Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Vitu vinavyonikera ndani ya ndoa

Mbona mie sijawahi kufuliwa chupi na mke wangu. Wenzangu mnafuliwa?
 
Mmeamini kuwa mwanaume asiyekuwa na hela ni mzigo usio bebeka? Anakuwa zoba hana msaada wa aina yoyote. Kero tupu.

Ushauri wangu ni kwamba. Bi dada endelea na majukumu yako kama kawaida, na wewe mkere kwa maneno ya kuudhi ili akatafute shughuli ya kufanya sio kuangalia TV. Usimpe hata shilingi yako, hata kwao kukiwa na shida inayohitaji attention yenu usijikombe kutatua.

Hakikisha watoto wako wanakula na wanapata huduma muhimu. Kuleni vizuri akirudi hiyo saa tatu mwekeeni mezani ugali na mchicha kila siku. Siku nyingine osheni masufuria akute hakuna chakula. Atatia Akili ku mkichwa.
 
pole dada kuwa na mwanaume kochi,hana kazi yeye ni kukaa kwny kochi na kugombania remote na watoto,anyway yote majaaliwa.ila huo ukali na manung,uniko yake ni kutokana na inferiority complex alinayo koz hana kazi anahisi unamdharau,pole sana,kaa nae chini mwombe msaada tu akusaidie atakuelewa.
 
Bila shaka ni lile kabila la ugonile ndaga wana uanaumenization sana hao watu Yan usiombe kukutana nao tena hata huruma hawana
 
Huyo mme wako anajua wajibu wake,big up kwake.[/QUOTE]

Ndo walewale kina ndaga fijo
 
pole sn kwa ndoa za kiafrica asilimia kubwa zipo hivo. wanawake wa cku hz mnataka kuiga tamaduni za kigen bila kufikiri..hkuna beijing ktk maisha halic..beijing ilikuwa inatazama haki za mcng z m/ke na sio me kudeki na kuosha vyombo...shida iliyopo hapo kwako ni kuwa ss hv mmeo anastress za kukos kazi. ss kufny kaz za ndan anajiona inferior. ongeza mapenz kwa mmeo muhurumie omba sn Mungu yataisha na atakupenda maradufu
 
Kwanza nianze kwa kukuita wewe mwanamke ni mpumbavu,tena siyo kidogo ni sana tu...kwa maelezo yako inaonyesha mambo yafuatayo.
1.Mapenzi yenu awali na hiyo ndoa vilijengwa au ulikubali kwa kuwa jamaa alikuwa mambo super,ndio sababu unaweza ukatamka kuwa kwa kuwa sasa hana kazi(ni kweli) basi jukumu lakulea familia ni lako,nini maana yakusema mvumiliane katika shida na raha??wewe siyo ajabu mwenzako akija pata kilema cha maisha ukamkimbia maana umekaa kistarehe zaidi,huyo mwenzako yupo katika hali nzito sana ya msongo wa mawazo ila kwa upeo wako mfupi umeshindwa kuelewa hilo..kwa sasa alivyo hata ukijamba ndani kwa kupumua atafikiri umemdharau,lazima ujifunze kuelewa hali aliyonayo sasa hivi.
2.Maelezo yako yanaonyesha kabisa wewe hujui majukumu yako kama mke ni yapi,unataka kutumia fursa hii ya jamaa kuwa katika kipindi kigumu kumpanda kichwani.
3.Inaonyesha kabisa una mdomo mchafu,huna kauli nzuri kwa maana yakutoelewa wakti gani uzungumze nini.
4.Wewe unaamini upo kwenye harusi na siyo ndoa.

Mwisho,wakati huu ni wakati muafaka wakumuonyesha mumeo yupo na mwanamke sahihi,yamkini MUNGU kawapitisha katika hali hiyo ili uhusiano wenu uwe imara zaidi..achana na maneno ya saloon,kaa ndani jenga ndoa yako.
 
ni mumeo we ndo unamuelewa kuliko sisi kaa nae chini umueleze hisia zako kuliko kuendelea kuuumia tu.
mwambie unaitaji msaada then utapata jibu kutoka kwake kwanini hasaidii
 
Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?

Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .

Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.

Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.

Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije kufua mie.

Anapiga mswaki na kukaa kwenye kochi kusubiri atengenezewe chai na apelekewe, atabadilisha chanel mpaka lunch atakula atabadilisha Chanel zake baadae anawasha gari kwenda kutembea. Saa mbili au saa tatu atarudi atakula atakamata tena remote mpaka saa sita ataingia kulala na ukali sasa kitu kidogo tu manung'uniko.

Hivi jamani wanaume mkioa kazi yenu huwa inakuwa kutoa matumizi ,kula na kulala tu?

Hakuna mnachoweza kusaidia?

Ladies hivi wote mko kwenye hali hii??

Usiaeme kwenye ndoa sema mumeo. Mimi nalea watoto wamenizoea hata kama mama yao hayupo nikiwepo mimi hamna shida tena hao mapacha wananyonya hata akilala huko aliko. Mumeo anahitaji elimu ya ECD aka MMMAM.
 
Ulifanyiwa kitchen party wewe...??? Siri za ndani hizo!

Huo ni utashi wa mtu mwenyewe, inawezekana kukosa kazi kunampa mawazo mengi sana na kupelekea stress!! Jaribu kuwa nae close na kwa upendo na utani unaeweza kumtania kuhusu kitanda!! Usitumie maneno makali coz anaweza kuhisi kukosa kwake kazi ndiko kunakufanya umfokee!

meipenda sana hii jaman, dat's the truth guyz
 
je kama mume naye angekua anafanya kazi, je angemuomba amsaidie hizo kazi za ndani?
Ishu hapa ni huyo jamaa kukosa kazi, lkn cha ajabu unaweza kukuta pengine huyo jamaa alimsomesha au kumuendeleza kitaalum/ujuzi wakati ana kazi labda wakiwa wachumba.
ukweli ni kwamba wanawake sio permanent/longterm providers,
 
Kwanza nianze kwa kukuita wewe mwanamke ni mpumbavu,tena siyo kidogo ni sana tu...kwa maelezo yako inaonyesha mambo yafuatayo.
1.Mapenzi yenu awali na hiyo ndoa vilijengwa au ulikubali kwa kuwa jamaa alikuwa mambo super,ndio sababu unaweza ukatamka kuwa kwa kuwa sasa hana kazi(ni kweli) basi jukumu lakulea familia ni lako,nini maana yakusema mvumiliane katika shida na raha??wewe siyo ajabu mwenzako akija pata kilema cha maisha ukamkimbia maana umekaa kistarehe zaidi,huyo mwenzako yupo katika hali nzito sana ya msongo wa mawazo ila kwa upeo wako mfupi umeshindwa kuelewa hilo..kwa sasa alivyo hata ukijamba ndani kwa kupumua atafikiri umemdharau,lazima ujifunze kuelewa hali aliyonayo sasa hivi.
2.Maelezo yako yanaonyesha kabisa wewe hujui majukumu yako kama mke ni yapi,unataka kutumia fursa hii ya jamaa kuwa katika kipindi kigumu kumpanda kichwani.
3.Inaonyesha kabisa una mdomo mchafu,huna kauli nzuri kwa maana yakutoelewa wakti gani uzungumze nini.
4.Wewe unaamini upo kwenye harusi na siyo ndoa.

Mwisho,wakati huu ni wakati muafaka wakumuonyesha mumeo yupo na mwanamke sahihi,yamkini MUNGU kawapitisha katika hali hiyo ili uhusiano wenu uwe imara zaidi..achana na maneno ya saloon,kaa ndani jenga ndoa yako.
Kweli kabisa uliyosema,nami nilimweleza yanayofanana na haya. Msongo wa mawazo unaweza kukufanya usijisikie fanya chochote. Sidhani kama likuwa busara kuja muumbua humu hata kama hatumjui.
 
Hivi Ladies kuolewa maana yake ni nini?

Mimi kuna vijambo vinanichosha mpaka imekuwa kero na kuona kama ndoa ni ngumu. Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa mme wangu kazi iliisha yupo nyumbani huku akiangaika kutafuta kazi sehemu zingine .

Hiyo sio big deal mie nafanya kazi thanks God kamshahara kangu kanasaidia kucover matatizo yote ya nyumbani ingawa sio kama tukiwa wawili. Kinachonichosha sana ni ratiba ya mme wangu.

Mimi nina watoto wawili wa kiume mmoja 5 years na mwingine 9 month. Mme hata mtoto akiwa analia eti yeye hawezi kumbembeleza anamwangalia tu ukimuuliza anasema yeye amfanyeje wakati hana maziwa ya kumnyonyosha, mimi hapa usiku silali mtoto anasumbua asubuhi kuamkia kazini, jioni kufika kumwangalia mtoto na kuandaa maakuli ya familia.

Nina binti anaenisaidia nikiwa kazini. Lakini mme anaamka saa nne kitanda hagusi kutandika mpaka nitoke kazini nakikuta hivyo hata net haijatolewa kutandika ndio basi tena pia hata akivua nguo za ndani atarundika hapo nije kufua mie.

Anapiga mswaki na kukaa kwenye kochi kusubiri atengenezewe chai na apelekewe, atabadilisha chanel mpaka lunch atakula atabadilisha Chanel zake baadae anawasha gari kwenda kutembea. Saa mbili au saa tatu atarudi atakula atakamata tena remote mpaka saa sita ataingia kulala na ukali sasa kitu kidogo tu manung'uniko.

Hivi jamani wanaume mkioa kazi yenu huwa inakuwa kutoa matumizi ,kula na kulala tu?

Hakuna mnachoweza kusaidia?

Ladies hivi wote mko kwenye hali hii??
Hapana, wangu anapika anafua na kufanya shughuki za usafi wa ndani na nje. Anapikia hata wageni na watoto wetu. Amewafundisha watoto wetu wote kupika. Na wanafurahia wanapoona baba yao anawapikia pia.
 
Mmeamini kuwa mwanaume asiyekuwa na hela ni mzigo usio bebeka? Anakuwa zoba hana msaada wa aina yoyote. Kero tupu.

Ushauri wangu ni kwamba. Bi dada endelea na majukumu yako kama kawaida, na wewe mkere kwa maneno ya kuudhi ili akatafute shughuli ya kufanya sio kuangalia TV. Usimpe hata shilingi yako, hata kwao kukiwa na shida inayohitaji attention yenu usijikombe kutatua.

Hakikisha watoto wako wanakula na wanapata huduma muhimu. Kuleni vizuri akirudi hiyo saa tatu mwekeeni mezani ugali na mchicha kila siku. Siku nyingine osheni masufuria akute hakuna chakula. Atatia Akili ku mkichwa.

Vitimbwi na hila zote za nini? Mlikubaliana wawili kwa hiari kukaa pamoja, ya nini leo kutafutiana presha, moyo na sukari?

Kuwa mkweli kuliko undani wote huo. Uliingia kwa hiari, toka kwa hiari pia. Kwani ni lazima kukomoana hadi mtu atoke roho ndio uone umuhimu wa kukaa peke yako? Kwa nini ung'ang'anie ndoa kihivyo, kwani dunia nzima mwanamume ni huyo tu?

Hoja kama ni hadi mtenganishwe na kifo, je, ukiwekewa panga kooni utasubiri kuchinjwa ili tamko litimie?

Inaudhi sana unapopanga mbinu za kumkomoa mtu kisa kachoka kimaisha; unafikiri bila wewe hataishi? Ni vile akili ni nywele, kila mtu ana zake; angeliujua uzi huu maneno yote yasingefikia hapa!
 
Mmeamini kuwa mwanaume asiyekuwa na hela ni mzigo usio bebeka? Anakuwa zoba hana msaada wa aina yoyote. Kero tupu.

Ushauri wangu ni kwamba. Bi dada endelea na majukumu yako kama kawaida, na wewe mkere kwa maneno ya kuudhi ili akatafute shughuli ya kufanya sio kuangalia TV. Usimpe hata shilingi yako, hata kwao kukiwa na shida inayohitaji attention yenu usijikombe kutatua.

Hakikisha watoto wako wanakula na wanapata huduma muhimu. Kuleni vizuri akirudi hiyo saa tatu mwekeeni mezani ugali na mchicha kila siku. Siku nyingine osheni masufuria akute hakuna chakula. Atatia Akili ku mkichwa.

MadameA umenichekesha sana aisee!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom