1994 ila wale waliokuwa wanatoka mtoni walikuwa wanaangalia video siyo tv. Radio tulikuwa na Radio TZ kiswahili na kiingereza na mtangazaji wa english channel alikuwa anaitwa Eda Sanga .
Asante mkuu.
Mi pia nilikuwepo zama hizo kiongozi, nayakumbuka yote hayo.
Nakumbuka tukio la mmiliki wa CTN Al Munir Karim kumkodishia wauwaji Regnald Mengi, kwakuwa tu mswahili naye anaanzisha TV channel.
Ilikuwa mwaka 1992-93.
Kashfa hiyo iliondoka na aliyekuwa kamanda wa polisi D'salaam aliyeitwa Triphon Maji na Aliyekuwa katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani wakati huo Silivano Adeli.

Nakumbuka fainal za kombe la Dunia mwaka 1994 tulijimwambafai kwenye TV channel zetu kupitia ITV.
 
Back
Top Bottom