Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Enzi zilee
IMG_0937.jpg
 
Hiki siyo kituko.
punguza kumeza meza panadolView attachment 1773716
I got that lesson, sinamchezo na pain killer yoyote kwa sasa
Shida ya pain killers nyingi za kawaida ni huyo mdudu Acetaminophen (na ndugu zake). Anaharibu ini kwa haraka sana akitumiwa hovyo hovyo na sehemu nyingi kumewekwa onyo kali kwamba atumiwe kwa uangalifu sana. Ni hatari zaidi akichanganywa na pombe hata kama ni kwa kiasi kidogo tu.

Sasa sisi watu wala hatuzingatii dosage tunabugia tu. Na unakuta mtu anameza acetaminophen kichwa kinatulia halafu anaendelea tena kugida bia. Ni hatari mno...

Na maumivu mengi ya kichwa sababu yake kuu mara nyingi ni dehydration tu. Inashauriwa sana ukiumwa na kichwa hasa kama ni wakati wa joto, kunywa glasi mbili au tatu za maji halafu usubiri nusu saa. Mara nyingi kichwa kitapotea kama ni cha kawaida tu.

Shida sasa mtu uko dehydrated kichwa kinakuuma halafu unajipigilia dawa zenye acetaminophen kama Panadol, Hedex na Tylenol. Unaumiza sana ini na ukizoea ni kujiandalia matatizo makubwa mbele ya safari. Na ini likikorofisha hakuna cha msalie mtume.

Hata pain killers zenye ibuprofen na NSAIDs (isipokuwa aspirin japo nayo inaweza kusababisha kuvuja kwa damu), zinaongeza sana uwezekano wa kupata mashambulizi ya kiharusi na mshtuko wa moyo. Ni za kutumia kwa uangalifu sana !!!
20210504_185353.jpg
 
Back
Top Bottom