Vitendo ndani ya School buses!

Kuna shule moja jirani na ninapoishi mabasi yanaposubiri wanafunzi ni balaa ni moshi tu sijui ni bangi au sigara halafu wanawake wakipita utasikia miruzi ya tamaa za ngono sasa unategemea watoto watakuwa salama kweli kwenye mabasi:sad::sad::sad:
 
Kwanini unasema hivyo ? Ungana na jamii kupambana na vitendo vya ukatili juu ya watoto!
Hii kweli inazingua aiseh! Unajua katika uandishi kila mmoja anahakika anatunga stori ya kuvutia lakini hii kidogo iko shaghala sana, imekosa ubunifu ndio maana kama haieleweki 'iko dede'
Japo ujumbe wake umeegemea ktk maadili na ustawi wa vijana wetu wa shule za msingi na sekondari na manyanyaso wapatayo.
Jaribuni kuwa wabunifu ili tuweze kuipata pata fresh na hii husaidia michango endelevu (jengeni hoja ktk mawanda mapana kwa mtiririko unaoeleweka)
 
It is error alone which needs the support of an individual. Truth can stand by itself.
Hatuwzi wote tukawa wabunifu but kama umepata ujumbe nashukuru..
 
Story ya kutunga hii!

Obuntu huna mtoto ndiyo maana unasema hii story ni ya kutunga. Mimi nilikuwa nalipia transportation kila mwezi lakini mtoto wangu na wenzake waliokuwa wadogo siku zote walikuwa hawapati nafasi ndani ya basi kwani huwa limejaa sana na wao wadogo ndiyo wanaondolewa kwa nguvu na wakubwa. Alikuwa analalamika sana na mwisho nikaamua kuachana kabisa na usafiri ule.

Hebu fikiria mtoto mdogo anasimama kwa saa moja au zaidi kwenye basi ambalo nauli yake ni kubwa na umelipia ili kumrahisishia usafiri.

Na hayo mengine yanawezekana kabisa kuwa yanatokea kwenye mabasi haya wala si ajabu.
 
Hili ni tatizo lingine la kukurupuka. Wazazi wameona school bus ndio mwisho wa matatizo. Hajui mwanawe anachukuliwa na basi gani wala anaendeshwa na nani. Madereva bangi wanakimbiza magari ya watoto hovyo na kupita njia zingine za ajabu ajabu

Mabasi yenyewe mmeyaona? ni mikweche watoto wanalundikwa kama nyanya na bahati mbaya hakuna anayejali, sijwahi kuona basi la shule limesimamishwa na traffic police kwa sababu yoyote ile
 
mmenishtua nitakuwa nampeleka mimi mwenyewe, asante kwa kuleta mada hii!
 
Cjui wanatishiwa hawa watoto, huwa hawasemi wanayofanyiwa hadi wachunguzwe.

Mzazi mchunguze mwanao kila wakati, jenga tabia ya kuzungumza na mwanao ili asikuogope

Tatizo kubwa wanatishiwa na kuwa wafiche siri. Sasa mzazi inabidi ujue kucheza na saikolojia ya mtoto mfano kwa vitu 'sensitive' kama hivi vitendo vya unajisi usimfokee na kumtishia utampiga asiposema chochote. Hili suala la kuongea na watoto pia inategemea na mahusiano ya wazazi na watoto, je wazazi wanakuwa na muda na watoto kuongea nao hata vitu vya kawaida au kila siku wako bize wanaondoka usiku kwa usiku..

Pia watoto inabidi waelezewe kuwa hamna siri duniani ili kama ana siri aweze kukwambia japo kwenye hili pia inategemea 'approach' ya wazazi kwa watoto..

Mambo mengi yanayotokea kwa watoto kwenye jamii inayotuzunguka ni kwasababu wazazi hawapo karibu na watoto kuweza kuchunguza maisha ya kila siku ya mtoto yameendaje anapokuwa shuleni au kwenye mabasi na usafiri mwingie na vile vile hata mazingira ya nyumbani ambapo kuna vitendo vingi vichafu vinatokea dhidi ya watoto bila wazazi kufahamu.
 
Michango yote ni ya kizushi tu. Inaonekana hisia imetumika zaidi ya kuwa na hoja za msingi

Halafu kumbuka hata watoto wa dada/kaka zako ni kama wako..ikitokea bahati mbaya ukakutana na hii hali kwa mtu wako wa karibu ndiyo utatia akili. Hisia kwenye jambo kama hili ni muhimu, umeshawahi kupata picha mtoto wa miaka 2 au 3 nk akilawitiwa? au ushuhudie kabisa ndiyo utaelewa?

Vitu vingine havihitaji akili ya ziada kuelewa hata kama huna mtoto kwenye hili swala.
 
Obuntu huna mtoto ndiyo maana unasema hii story ni ya kutunga. Mimi nilikuwa nalipia transportation kila mwezi lakini mtoto wangu na wenzake waliokuwa wadogo siku zote walikuwa hawapati nafasi ndani ya basi kwani huwa limejaa sana na wao wadogo ndiyo wanaondolewa kwa nguvu na wakubwa. Alikuwa analalamika sana na mwisho nikaamua kuachana kabisa na usafiri ule.

Hebu fikiria mtoto mdogo anasimama kwa saa moja au zaidi kwenye basi ambalo nauli yake ni kubwa na umelipia ili kumrahisishia usafiri.

Na hayo mengine yanawezekana kabisa kuwa yanatokea kwenye mabasi haya wala si ajabu.
We acha tu watoto hadi watoto wanakosa hewa , wakishuka ndani ya bus hoi
 
Kweli hili ni tatizo na leo asubuhi kwa macho yangu nimeona Ki- school bus kinakimbizwa ovyo ovyo na kuyumba ndani yake kukiwa na vitoto i think ni Chekechea bahati mbaya sikuweza kufahamu ni cha shule gani. Yaani nilipatwa na mshituko! nadhani haya mabasi yaandike majina ya shule zao iwe pia rahisi kuwafuatilia.
 
Hii ni kwasababu wazazi wamekabidhi hawa malaika kwa hawa madereva na ma uncle wasio kuwa na ustaarabu.
 
.... kweli huwezi kuamini, mtoto wangu wa kike 6 years aliombwa apeleke sh 5,000 na "uncle" wa school bus. na huu ndio ulikiwa mwisho wa school buses kwangu ....

Tatizo siyo hao "uncles", tatizo ni mfumo wa usimamizi uliopo katika kila shule.

Uongozi wa shule lazima usimamie hawa watoa huduma ya usafiri, mfano wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa na walimu wawili kwa kila basi na watakuwepo vituo vya mwanzo wa safari na watakuwa wa mwisho kushuka wakati wa jioni.
 
Kwa walimu kuchukua jukumu hilo ni kuwaongezea kazi, mimi naona kama ulivyosema mfumo wa usimamizi uweze kuhakikisha kuwa badala ya ma uncles wawepo ma matron wenye uzoefu, walipwe , bora school bus money iongezwe kidogo kumeet hiyo mshahara ya mamatron
 
tumewashambulia sana ma anko wa school buses pasipo kuangalia pande zote katika sakata zima.......tumesahau kuwa wengine tunawakodishia watoto wetu TEKSI,ama hata derva wa ofisini, ama wa nyumbani.......tunasahau kuuwa...watoto wenyewe ka wenyewe, pamoja na hao wawapelekao na kuwarudisha toka shuleni....WAZAZI na WALIMU wanamchango gani katika kuhakikisha watoto wanakuwa salama....! BADO HATUJACHUKUA HATUA TUNALALAMIKA TU....!AS USUAL
 
ST. MARY'S....kesi kama hii imewahi kutokea....UONGOZI WA SHULE ukataka mzazi wa mtoto wa aliyelawitiwa (na mwanafunzi mwenzake) kutokana na usimamizi duni waelewane na mzazi mwenzake YAISHE.....!(?)
 
Umenena , wote inabidi kuangaliwa kwa mapana. Mtu yeyote unayemkabidhi awe na mwanao hata kwa dakika chache nivyema ukawa makini
 
ST. MARY'S....kesi kama hii imewahi kutokea....UONGOZI WA SHULE ukataka mzazi wa mtoto wa aliyelawitiwa (na mwanafunzi mwenzake) kutokana na usimamizi duni waelewane na mzazi mwenzake YAISHE.....!(?)

Huwa wanapenda kuyachukulia kihivyo kwa kuogopa kuwafedhehesha watoto.
Kwani one ikiwa kesi polizi bas ni public issue.
Ingewezekana kukawa na mahaka rasmi za kuhukumu kesi kama hizi
 
Tatizo lipo na ni kubwa.mara nyingi wenye mashule wana shauriwa waweka matroni mtu mzima badala ya konda wa kiume. kwa namna moja inapunguza tatizo.

Matron anasaidia. Ila kuna siku niliwahi kumuona 'matron' au dada wa shule akishuka kabla mtoto wa mwisho hajashushwa..
 
Back
Top Bottom