A
Anonymous
Guest
Ningependa kutoa kero yangu kuhusu hali ya vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufutika kwa haraka mno, na hii ni kwa vitambulisho vinavyotolewa kipindi hiki vinapoteza maandishi kwa muda mfupi tangu vitolewe hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Tofauti kubwa inaonekana kati ya vitambulisho vya awamu ya kwanza na hivi vya sasa ambavyo awali vilikuwa imara zaidi na maandishi yake yalidumu kwa muda mrefu bila kufutika. je ni kwanini ubora wa vitambulisho vya sasa umeshuka kiasi hiki??
Kama wahusika wameona tatizo hili, je wamechukua hatua gani kuhakikisha vitambulisho vinatolewa kwa ubora unaostaili? vitambilisho hivi ni nyaraka muhimu kwa utambulisho wa mtu, huduma za benki, usajili wa laini za simu, ajira na hata safari, hivyo si haki kwa wananchi kuendelea kupata usumbufu unaotokana na kasoro ambazo zinaweza kuzuilika.
Mwisho niwaulize nyie wahusika wa NIDA pamoja na mamlaka husika kuwa tatizo hili nyie mnalichukuliaje maana tayari mmesha kutana na watu wengi walio rudi kwenu kuelezea tatizo hilo ikiwa ni pamoja na mimi nakuambiwa nijaze fomu upya na kuleta loss report halafu nikalipie shs. 20,000/= ili nipewe kingine je ni hicho ndicho kinacho wafurahisha mpaka mnaendelea kutengeneza vitambulisho vyenye ubora wa chini kiasi hiki?
NIDA Tanzania
Majibu ya NIDA haya hapa ~ NIDA: Kitambulisho kikifutika kilete Mkandarasi atakichapisha upya bila malipo