nessonlegend
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,698
- 1,514
Nimekaa na kutafakari, uchumi wa nchi upo taabani kama sio umekufa kabisa. Katika hali ya kushangaza na kufikirisha.. Imefika hatua madereva wa Bodaboda na Bajaji wanatakiwa kuwa na VITAMBULISHO VYA UJASIRIAMALI. Hii imejidhihirisha hapa Mjini Mbeya tarehe 8-2-2019 ambapo mkuu wa mkoa aliwaita madereva hao kuwaeleza umuhimu wake, na hivyo hawana budi kuwa navyo.
Maswali ni mengi kuliko majibu.....
Hivi toka lini dereva akawa mjasiriamali?
Ikatokea amegonga gari au mtu, hicho kitambulisho kinaweza kumkinga mahakamani?
Je ukiwa na kitambulisho hicho haina haja ya kuwa na leseni?
Vipi kuhusu wale madeiwaka, leo wana kazi kesho hawana, watakuwa wanakilipia kitabulisho?
Kati ya mmiliki na dereva nani awe nacho?
Kwa hali hii tusijeshangaa siku imewekwa kodi mpaka kwenye nyumba za ibada, ukitoa sadaka shilingi 1000 unakatwa shilingi 100