Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Huyo ni mvivu.tu wa asili, ndio maaana hata kazi anashinfwa kutafuta, chamssingi sema nae, ukikna haelewi, watafute wakubwa zake, maana bila kusema, kimya kingi kina mshindo mkuu
 

Hujaachia kitu mkuu na ukitaka kujua rangi halisi ya mwanamke ni wakati wa shida wengine anaweza kukuambia ukatupe mpaka pedi.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
 
Wanawake ni watu hatari sana,utakuta hata hyo nyumba wanayoishi kaikuta ajawai kulalamika imejengwaje gari, analotumia pia hivohivo.ni mambo mangapi mmeo kakufanyia kipindi ajawa block.?yote hayo umeyasahau umeamua kumnanga mmeo.?ukiyoka kazini ukaandaa kitanda itakukost nini.?ithought it feels gud to prepare a bed gor ur husband.hapa tatizo ni kazi na wanawake ndo mlivo kutoa hela ya mboga na hela ya chakula unaona umeingilia majukum ya watu na hicho hasa ndo kinachokusumbua hayo mengine umejazia tu.hela zenu ni za salon kusuka nywere na pedecure.
 
Hujawahi kupata stress wewe. Yaani unaamka huna hata energy ya kutoka kitandani. Ukijilazimisha kuoga ndo imetoka hiyo.

stress ni mbaya sana. Na zaidi mwanaume anaweza kuwa anajisikia nikifanya kazi nitaonekana ni kwa sababu sina hela. Hata hiyo kuomba kikombe cha kahawa, anataka kumkumbusha kuwa mimi ni mumeo.

wakati mwenza anapitia hali ngumu anahitaji support ya hali ya juu. Kuna hausigelo, wasaidiane kazi za nyimbani. Period!
Stress zinamfanya nini mtu?
Je mwanamke nae akiwa na stress awe hivyo?
Hiyo ni tabia tu ya mtu kiukweli.
Hata kama una stress ukikaa na mtoto na kucheka nae stress zinapungua.
 
Yaani nakubaliana na wewe kabisa. Mwanamke akikupa mia yake ataifuatilia hadi ushike adabu yako. Ila huyu nampongeza, anamuwekea mafuta pia jamaa anaweza kuzurura? Mwanamke mwingine angemuacha hapo achine!
 

Yani hivi ndivyo inavyokuwa ikitokea mwanaume umepata matatizo kazini huku mkeo akiwa kazini! Kwa hiki ulichoandika nadiriki kusema huu ni u-self centred at it best level!

Yani mume wako yupo katika kipindi cha mpito cha kula bench (jobless), halafu wewe kwa akili zako fupi unakuja kumuanika humu mitandaoni!? Naamini kama huyo mumeo angejua your inner part ikoje asingekuoa in the first place regardless of how much he loves you. Hii tabia ni ya ajabu sana!

WanaJF, binafsi natambua kama maisha yana ups and down za kutosha tu, mara leo unacho kesho huna, hayo ndio maisha. Sasa ikitokea una mwenza wa aina hii (kama huyu mleta mada), si ndio kitakuwa chanzo cha kupata msongo wa mawazo? Tena ushukuru mumeo hata pombe anywi!
 
Yaani nakubaliana na wewe kabisa. Mwanamke akikupa mia yake ataifuatilia hadi ushike adabu yako. Ila huyu nampongeza, anamuwekea mafuta pia jamaa anaweza kuzurura? Mwanamke mwingine angemuacha hapo achine!

Serious dada inaumiza,huyu Dada ilibidi ajue mmewe yuko katika hali gani,kweli wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika,yani kukuja net na kutandika kitanda yanakufanya unasahau mema yote mmeo alokutendea pindi yko poa.?sie tuso oa mnatufanya tufikilie mara mbili mbili aina ya mwanamke wa kuoa.yale maneno ya kuishi kwa dhida na raha kipindi cha ndia hayana maana tena siku hizi.
 
Ndiyo ilivyo kaka,mm ni mhanga wa hii kitu nilikuwa naitwa kama mvivu na nisiyejielewa hasa anaanzisha mazungumzo haya ya dharau mkiwa mna wageni au mnakula!
Ni shida

Duuh!! Imeniuma kaka hebu tupe uzoefu wako liliishaje?? Wanawake ni viumbe wa kukaa nao kimtego mtego ukijiachia unaumbuka
 
Duuh!! Imeniuma kaka hebu tupe uzoefu wako liliishaje?? Wanawake ni viumbe wa kukaa nao kimtego mtego ukijiachia unaumbuka

Mkuu sisi wanaume hatuongei sana mambo haya lkn nakuambia kuwa kama ww na mkeo wote mnafanya kazi ni vyema sasa kuchangia bills ili kama mambo kwako siyo mazuri hapo baadae uwe na cha kuanzia!

Kama unatoa hela zako kila bills na zake unamuachia azihifadhi kazi ukipoteza huwa baadhi yao wanasahau kama zake hazikuwahi kulipa bills!Nimejifunza kwa hilo
 
Yaani nakubaliana na wewe kabisa. Mwanamke akikupa mia yake ataifuatilia hadi ushike adabu yako. Ila huyu nampongeza, anamuwekea mafuta pia jamaa anaweza kuzurura? Mwanamke mwingine angemuacha hapo achine!

Ndoa haziendi kimikwara hivyo. Siku za neema akitoka ilikuwa sio kuzurura, akitoka leo kwa mafuta ya mke ni kuzurura! Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi!

Na halafu kwamba 'angemuacha achine', yaani mnaona hiyo ndoa mume kaing'ang'ania sana au? Kuna kanuni moja:Mwanamume yeyote anaweza kuwa mume kwa mwanamke yeyote, na mwanamke yeyote anaweza kuwa mke kwa mwanamume yeyote.

Kwa mantiki hiyo basi, wawili hao hakuna anayelazimika kukaa na mwenziwe; ni makubaliano ya hiari tu. Kama mnaona mwanamume 'atachina' basi huyu mkewe na amuoneshe mumewe hii mada tunayoijadili hapa kisha atambue kumbe boxer zake zimeanikwa JF, kama hamtamuanzishia mwenzenu uzi mwingine wa kumtafutia chumba mtaani. Maneno ya udhalilishaji na nyodo siku zote humpeleka mtu pabaya!
 

Yaani mkuu nimekosa nyongeza na msamiati fasaha wa kuweka hapa, all in all you're more than correct!
 

Pole mwaya,Mume wako ni mvivu tu mwenzangu looh,ni vizuri ukimwambia ukweli kua tabia zake zinakukela,kwani hata wewe ni binadamu na unahitaji kupumzika pia,lakini mwambie kwa lugha laini na ya upole,naimani atabadilika.
 
Ndiyo ilivyo kaka,mm ni mhanga wa hii kitu nilikuwa naitwa kama mvivu na nisiyejielewa hasa anaanzisha mazungumzo haya ya dharau mkiwa mna wageni au mnakula!
Ni shida


Pole sana mkuu Malafyale,,,,hii post imenisikitisha kweli...ila nashukuru kwa busara za wana MMU wamemjibu vizuri sana nami sina la kuongeza....On ur side I hope umesolve issue sasa

Big upo King'asti, Heart, nyumba kubwa PATIENT ZERO na wengine uzoefu wenu unaonekana
 
Last edited by a moderator:
we mwanamke wewe leo lazima nikulime talaka urudi kwenu
Alaaa.......!! Yaani umeona bora uje unianike huku aise leo utanitambua ngoja urudi huko kibaruani kwako utakuta nishatoa kila kitu nje
Ha ha ha ha! Mkuu utakula nini akiondoka? Bibie si ndio anasimamia shoo nzima? Usije kwenda kumbembeleza kwao kwa magoti na machozi.

Fanya hivi,
Msaidie mkeo kulea mtoto.
Ukiamka tandika kitanda.
Msaidie mkeo baadhi ya
Vitu.
Nilitaka kusahau, boksa zako fua mbona muda unao mkuu? Punguza u-dume utachokwa ohoooo!
 
Kama alimtafuta huyo wa kwanza atapata tu na mwingine.

hujanielewa, mimi huwa najishangaa sie wanawake ni wabinafsi sana aisee. Hujawahi kuona mwanamke anaishi na mumewe na nyumba imejaa ndugu za mke. Ila thubutu mama mkwe ama shemeji aje akae mwezi. Atafanya visa ajabu. Na hapo unakuta hanunui hata kitunguu humo ndani?

suali ni kuwa, hiyo mwanaume alikuwa anatandika kitanda ama kujitengenezea kahawa enzi ana ajira? Na hata kama alikuwa anafanya, kama umeelewa posts zangu naongelea stress inavyoweza kukufanya ukakosa hata nguvu ya kuoga!

kuna mdada ofisini alikuwa anauguza mama mkwe nyumbani kwake. Mama wa watu ana mabinti walioolewa 4, wote jobless wanakula hela za waume zao wenye uwezo. Kwa hiyo kila siku wanashinda kwa kaka yao wanampikia mama na kumuogesha. Shosti analalamika eti nikisema nimuogeshe mama wananikatalia. Namuambia si mama yao, acha wamuogeshe bwana! Ooh wanaweka carrots nyingi wanafuja chakula! Mama mwenyewe ana terminal disease, wewe hununui hata karoti humo ndani! Why bother? Tulimzodoa hadi akaacha kuwamaindi wifi zake.

hao ndio wanawake kaka. Mungu akujaalie upate chizi kama mie ama snowhite asiejali petty issues. Ila kuna button ukibonyeza utazijua rangi zoote hahaha
 
Last edited by a moderator:
Nyie hamjui uvivu na kudeka ni sehemu ya mapenzi jamani? Mkoje? Mie hata nikisimamishwa na polisi naulizwa card ya gari na triangle, nampigia Paw. Na hadi aseme lipa fine ndo ntalipa. Kama gari ya kufungua bonnet ntamuuliza inafunguliwa wapi! Mie ntafua boksa na kutandika kitanda ila ndo ajue na yeye ana sehemu yake! Kutandika kitanda na kupandisha net takes dakika 5, kweli ndo zinamvunja mgongo huyu shosti ama anashindwa tu kumsimanga baba wa watu?
Pole mwaya,Mume wako ni mvivu tu mwenzangu looh,ni vizuri ukimwambia ukweli kua tabia zake zinakukela,kwani hata wewe ni binadamu na unahitaji kupumzika pia,lakini mwambie kwa lugha laini na ya upole,naimani atabadilika.
 
Last edited by a moderator:
Tamthilia za kifilipino zimewaharibu vijana. Hawajui ndoa ni mapito na wakati wa shida ukikumbuka fadhila maisha yanaenda. Paw wangu akivua viatu kimoja unakuta sebleni na kingine bafuni. Sasa akifulia ndo kuna mabadiliko? Mie sijutii kuzeeka, sokoni hamna waume wala wake! Msalimie wifi kaka.
 
Last edited by a moderator:

Zandile kwanza pole, kikubwa katika kuboresha mahusiano ni pamoja na mawasiliano "communication" ongea na mumeo in a positive way si kwa kumlaumu au kulalamika, lakini pia omba kabla haujaongea naye. Mungu anaweza fanya kitu katika hiyo shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…