Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

FB_IMG_16121965292621230.jpg
 
Hahahaaa, nmekumbuka mbali kweli, huu utundu bwana. Mimi kipindi mdg nilikuwaga najiingiza bunje za mahindi kwenye matundu ya pua, badae zikaa muda mrefu vikatuna bwana, si unajua unyevunyevu wa makamasi! Sasa Okwaaa nikataka nizitoe, zikagoma, jaribu tena wapi! Aiseee nilichanganyikiwa nikaanza kulia, wazee wanakuja jaribu wee wapi, penga makamasi yanatokezea pembeni zenyewe zinabakiii, heeee. Mwisho wakakata tamaa ety inabidi apelekwe hospital wakamfanyie operation 😁😁😁😁, sielewagi walivoingia ndani sijui nilizitoaje zoteee😁
Ck nyingine wakasema kapeleke chupa dukani, mi njiani nikaanza kuzichezea, nikaangiza vidole kwenye chupa. Tembea wee nikajisahau, nmefika dukani nikajieleza, sasa toa hizo chupa, heee nilihangaika wapi, muuza duka akatoka nisaidia naye vuta chupa weee nikawa napata maumivu ya vidole sanaaa, badae muuza duka ety inabidi tupasue chupa tu ili vidole vichomoke, nikawaza huku nmenyanyua chupa kwa kila kidole, kwenye dak mbili tu nilivoshusha chupa zote zikaanguka chini😁😁, kumbe damu zilizokuwa zinashuka kwenye vile vidole zilishindwa kupanda tena kwa sababu ya kuminywa na chupa hivo zikajaa nyingi na kufanya vidole vivimbe sehemu zilizozama kwenye chupa, kwa hiyo kitendo cha kuweka chupa juu kwa kuinamisha midomo ya chupa kumbe na damu ndo zilipopata balance ya kupanda kwenye vidole😁

HUYU MTOTO NA HUO UTUNDU WAKE KANIKUMBUSHA MBALI SANAAAA.

Na kupitia utundu wangu nimepata ujuzi wa vitu vingi japo uharibufu nao ulikuwa mwingi sanaa. Ilifika hatua kitu chochote kikiharibika nyumbani utasikia huyo ni Okwaaa kaharibu yani hata kama siyo mm ila mimi ndiye nilibeba msalaba wa wengine🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom