Kuna habari moja niliisikia mwaka jana shule moja iko Upanga kama sikosei. Kuna mtoto wa kike alikuwa wa kwanza kuchukuliwa nyumbani , wa mwisho kurudishwa. Ikafika kipindi akawa anakataa kwenda shule asubuhi. Mama yake akawa anamgombeza sana, umeshakuwa mtoto mbaya wewe, unakataa shule kwa nini (Waafrika ndivyo tulivyo, hatuna muda wa kudadisi atoto we2). Basi mwalimu wa yule mtoto akawa ameobserve changes kwa kale kabinti, mtoto hakuwa na raha hata kidogo. Akapeleleza hakupata jibu. Siku moja akawapa watoto wote darasani kipande cha karatasi. Akawaambia kila m2 aandike asichokipenda. Basi wale watoto wakaanza kuandika. Wengine waliandika hawapendi uji, wengine kuoga, malaria etc. Lakini yule mtoto akaandika sipendi "School Bus"! Mwalimu akajiuliza ni kwa nini? Coz zoezi lote lilimtarget yule mtoto. Nadhani huyu mwalimu anafahamu vizuri saikolojia ya watoto.
Basi akamwita mzazi wa yule mtoto, wakaanza kumpeleleza, wakakuta mtoto keshaharibika siku nyingi! It was too late. Jamani tuwe na mazoea ya kuwahoji watoto wetu kuhusu vitu wasivyovipenda, na wanavyovipenda na tuwafwatilie kwa makini.