The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 7,382
- 8,437
Habari ndugu wakulima wenzangu.
Leo natoa taarifa tuu ya Hadhara kwamba mjiandae kisaikolojia maana bei ya Mahindi itaenda kushuka sana.
Kenya ambayo ndio soko kuu la Mahindi ya Tanzania bei imeshuka kutoka Tsh 130,000 Kwa gunia la kilo 100 Hadi Tsh.80,000.Ikumbukwe Kenya ndio soko kuu la Mahindi ya Tanzania..
Hii imetokana na sera ya Ruto ya kuingiza mahindi ya GMO kutoka Nje ya Nchi tena bila ushuru wowote.
Aidha Msimu huu mvua zimekubali maeneo mengi ya Nchi plus mbolea ya ruzuku so mazao yatakuwa mengi sana na hivyo yatakutana na hali mbaya ya bei.
Ambae anauwezo ni kuandaa stoo vinginevyo msimu wa mavuno usije shangaa gunia kuuzwa 30,000 na wateja hakuna,maana wafanyabiashara wengi watakimbilia kwenye mchele/mpunga ambao naona bei zitashuka ila Kwa kiasi kidogo.
Nitoe wito Kwa serikali Kupitia bodi ya mazao Mchanganyiko PBZ na wakala wa Hifadhi wa Chakula NFRA chini ya Wizara ya Kilimo kutenga Bajeti ya kutosha Ili kuja kununua mazao Kwa mkulima Ili Kuokoa uzalishaji msimu utakaofuata maana mfanyabiashara hawezi nunua wakati hakuna soko.
Pia Serikali iangalie uwezekano wa kutafuta Soko Ethiopia,Sudan Kusini na Somalia Moja kwa Moja badala ya kutegemea Kenya pekee.

Unga drops: Maize prices decline by over KSh 1000 per 90kg bag
Kenyan consumers can breathe a sigh of relief following a drop in maize prices by over KSh 1,000 for a 90kg bag. Millers have filled their stores in North Rift.
www.tuko.co.ke