Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

jamani hivi kweli ni sawa unaamka asubuhi unamwacha amelala unarudi jioni hata net haijatolewa hiyo ni sawa??mmmh

Hiyo sio sawa...ila ukizungumza nae taratibu na kwa upendo mbona hadi kufagia atafagia huyo mumeo. Tatizo hujataka kuzungumza nae,unaishia kumlaumu tuu.!
 
Ni uzembe wako hayo wenzako wajanja huwa wanayaangalia tangu kipindi cha uchumba,jamaa yupo sahihi kwa maana hukujua kuishinae tangu mwanzo wa mahusiano. Ingawa mimi binafsi ingawa sijaoa lakini nauhakika nitakuwa namsaidia mke wangu kwa hali zote hata nikiitwa bushoke poa tu mradi yeye ananikubali na kunipenda. Poe sana dada yangu
 
Haya mleta mada.soma katikati ya mistari,kunywa maji ujipooze na kisha changanya na zako!
 
Haya mambo mkiwa wachumba hua mnaona sema mnachuniaga tu..

Umeona eeeh!Si huwa kuna zile hope za kwamba atabadilika tu...wakati hufanyi initiative yoyote ya kimueleza hupendezwi na kitu fulan.
 
Wamama wengi huchukia waume zao pindi wakiwa na watoto wadogo....

Sababu kuu ni moja...they feel like they don't love or care for their babies...na hakuna mama atampenda mtu anayemshuku kumchukia/kutomjali mtoto wake...

Naweza sema asilimia 90 ya wanaume duniani shughuli ya kulea mtoto mchanga bora umpe shoka apasue kuni (na wazungu ni hivo hivo msiwaone barabarani mkazani ni exceptional)

Sasa michango humu isije chochea ugomvi nyumbani...hata wachangiaji wengine humu ukute waume zao ndio worse...

Na aina maana kuwa hawapendi watoto wao...wakikua watakuwa wanaongoza madukani...na mishe mishe nyingine...

Vumilia tu yatapita...

Afu usichanganye weakness zake na kuwa jobless kwani hapo unaharibu hata uulichotaka kusema na unataka ku prove kuwa wanawake wakiwa na pesa kuliko waume zao ni wanyanyasaji...

je angekuwa na kazi bado ungemlaumu akusaidii mtoto...?

Kazi kama ni nyingi ongeza house helper mwingine mpaka mtoto akue kuepusha maugomvi na ligi zisizo za lazima...

umelikoroga kulileta hapa na lazima ulinywe,,,,,akipata kazi uje tena hapa.....kanga mweupe wewe.....
 
MM ndio maana nasema ndoa kama ndoa ni nzuri na tamu sana na hata Mungu aliiweka kwa nia njema ila sisi wenyewe ndio hatujielewi, tunachukua hulka, uzembe ,uvivu na kila uozo tunaunganisha nakusema ndoa ni ngumu.

Mfano huyu mume wako ameadhiriwa na mfumo dume anachufahamu yeye nikwamba mwanamke ndio anajukumu lakufanya kila shughuri ndani ya nyumbani . Nawewe limekukera kwakua unalisha familia ila mume angekua na kazi akahudumia familia hata usingelalamika hapa .
 
Kabisaa! Mwanaume ni vile umleavyo,ukienda nae kiupendo atakusaidia tu tena kwa moyo ila ukileta kauli za 'yaani mimi ninavyo hangaika ina maana huoni,? Kutwa nzima kwenye makochi...inakera kwakweli arghhh..' Na mdomo unakunja....na kumnyari juu. Hawezi akawa mstaraabu,coz ile pride yake kama mwanaume itakuwa inamsukuma.




Ni kweli ndugu angu!
 
Nope! Si kila kitu ni mfumo dume, hali aliyonayo ya kukosa kazi inaweza kuchangia kumpa stress. Mtu mwenye stress unaweza ukamchukia kama hujamjua, hujikuta anawaza muda wote na asijue alifanyalo ni kosa!!

Swali ni kwamba, alikuwa hivyo mwanzoni akiwa na kazi?? Tabia halisi ni tofauti na stress ujue, inahitajika njia makini kubaini tatizo lake

kwel kabisa
 
Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?

Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .

Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.

Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.

Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije
 
Yani mi nadhan nmekuelewa vizur hapo tatizo si yale anayoyafanya mme wako ila tatizo ni kwamba mume wako hana kazi na ni kawaida kwa mwanamke kuana ivyo kama mme hana kazi. Na hata ivyo ndoa yenu iko hatarin kuvunjika endapo mme ataendelea kutokuwa na kazi Pole sana. kumbuka mwanamke ameumbwa kuhudumiwa na mwanaume na si mwanaume kuhudumiwa na mwanamke ndio mana yanakutokea hayo.
 
jamani hivi kweli ni sawa unaamka asubuhi unamwacha amelala unarudi jioni hata net haijatolewa hiyo ni sawa??mmmh

Kuna kazi ambazo ki ukweli ni ngumu saaana kwa mwanaume, kazi za ndani kama kutandka kitanda, kufua, kuosha vyombo n.k n kazi ngumu mnooo kwa wanaume tuliowengi, achana na mwanaume aliyeoa, jarb kumchunguza hta mwanaume bachelor tu utagundua wengi wanateseka na hizi kazi!!!
kosa la mumeo hapo ni moja tu, kutomtake care mtoto lakin hayo mengne n kawaida saaaana kwa wanaume.
 
Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?

Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .

Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.

Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.

Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije kufua mie.

Anapiga mswaki na kukaa kwenye kochi kusubiri atengenezewe chai na apelekewe, atabadilisha chanel mpaka lunch atakula atabadilisha Chanel zake baadae anawasha gari kwenda kutembea. Saa mbili au saa tatu atarudi atakula atakamata tena remote mpaka saa sita ataingia kulala na ukali sasa kitu kidogo tu manung'uniko.


Hivi jamani wanaume mkioa kazi yenu huwa inakuwa kutoa matumizi ,kula na kulala tu?

Hakuna mnachoweza kusaidia?

Ladies hivi wote mko kwenye hali hii??

Hapo kwenye red ni dalili za mwanamke kumchoka mume wake kisa hana kipato. Lazima ujichunguze wewe kwanza. Hizo nguo zamani ulikuwa hufui? chakula ulikuwa hupiki? mtoto ulikuwa hubembelezi? Nahisi pia umeanza kuchepuka ndo maana unamdharau mumeo kisa kipato.
 
Uliyataka mwenyewe. Hukulazimishwa kuolewa. Na bado. Hizo ni rasharasha.Subiri masika.


du daktari sasa kaamua kumuua mgonjwa ambaye amekuja kutibiwa...ushauri wako ni kama sumu kwenye kidonda, utazisha machungu best!!!
 
Teh Teh baba yake jamani! Ila wanaume mbadilike hata kumbeba mtoto kweli ? Mi napenda swaga za waarabu mda mwingi wapo na watoto wao

best tatizo kuu ni kuwa jamaa hana kazi...awa wanandoa wana mtoto wa miaka mitano ila baba hakuwa mzembe ila leo kuna mtoto ana miezi9 , hana kazi ndo misala imeanza...ukichanganya kutokuwa na kazi, stress plus kutotenda majukumu ya kuilisha familia ndo basi kila lawama itamzukia baba...kuna siku akirudi msitarini hautakaa uyasikie aya!! ujue kuna wadada mjini wana nyuma nzuri na zenye insurance, wana pesa na magari yenye bei na isurance , yaani yapo mpaka waamue kudispose....ila tu wanshinda kwa sangoma kusaka wachumba, wengine wanalalwa ili dawa iwaingie ili wapate wachumba maskini wanatapeliwa...wengine mna ndoa mnashangaa eti ooh mume wangu---- ajabu!!
 
huyo ana uzembe wa asili au ndo wale mfumo dume umeota mizizi damuni kwao
Na tulio wengi wa namna hiyo ndo huwa tunalalamika kuwa wanawake wakiwa na senti wanaota pembe na kushindwa kuwaheshimu waume zao. Kwa utaratibu huo wanaume tutanyanyaswa sana. Hata kitanda chake kutandika hawezi? Labda ana matatizo ya kisaikolojia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom