Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Ulifanyiwa kitchen party wewe...??? Siri za ndani hizo!

Huo ni utashi wa mtu mwenyewe, inawezekana kukosa kazi kunampa mawazo mengi sana na kupelekea stress!! Jaribu kuwa nae close na kwa upendo na utani unaeweza kumtania kuhusu kitanda!! Usitumie maneno makali coz anaweza kuhisi kukosa kwake kazi ndiko kunakufanya umfokee!

Hivi nyie wanaume kweli hauwezi kufika kipindi uone mkeo kazidiwa na wewe upo hata kumsaidia tu kuweka chai kwenye Kikombe ni ngumu?
Hata kufua nguo zako za ndani ni kazi??
Mie sijasema aje kuosha vyombo no..basi wakati mie nadeki na kupika kuna ugumu wa kufua Boxer zako mwenyewe?
Kutoa net Kitandani na kuweka shuka vizuri ni kazi??
 
Stress zinamfanya nini mtu?
Je mwanamke nae akiwa na stress awe hivyo?
Hiyo ni tabia tu ya mtu kiukweli.
Hata kama una stress ukikaa na mtoto na kucheka nae stress zinapungua.
Nope! Si kila kitu ni mfumo dume, hali aliyonayo ya kukosa kazi inaweza kuchangia kumpa stress. Mtu mwenye stress unaweza ukamchukia kama hujamjua, hujikuta anawaza muda wote na asijue alifanyalo ni kosa!!

Swali ni kwamba, alikuwa hivyo mwanzoni akiwa na kazi?? Tabia halisi ni tofauti na stress ujue, inahitajika njia makini kubaini tatizo lake
 
Hapa tukiangalia juu juu tunaweza kutoa ushauri mbovu wa kuharibu ndoa! Nawashauri wadau msichukulie poa poa sana!
:focus:
Kitendo cha kusema hana kazi na mambo yote unafanikisha wewe, huo sio uungwana! Mwenyewe si umesema kama anahangaika kutafuta?

Naamini hayo manung'uniko yako yamerise kwa kasi kubwa baada ya kuona masuala ya misosi unafanikisha wewe! Unataka malipo kana kwamba naye achukue jukumu lako! Naamini akiosha vyombo utafurahia kitu ambacho si kizuri!

Hizo kazi unazonung'unikia hapo ni wajibu wako wa msingi!

Nakubaliana nawe 100% kwamba mapenzi ni kusaidiana! But unahitajika kuwaza zaidi ya hapo! Kitendo cha kufukuzwa/kusimamishwa/kuacha kazi kimeathiri huyo mmeo! Kisaikologia ana adjustment disorder! Unatakiwa kumpa moyo na kumfariji na sio kumnung'unikia tu!

Nna uhakika huyo mme anakupenda sana!

In nature kuna me hawapendi kufanya kazi ulizojitaja especially wanapokutwa na majanga eg: kufukuzwa kazi!

Huenda huyo mmeo anajiuliza hivi: "Kwa kua sina kazi, na kwa vile mkewa wangu ana kazi na anawajibika, jee fact hizo zinifanye nifanye kazi za kike? How if ikiwa ni ubushoke? Kwanini kufukuzwa kazi iwe sababu ya kuondoa amani yangu!
...
Nakushauri kaa naye chini uongee naye kwa upendo, acha kumlalamikia sana! Malalamiko hayajengi yanabomoa tu! Naamini na nitaendelea kuamini kwamba ukifanya hivyo mtaishi kwa amani!
...
Waweza pita na hapa huenda ukajifunza kitu: https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/696522-makundi-manne-ya-binadamu.html

Wish you all the best!

Sijawahi kuwaza kwa vile hana kazi kwani najua hii kitu inaweza kumtokea mtu yoyote,
Ninachojiuliza hapa hata Kutengeneza Chai yako mwenyewe ni ngumu?
Mbali na hapo huoni mwenzio ananyonyesha mtoto anasumbua ,mama hulali hata kusema mke wangu ngoja nimsaidie hata kutandika kitanda?
ama mtoto amekaa karibu na wewe anacheza akilia unamwangalia tu?
Na nikikaa nae sasa ataona ninamsema kwa vile hana ajira ..
mmh?
 
Mbona ndivyo walivyo wengi sana hahahaah yaani Wanaume Weusi ( samahani kama nimewakwaza hapa kwenye rangi ila ndio ukweli ) Wachache sana wanaojua wajibu wao wa kusaidia hasa ishu ya watoto , yaani huyo hata iweje habadiliki Ngo ! Ndio alivyolelewa hajawahi Muona Baba yake akifanya hizo shughuli , na usiku anataka umchezee Segere kama kawa ....!:A S wink: na ukitaka kumbadilisha tu utaibua zogo la Mwaka ! ndio kilema chake na ukibebe tu sasa Till Death do apart !
 
Tatizo hapo ni kuwa umeolewa. Ingekuwa mmeoana kusingetokea tatizo kama hilo.

Tatizo lingine, ni pale mume anapokuwa mwizi akiwa kazini, akiachishwa kazi maisha yanakuwa magumu X 3.

Ukiona mwanamme mvivu namna hiyo ujuwe ni mvivu kazini pia na mvivu bedroom. Kwa situation kama hiyo usitegemee kama kuna ufumbuzi wowote utapatikana, hicho ndio kichocheo kikubwa cha wewe kutembea nje ya ndoa kama bado hujaanza mpaka leo.
 
Last week nilikuwa naosha Vyombo ,akaniita mama F naomba unitengenezee coffee akiwa ameshika remote anaangalia TV

Nikamwambia naosha vyombo my dear ila kila kitu kipo mezani please nisaidie kutengeneza wala hakunyanyua mguu anasubiri nikatengeneze ,na hapo mtoto nimeweka mgongoni wangu alikuwa mgonjwa

Nikatengeneza kikombe chake nikampa akasema asante basi


Dah... hili limeniuma! Pole bidada, ngoja wenye uzoefu wakushauri!
 
Umepata hata muda wa kuzungumza nae kweli?! Huu ni muda wa kumfariji na kuonesha upo pamoja nae katika kipindi hiki kigumu,pengine unam-mistreat maana unajiona ushakuwa 'fazahaus'... Zungumza nae kwa upendo,hakuna mwanaume timamu anaekubali kuwa chini ya mwanamke.. Sidhan kama ulikumkuta na kiburi hicho mlipoanza,wakati mwingine kiburi kinajengeka humo humo ndani ya nyumba...

Hiyo red hapo imeonyesha weledi wako,,,ni facts! ila huyu bidada kwann ameliingiza hili la kutokuwa na kazi kwa mmewe, kwani angesema jamani mme wangu yuko hivi na hv nishaurini nimbadilishe....anatakiwa kuelewa mmewe yuko kwenye wakati mgumu mno na yeye ndo mfariji pekee...so aache mbwembwe na kufikiria hasi zaidi.
 
hmmm kwanza pole...huyo mumeo bana anamatatizo...
Sio wote kwenye hali hiyo..kuna wanaume wengine wako safi mpaka raha,unasaidiwa kufua,kulisha mtoto,yaani kazi zooteee pale msaada unapohitajika/anapoona ni vyema kufanya...lakini kumbuka hiyo inategemea na malezi ya kwao..Mtu ambaye hajawahi kufanyishwa mazoezi ya kazi kwao usitarajie atakuja kufanya baadae.
Ikumbukwe pia mwingine anakuwa anajua kazi ila kufanya/kukusaidia anaona utamdhalau kuonekana mume ----- au kwakuwa hana kazi,kwahiyo hapo anajitutumua aonekane bado yumo..

Well said... Haya mambo ya kusikia saluni kwamba mume wa fulani anafanyaga hivi basi na yeye akataka kulipeleka kwa mumewe bila kujuwa background ya mumewe ni ssheeeiiidaahhh
 
Kwa sababu unatoa hela ya kuendesha familia haina maana kuwa mumeo ndio atandike kitanda. Hususan hawa wanaume tuliowaleoa kuwa "kazi za kike" na "kazi za kiume"

Wakati mumeo ana kazi nani alikuwa anatandika kitanda?

Huyo mwanaume hukumjua tabia kabla hajakuoa?

Ungelalamika kutokusaidia malezi ya mtoto. Lakini mengine yote kwa mtazamo wangu sioni kama yana tija

Na mume anaenda kutembea au anaenda kuangalia michongo?

Unless muneo ni mzungu, lakini kama mumeo ni mwafrika inabidi ujue wanaume wa kiafrika walivyo
 
Mleta mada unaonesha Ni kwa jinsi gani unavyotumia kete ya mwenzio kutomuwa na kazi kumnyanyasa.Umesema Una mwaka mmoja na nusu Katina ndoa lakini Una mtoto WA miaka mitano,je,mpaka mmefikia hatua ya kuwa na mtoto mkubwa namna hiyo,jukumu lake lilikuwa lipi❓❕➖Je,tabia hii alikuwa nayo kipindi chote au imetokea Mara tu baada ya kufukuzwa kazi❓
 
Tatizo hapo ni kuwa umeolewa. Ingekuwa mmeoana kusingetokea tatizo kama hilo.

Tatizo lingine, ni pale mume anapokuwa mwizi akiwa kazini, akiachishwa kazi maisha yanakuwa magumu X 3.

Ukiona mwanamme mvivu namna hiyo ujuwe ni mvivu kazini pia na mvivu bedroom. Kwa situation kama hiyo usitegemee kama kuna ufumbuzi wowote utapatikana, hicho ndio kichocheo kikubwa cha wewe kutembea nje ya ndoa kama bado hujaanza mpaka leo.

Duh, bi mkubwa umeua kabisa....
 
Kwa sababu unatia heka ya juebdesha familia haina maana kuwa mumeo ndio atandike kitanda.

Wakati mumeo ana kazi nani alikuwa anatandika kitanda?

Huyo mwanaume hukumjua tabia kabla hajakuoa?

Ungelalamika kutokusaidia malezi ya mtoto. Lakini mengine yote kwa mtazamo wangu sioni kama yana tija

Na mume anaenda kutembea au anaenda kuangalia michongo?

Unless muneo ni mzungu, lakini kama mumeo ni mwafrika inabidi ujue wanaume wa kiafrika walivyo

jamani hivi kweli ni sawa unaamka asubuhi unamwacha amelala unarudi jioni hata net haijatolewa hiyo ni sawa??mmmh
 
pole shemeji kwa hatua unayoipitia.

mimi nimeoa nina mke na watoto namsichana wa kazi.ndio familia yangu.

i can say mambo mengi apo wanaume wengi tunafanana.mimi binafsi ni mvivu to hell kwa kazi za home...

tangu nimeoa sijawahi kufua,kupika wala kutandika.....

the good about me nina kauli nzuri sana kwa mke wangu.sijawahi kuidharau family yangu kwa namna yeyote ile...

malezi ya mtoto najitahidi sana....mara kadhaa napenda kuwalisha wanangu...kumwogesha mtoto,kucheza nao n.k

napenda pia kuongea mamwili matatu na wife na kumfanya rafiki all the time...

jaribu kukaa chini na jamaa mwelekeze taratibu..,japo aanze na la kulea mtoto...ni muhmu sana ayo mengine dada anaweza kuweka sawa!!!
Hongera kwa ujasiri wa kuweza kulea familia peke yako....
 
Tena wanaume wa hivyo wapo humu humu mmu....

Kiatu kinavuliwa barazani

Soksi inatolewa sebuleni

Shati linatupwa koridoni

Suruali chumbani

Singlend bafuni





Pole mwaya..... huyo kidume ndivyo alivyo na huwezi kumbadili maana hiyo iko kwenye damu. Lakini shost tabia hizo za uvivu hukuzigundua mkiwa wachumba? wanaume kama hawa huwa hawawezi hata kufuta viatu vyao na kuvipanga sehemu yake.

Na humu JF wapo kibaoooo kutwaaaaa na vilaptop/visim vyao hawajisogezi. Subiri kidogo utawaona tu....

Amani moyoni mwako jipe mwenyewe! Fanya shughuli zako usishughulike naye afanye sawa na asipofanya sawa tu... atabaki mumeo daima. Upo hapo zandile?
 
Last edited by a moderator:
Mumeo anashida kubwa na kuwa mwangalifu,ni kipsycologia huwakuta wengi baada ya kukosa kazi au kipato!ni kama bomu kuwa mwangalifu mfariji na kumpa matumaini lasivyo jambo dogo anaweza fikiri unamnyanyasa,anaweza kujiua ukakosa vyote! Kuwa makini na msali pamoja,tena unabahati angekuwa anapiga ulabu ndio ungezimia bora anakaa na TV.
Mpe matumaini na asichague kazi hata inakipato kidogo ili imkipu busy!
Hiki ni kipimo cha ndoa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hapo issue ni kuwa jamaa sasa kawa mzigo maana kama hizo tabia nina uhakika hazijaanza leo lkn ukawa unamvumilia sababu na yy anachangia tena labda zaidi kwenye pato la familia!

Jamaa kachokwa sababu haleti chochote home kuchangia na hii ndiyo zenu madada wengi!Yalinikuta kama haya nilifukuzwa kwa kuitwa "mbweha"usiku wa manane miezi 7 baada ya kupoteza kazi ehehehehe

Huyu mleta mada hajakuwa wazi sana kuhusu mazingira yote ya ndoa yake. Hata hivyo hapa hapakuwa mahali muafaka sana pa kukimbilia, ilikuwa kwanza waongee wenyewe ikishindikana ndio achukue hatua zingine.

Asili ya ndoa ni watu wawili, na ina stara yake. Kumjadili mume au mke hadharani hivi ni kuidhalilisha ndoa pamoja na wewe mwenyewe, labda kwa jambo lilnalofanania jinai ambalo ni lazima jamii ijue. Mume katoswa kazini, yuko frustrated tena bado katulia nyumbani hana vituko wewe tayari ushamvua nguo zote hapa jamvini! Kwani kabla ya hapo alikuwa anakuoshea vyombo? Hapa unataka ushauri gani sasa, si aibu yenu hiyo?

Mpende mumeo kama ulivyokubali kuolewa, setirianeni, kukiwa na tatizo fuata taratibu za ndoa na ndio maana kuna wasimamizi wa ndoa. Mume kakosa kazi muda mfupi hivi malalamiko kibao tena hadharani, ungeilisha familia wewe siku zote ingekuwaje? Si ndio kuishi pamoja kwa raha na shida?
 
Mleta mada unaonesha Ni kwa jinsi gani unavyotumia kete ya mwenzio kutomuwa na kazi kumnyanyasa.Umesema Una mwaka mmoja na nusu Katina ndoa lakini Una mtoto WA miaka mitano,je,mpaka mmefikia hatua ya kuwa na mtoto mkubwa namna hiyo,jukumu lake lilikuwa lipi❓❕➖Je,tabia hii alikuwa nayo kipindi chote au imetokea Mara tu baada ya kufukuzwa kazi❓
nimesema mme wangu ana mwaka na nusu sasa kazi iliisha
sijasema ndoa ina mwaka na nusu
Siwezi kumnyanyasa na yeye anajua hanyanyasiki hata kidogo
sema ni hivyo vimatendo vyake ndio vinanikera
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom