Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Pole sana mdada na inaonekana ulimzoesha toka zamani sasa ukianza kumsema hiki kipindi hana kazi utaambiwa unamsimanga japo unaweza kujaribu kumueleza anaweza akakusikia
 
Sijawahi kuwaza kwa vile hana kazi kwani najua hii kitu inaweza kumtokea mtu yoyote,
Ninachojiuliza hapa hata Kutengeneza Chai yako mwenyewe ni ngumu?
Mbali na hapo huoni mwenzio ananyonyesha mtoto anasumbua ,mama hulali hata kusema mke wangu ngoja nimsaidie hata kutandika kitanda?
ama mtoto amekaa karibu na wewe anacheza akilia unamwangalia tu?
Na nikikaa nae sasa ataona ninamsema kwa vile hana ajira ..
mmh?

Mwanamke unadhihirisha jinsi ambavyo huwezi kukaa na mwenzio!! We huoni hilo ni tatizo (hapo kwenye bold)?

Yaani ni hivi huyo mumeo keshaathirika kisaikolojia na anaelekea kuwa au keshapata stress kwa kuwa hana kazi, wa kumliwaza na kumuondolea hilo tatizo ni wewe kwa kumfariji na kumuweka ajione hiyo hali ni ya kawaida.

Kumbuka siyo zoezi la kusema dakika moja ukajua limepona, linaweza kuchukua miezi kutegemea na alivyoathirika!! Ukianza kulalamika hivi, ndiyo unammaliza kabisa huyo jamaa!! Tumia busara na akili ya ziada kwa kusoma kwenye mitandao namna ya kukaa na mtu wa namna hiyo
 
Sasa mkuu we unaona suala la kutoa au kutotoa neti ni la kuleta hapa jamvini kweli? Unadhani mumewe anaiona hii post? Mshikemshike wake angeumudu? Kama hivyo unamshauri nini huyu dada kuhusu neti?

Kila mume au mke ana udhaifu wake tena pengine wa kawaida tu kama huo. Si kila kitu kina ushauri, mahali pengine unaijua tabia ya mtu wako na masuala yasiyokuwa na athari kubwa mkavumiliana. Kama kila kinachodhaniwa kuwa tatizo kitaletwa hapa hili jamvi halitakuwa na mada zingine tena.

Kuna mambo ktk ndoa unaweza kudhani ni tatizo kumbe ni tabia ya maumbile ya mtu; na hii KILA mtu anayo. Na hayo ndiyo mambo ya kuvumiliana na kukubaliana, kama mfano wa mtu mwenye wivu uliozidi. Ni lazima umjue mtu, ujue jambo fulani ni asili yake, ndipo utaweza kuishi naye. Ukisikia jubilei ya miaka hamsini ya ndoa usidhani wamefika hapo kiwepesi tu. Maisha yana milima na mabonde mengi, juaneni, vumilianeni, mtapendana na mtafika!

Sina hata cha kushauri kwa kuwa haya mambo kila mtu ni unique na huwa anatafuta jinsi yake ya kupambana nayo (hasa niki-refer kipengele cha jubilei). Kuna wengine wanayazungumzia na wengine wanayapotezea kiukweli na wanaopotezea huku wakiumia alimradi kuitafuta gold jubilee.

Bottom line, mchango wako ni mujarab kwa kusongesha taasisi nyeti ya ndoa.
 
Ndio tatizo la baadhi ya Wanawake wakishakuwa na ka kazi cha kulisha familia basi nae atajiona m/ume, kwahili sishangai w/ume wakiwa wanawakataza kufanya kazi.
Real kabisa unakuja kulalamika eti hatandiki kitanda? Naona jamaa kushika remote kubadilisha stations hapo kwenye King'amuzi inakukera sana?
Ishu kubwa hapa ni kuwa jamaa JOBLESS lkn ulivyovitaja ni bijisababu tu maana huo udhaifu mpk mnapata watoto wawil hukuliona?


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?

Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .

Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.

Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.

Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije kufua mie.

Anapiga mswaki na kukaa kwenye kochi kusubiri atengenezewe chai na apelekewe, atabadilisha chanel mpaka lunch atakula atabadilisha Chanel zake baadae anawasha gari kwenda kutembea. Saa mbili au saa tatu atarudi atakula atakamata tena remote mpaka saa sita ataingia kulala na ukali sasa kitu kidogo tu manung'uniko.


Hivi jamani wanaume mkioa kazi yenu huwa inakuwa kutoa matumizi ,kula na kulala tu?

Hakuna mnachoweza kusaidia?

Ladies hivi wote mko kwenye hali hii??
we mwanamke wewe leo lazima nikulime talaka urudi kwenu
Alaaa.......!! Yaani umeona bora uje unianike huku aise leo utanitambua ngoja urudi huko kibaruani kwako utakuta nishatoa kila kitu nje
 
SIJUI NIANDIKE MAKALA AU KITABU??
kweli wanaume mna wake wa ajabu sana, mke anataka utandike kitanda? mke anataka ukae ukafue mashuka , mtoto amekojoa ukafue na kuanika matandiko? anataka uingie jikoni uanze kupika, ukate nyanya, ukate kituu na uonje chumvi kwenye mwiko...anataka upike chai/cofee na uonje kama sukari imetosha>>....INAWEZEKANA NINA MKE MWEMA, NINA MKE ALIYELELEWA AKAJUA KAZI ZA MWANAUME NA ZA MKE...tangu niwe na mdogo wenu katu haniruhusu kufanya izi kazi, uwa tunagombana sana asubuhi, naamka mapema , nashika brashi na dawa ya viatu ghafla namuona nyuma yangu...'dia unafanya nini???' ...nanyanganywa brash, naandaliwa nguo na kila kitu, yani mwanzoni ilikuwa taabu kufanyiwa kila kitu ila nshazoea na kuona haki yangu...WATOTO WA KICHAGA MIXER TANGA mna mambo sana...mnajua baba anataka nini na wakati gani...mimi ni kuleta fweza nyumbani, kulea mke na watoto na kuleta maendeleo.

TURUDI KWA TOPIC

Mleta mada kwa nini unameanza misala tu baada ya mzee kukosa kazi?
Mbona miaka imekatika haujawahi kumwambia aingie jikoni, afue nepi na kujipkia cofee?
Kama unakwazika weka binti wa kazi afagie nyumba, alambe mwiko-aonje chumvi
Shida yangu kubwa ni kuona unaonekana kuelemewa na mzigo wa familia kwa mwaka mmoja tu wakati mmesaidiana na mzee kwa zaidi ya miaka 6.
- Mama unashaurije waume wenye wako kibao ambao wake uwa hawafanyi kazi wanasubiri baba alete, je nao wachoke kama wewe? Hapo ndo ujue wanaume wenye wake wasiofanya kazi wana busara sana, ikitokea mme ndo hana kazi daah anatangazwa JF , uwazi na sani, ooh mume anakaa kwenye Tv, ooh mume hana kazi, ooh analelewa... nk nk ayo ni mambo ya ajabu best!!

Kama una kazi nyingi, tafadhali muweke dada au kaka wa kazi, hatukukupa kaka yetu akapike, akafue nguo za watoto, na mbona wakati ana kazi aya yote uliona poa??

Nakumbuka wakati ana kazi, na wewe haujawa na ka duka ka kusaidia kusogeza maisha ukisaidiana na mshahara wako haikuwa shida, leo hii unataka akafue?

Nakuomba dada yetu tafadhali muache mumeo apunguze stress, na mshahara ujao naomba umnunulie CD za kutosha, naomba uongeze channel za DSTV , uweke na binti wa kazi...Baba muache ajiriwaze, mpende kama ulivokuwa unampenda wakati ana kazi....nakuhakikishia mtu wenye ujuzi na mwenye maono kuna siku atapata kazi na utaanza kuona aibu kwa aya yaliyojitokeza wakati hana kazi.

Kuna mzee mmoja aliwahi kupitia hali hii akiwa injinia wa wakati wa Tics ya karamagi, akapata shida sana na madharau kibao hadi kufikia hatua ya kunyimwa gari na mke au hata nauli na kipesa cha kujikimu mpaka tukawa tunamsaidia....Baada ya kupata tenda na kurudi bandarini kitengo kingine, leo hii anamiliki canter, ana gari2 za kutembelea, na ghorofa lake limeisha pale kimara na amehamia july toka ki-jumba chake cha Morocco.
MKE UPENDO UMERUDI KANA KWAMBA NDO WAMEOANA JANA, WATOTO WALIKUWA WAJEURI SASA WANAMSALIMIA BABA KAMA MFALME, JAMANI TUJITAHIDI KUONESHA UPENDO WAKATI BABA AU MAMA AMEKWAMA. NINA MENGI ILA DADANGU TAFAKARI AYO KWANZA!!
 
Last week nilikuwa naosha Vyombo ,akaniita mama F naomba unitengenezee coffee akiwa ameshika remote anaangalia TV

Nikamwambia naosha vyombo my dear ila kila kitu kipo mezani please nisaidie kutengeneza wala hakunyanyua mguu anasubiri nikatengeneze ,na hapo mtoto nimeweka mgongoni wangu alikuwa mgonjwa

Nikatengeneza kikombe chake nikampa akasema asante basi

Hapo bado hamjaongea unaona. Umetoa tu mfano wa yale yanayokukera. Tafuta muda muafaka tena kwa lugha nzuri tu mwambie dukuduku lako. Vinginevyo ataendelea na Remote Control yake huku wewe unaumia.
 
pole zandile kwani kuna shida gani ukimwambia baba watoto vijikazi vimenielemea nisaidie vijikazi kidogo
tena wamwambia kiutani ,leo nakata kitunguu wewe utanisaidia kukata nyanya dear haha..
kahawa nimeshweka mezani ukitengeneza yako baba Chanja usisahau na kikombe cha mie nadhani kahawa iliyotengenezwa na wewe nahisi nitamu sana
Sie Chief>
 
Kwanza pole. Pili kwani wakati mnaanza urafiki mpaka uchumba alikuwa na tabia hizo hizo zakila kitu ufanye wewe? Kama ndio na wewe ulimchukuliaje wakati ule? Maana sometimes kuna magonjwa tunayoyalea sisi wenyewe kasha baadae tunalalamika yanatuchosha..... ukiondoa suala la motto ambalo utasema kuwa kipindi kile isingekuwa rahisi kumpima nalo but kuna engine mfano hilo la mkiamka wewe ndo utandike kitanda kwani zamani ilikuwaje ikiwa ulikuwa una"sleep over"?.... Otherwise kaa nae kwa upendo siku amefurahi ogea naye, vunja ukimya otherwise utazeeka siku si zako kasha yeye akatafute mchepuko kijana kitaani. Wakaka wa siku hizi mbona wengi ni waelewa tu ilmradi uonyeshe msimamo wako na ujue namna ya kuuonyesha.
 
Aisee, pole sana na mtihani huo.
Ila au hakuna mapenzi kati yenu au ulimuendekeza kuanzia mwanzo. Sasa hiyo ni defence mechanism yake, anaona akifanya kitu ndio utaona imekuwa wajibu wake.

Ila wanaume jiaminini basi, kitu kama hiki chaweza vunja ndoa halafu mnaanza kutafuta mchawi. Ukute akiwa bachelor alikuwa anafanya zaidi ya hayo.
Any way, siwezi imagine kuwa na mume wa design hiyo hivyo sidhani kama naqualify kushauri.
 
duuuu pole shostito haya maisha bila kusaidiana utamuona mtu mzigo bure,embu jaribu kukaa nae chini mliongelee hili swala
 
Mie nadhani inapobidi kusaidia inabidi msaidiane tu angalau kudumisha mapenzi ndio maana ya watu wawili
,Mwanaume nae ajifunze hata kutandika kitanda once a week ha ha duuh:A S wink:
 
Wamama wengi huchukia waume zao pindi wakiwa na watoto wadogo....

Sababu kuu ni moja...they feel like they don't love or care for their babies...na hakuna mama atampenda mtu anayemshuku kumchukia/kutomjali mtoto wake...

Naweza sema asilimia 90 ya wanaume duniani shughuli ya kulea mtoto mchanga bora umpe shoka apasue kuni (na wazungu ni hivo hivo msiwaone barabarani mkazani ni exceptional)

Sasa michango humu isije chochea ugomvi nyumbani...hata wachangiaji wengine humu ukute waume zao ndio worse...

Na aina maana kuwa hawapendi watoto wao...wakikua watakuwa wanaongoza madukani...na mishe mishe nyingine...

Vumilia tu yatapita...

Afu usichanganye weakness zake na kuwa jobless kwani hapo unaharibu hata uulichotaka kusema na unataka ku prove kuwa wanawake wakiwa na pesa kuliko waume zao ni wanyanyasaji...

je angekuwa na kazi bado ungemlaumu akusaidii mtoto...?

Kazi kama ni nyingi ongeza house helper mwingine mpaka mtoto akue kuepusha maugomvi na ligi zisizo za lazima...
 
Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?

Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .

Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.

Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.

Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije kufua mie.

Anapiga mswaki na kukaa kwenye kochi kusubiri atengenezewe chai na apelekewe, atabadilisha chanel mpaka lunch atakula atabadilisha Chanel zake baadae anawasha gari kwenda kutembea. Saa mbili au saa tatu atarudi atakula atakamata tena remote mpaka saa sita ataingia kulala na ukali sasa kitu kidogo tu manung'uniko.


Hivi jamani wanaume mkioa kazi yenu huwa inakuwa kutoa matumizi ,kula na kulala tu?

Hakuna mnachoweza kusaidia?

Ladies hivi wote mko kwenye hali hii??

Uliyataka mwenyewe. Hukulazimishwa kuolewa. Na bado. Hizo ni rasharasha.Subiri masika.

 
Hiyo red hapo imeonyesha weledi wako,,,ni facts! ila huyu bidada kwann ameliingiza hili la kutokuwa na kazi kwa mmewe, kwani angesema jamani mme wangu yuko hivi na hv nishaurini nimbadilishe....anatakiwa kuelewa mmewe yuko kwenye wakati mgumu mno na yeye ndo mfariji pekee...so aache mbwembwe na kufikiria hasi zaidi.

Kabisaa! Mwanaume ni vile umleavyo,ukienda nae kiupendo atakusaidia tu tena kwa moyo ila ukileta kauli za 'yaani mimi ninavyo hangaika ina maana huoni,? Kutwa nzima kwenye makochi...inakera kwakweli arghhh..' Na mdomo unakunja....na kumnyari juu. Hawezi akawa mstaraabu,coz ile pride yake kama mwanaume itakuwa inamsukuma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom