Vita ya Uchumi: Bei ya mbaazi yashuka hadi kufikia Tsh.50 - Tsh.200 kwa kilo

Uongo haujawahi KAMWE kumuacha muongo salama.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amesitiza kwamba uchumi wa nchi unaendelea kukua, na kwamba wanaosema hivyo ni waongo na wazushi, na kuwataka watanzania wawapuuze.

Ndugu wananchi mliojawa na woga msiokuwa tayari kuwachukulia hatua viongozi wasiojua mbele wala nyuma ya uchumi napenda kuwapa habari mbaya za soko la mbaazi na mazao ya jamii ya kunde

Baada ya soko kunawiri msimu uliopita mpaka kufikia Tsh.2500 kwa kilo, bei katika robo hii ya mwaka imeshuka kufikia Tsh.50 mpaka Tsh.200 kwa kilo.

Jiulize mkulima unaelekea wapi,na msimu wa mvua unaotegemewa kuanza hivi karibuni utasimama wapi? Ihoji serikali yako iliyojitapa kutengeneza mazingira mazuri kwa wanunuzi wa nje na ndani pamoja na kukuza uchumi kupitia viwanda.....

Ihoji serikali nguvu inayowekeza kupambana na upinzani,Mange Kimambi,kubwatukia watumishi kwa nini isitumike kuimarisha soko la mazao?
 
Kibaya zaidi serikali ilihamasisha wakulima walime kwa wingi soko lipo kwa ahadi ya waziri mkuu wa India.Na hii ndio tatizo la masuala ya biashara kuingiza siasa.Soko la bei likiwa zuri serikali inatamba kwamba ndio chanzo mambo yakienda kombo wanakimbia.Bado bomu la korosho linakuja Tar 20 ijumaa.
 
Wala msihofu. Ni muda muafaka wa kujipanga. Kwani sisi hatuhitaji kula Mbaazi au korosho
 
Huu ni uongo wa KUTUPWA na wa kipumbavu mbaazi haijawahi wala haitawahi kuuzwa hiyo bei wala karibu na hiyo bei na kwa taarifa yako mbaazi yetu imepata soko nono Uingereza, Uarabuni na Africa Kusini wanazigombania kama njugu.

Njoo ununue sokoni kwa hiyo bei
Soko la mbaazi limeshuka,acha kupotosha. Bei iliyopo kule kusini ni chini ya Tsh 500, wakati mwaka jana waliuza angalau Tsh 2,000!
 
Huu ni uongo wa KUTUPWA na wa kipumbavu mbaazi haijawahi wala haitawahi kuuzwa hiyo bei wala karibu na hiyo bei na kwa taarifa yako mbaazi yetu imepata soko nono Uingereza, Uarabuni na Africa Kusini wanazigombania kama njugu.

Njoo ununue sokoni kwa hiyo bei
Usiongee kisiasa njo kwa wakulima vijijini uone tunavyoumia hiyo soko limesemwa juzi tu na hatuna uhakika kama zitanunuliwa. Yaani we acha kabisa tumelima lkn hata gharama za kilimo hazirudi tumerundika mbaazi store tu.
 
Huu ni uongo wa KUTUPWA na wa kipumbavu mbaazi haijawahi wala haitawahi kuuzwa hiyo bei wala karibu na hiyo bei na kwa taarifa yako mbaazi yetu imepata soko nono Uingereza, Uarabuni na Africa Kusini wanazigombania kama njugu.

Njoo ununue sokoni kwa hiyo bei
Hujielewi.unajua masoko makuu ya manunuzi ya mbaazi we.nenda afrisian,nenda vingunguti,premium agro chemistry,nenda export trading group,nenda epza..wakupe bei ya mbaazi. Mbaazi ni 440 kwa kilo na bado wahindi hawataki mzgo wanasema India Kuna surplus ya kutosha.440 kwa kilo bado usafirishaji,bado ushuru,bado gharama ya uvunaji kwa ekari.usifikir kwa hisia.
 
HONGERA CHAMA CHA ACT WAZALENDO KWA KUWASEMEA WANANCHI.
Ndugu wananchi mliojawa na woga msiokuwa tayari kuwachukulia hatua viongozi wasiojua mbele wala nyuma ya uchumi napenda kuwapa habari mbaya za soko la mbaazi na mazao ya jamii ya kunde

Baada ya soko kunawiri msimu uliopita mpaka kufikia Tsh.2500 kwa kilo, bei katika robo hii ya mwaka imeshuka kufikia Tsh.50 mpaka Tsh.200 kwa kilo.

Jiulize mkulima unaelekea wapi,na msimu wa mvua unaotegemewa kuanza hivi karibuni utasimama wapi? Ihoji serikali yako iliyojitapa kutengeneza mazingira mazuri kwa wanunuzi wa nje na ndani pamoja na kukuza uchumi kupitia viwanda.....

Ihoji serikali nguvu inayowekeza kupambana na upinzani,Mange Kimambi,kubwatukia watumishi kwa nini isitumike kuimarisha soko la mazao?
 
Kwa kweli hii ni hali ya hatari sana kwa maendeleo ya nchi na uchumi wa taifa kwa ujumla. Mamlaka inayohusika na jambo hili iliangalie kwa undani wake, fikiria mkulima anatumia muda gani hadi kufikia hatua ya kuvuna, ni muda gani anatumia kuandaa shamba hadi kuvuna, ni gharama kiasi gani ametumia kuandaa shamba hadi kuvuna kwake, harafu leo tunaambiwa ya kwamba bei imeashuka hadi 50/=hadi 200/= kutoka 2500/= ni wapi tunakompleka mkulima wa nchi hii? Je wakulima wataendela na moyo wa namna hii?
 
Mbaazi haijawahi kuuzwa hata japo 500 kwa kilo achilia mbali 200 hiyo ni siasa ya kipumbavu.

Chadema mnatakiwa mfanye siasa kwa mahesabu jf inafatiliwa mijini tu tena wanaofatilia jf hawazidi hata laki moja nchi hii tupo zaidi ya 56 million.
Wewe unanunua bei gani huki Lindi kama siyi 50? Twende hata Leo na 50 kama hujazikimbia.
 
Back
Top Bottom