Vitendo ndani ya School buses!

Tangu nimeanza kuyasikia na kuyashuhudia kama mara mbili hivi ni zaidi ya miaka minne sasa,sikujua watu bado wamelala usingizi mzito.
 
Story ya kutunga hii!
Siyo ya kutunga kuna kesi kama mbili hivi nimezisikia na moja ni ya ndugu wangu wa karibu...
Hii ishu inabidi iangaliwe kwa mapana zaidi na ikiwezekana hao watoto wawe wanasindikizwa na walimu wao hadi watakapohakikisha mtoto wa mwisho kashushwa.
 
School Bus haihitaji Koda ni Dereva tu pekee yake na Mwalimu wa zamu.Haingii akilini mtoto kufanyiwa mabaya na wazazi kukaa kimya. Tunajenga taifa gani hili?
 
Tangu nimeanza kuyasikia na kuyashuhudia kama mara mbili hivi ni zaidi ya miaka minne sasa,sikujua watu bado wamelala usingizi mzito.

Tena wa pono, je uliposikia ulijulisha jamii kwa njia yoyote shsti?
 
Siyo ya kutunga kuna kesi kama mbili hivi nimezisikia na moja ni ya ndugu wangu wa karibu...
Hii ishu inabidi iangaliwe kwa mapana zaidi na ikiwezekana hao watoto wawe wanasindikizwa na walimu wao hadi watakapohakikisha mtoto wa mwisho kashushwa.

Walimu tutawapa kazi nyingi na wapo wachache konda awe matroni alipwe hata na wazazi ikiwezekana
 
Akina siye watoto wetu wanasoma katika shule za kata.
Hiyo school bus wanaiskia tuu ila cha moto wanakiona kwenye madala dala, adha za makonda na akina Fataki.
 
Akina siye watoto wetu wanasoma katika shule za kata.
Hiyo school bus wanaiskia tuu ila cha moto wanakiona kwenye madala dala, adha za makonda na akina Fataki.

Bora hao mara mia wanapanda ndani ya daladala na wazazi wamo wanaweza kemea vitendo ovu
 
Hili ni tatizo lingine la kukurupuka. Wazazi wameona school bus ndio mwisho wa matatizo. Hajui mwanawe anachukuliwa na basi gani wala anaendeshwa na nani. Madereva bangi wanakimbiza magari ya watoto hovyo na kupita njia zingine za ajabu ajabu

Mkuu, hapo penye rangi umenigusa. Kuna watoto wa majirani zangu wanapelekwa na school bus shuleni. Jana tu nilikuwa naongelea swala hili nyumbani kwangu kuhusu mwendo kasi wa madereva wanaopeleka watoto hao. Nashauri wazazi waone hili kuwa ni tatizo nalijadiliwe katika shule.

Tuhuma za kuharibu watoto zipo na hasa wale ambao wanakuwa wa mwisho kushushwa. Niliwahi kusikia kuhusu case ambapo mtoto wa darasa la nne aliambukizwa ukimwi na dereva wa gari la shule. Parents be careful
 
Tena wa pono, je uliposikia ulijulisha jamii kwa njia yoyote shsti?

mhanga mmoja mlezi hakulinyamazia jambo hili alimfikisha mhusika kwenye vyombo vya sheria na kwa huyo mwingine nafikiri kwa kutotaka mambo yajulikane walimtafutia shule ya karibu.kwa mlezi wa kwanza maana wazazi walifariki tulishiriki kikamilifu ndugu yangu kuutokomeza uovu huu,ndio maana nashangaa kusikia bado upo.
 
Bado dear upo sana, nahuwa hautangazwi. hawa mauncle wenyewe wachafuu!
 
Michango yote ni ya kizushi tu. Inaonekana hisia imetumika zaidi ya kuwa na hoja za msingi
 
Michango yote ni ya kizushi tu. Inaonekana hisia imetumika zaidi ya kuwa na hoja za msingi

ummojawapo nini au mgumba na hauna hata moyo, maana ungekuwa na mtoto ungejua kama ni uzushi au?
 
hii si stori ya kutunga kama baadhi yetu wanavyofikiri. haya mambo yapo,baadhi yetu yameshatutokea. imefikia hatua kumzuia mwanangu asiende shule kama basi la shule halina matroni (kama hakuja siku hiyo) asubuhi lazima nilikague bus la shule kabla ya mwanangu kupanda.
So kinachoongelewa ni facts with experience.
 
Aisee this is shocking, hivi jamani tunaelekea wapi? Kila kona kunakuna na kero au tatizo! Sio huduma za jamii, fedha zetu zinaibiwa, jamani hata watoto wetu pia wanajisiwe...! This is pathetic...!
 
Back
Top Bottom