SoC01 Vita ya Jirani na Utalii Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
VITA YA JIRANI NA UTALII TANZANIA

Lazima tuingie gharama ili kuitangaza Tanzania na kuwavutia watalii Tanzania. Pamoja nan chi yetu kuwa na vivutio vingi vya utalii, yani vingi sana na nikivitaja hapa nitaishia kuvitaja tu hadi kuchoka kuandika, lakini ukweli ni kwamba tuna idadi ndogo ya watalii wanaokuja ndani ya nchi yetu.

Sijui kama tunaweza kupata majibu ya kwamba, je Tanzania tunaweza kwenda kufanya biding ya kuwa mwenye wa mikutano mikubwa inayofanyika duniani na tukaweza kuwalaza kwenye hotel zetu zenye hadhi ya kimataifa ndani ya mkoa mmoja mfano DSM? Nadhani sasa upo unahesabu hotel hizo ndani ya dsm, najua haujavuka 20 ambazo zinaweza kubeba watu kuanzia 100.

Tuliwahi kuwa na mkutano wa Sulvani nadhani wageni wa mkoa kwa mkoa ambao huwa hawana booking walijuta au wale wageni wa ndani mkoa(Anatoka dsm anaenda dsm) hawakupata sehemu za stahili zao.

Leo hii kuna hotel nyingi zilizokuwa na hadhi ya juu zimekufa na tumeziacha zife kwa sababu hazituhusu(Labda)

Kabla hatujatangaza vivutio lazima tujue watu hawa watalala wapi na gharama za malazi zikoje kwao. Sio watalii wote ni matajiri, wengi wana hali za kawaida kabisa na wanajibana mwaka mzima au miaka miwili ili aweze kufanya utalii kwa sababu ni asili yao wanapenda.

Huyu mtalii sio zuzu, lazima ingie kwenye mitandao na wakala wa safari ili ajue gharama kuanzia nauli, visa, malazi, chakula n.k.

Pamoja na kwamba anataka kuja kumuona Simba huko Serengeti lakini gharama za hivyo vitu vingine vikiwa juu basi ataamua kwenda kumuona Simba wa mbuga nyingine ambapo gharama hizo ni nafuu kwake.

Gharama za hotel zipo juu kwa upande wetu na sababu kubwa ni kwamba gharama za kuijenga na kuiendesha hii hotel zipo juu pia. Gharama za mikopo za ujenzi wa hizi hotels zipo juu na benki wanafanya baishara kwahiyo lazima ahakikishe anapata faida, kadhallika na mwekezaji. Hizi gharama zote zinahamia kwa mteja(Mgeni, Mtalii). Kwahiyo tukitangaza utalii wetu lazima gharama zetu kwa mtalii huyo ziwe chini ili tupate watalii wengi Zaidi.

Mwaka 2019 idaidi ya watalii Tanzania ilikuwa chini ya 2M na idaidi ya watalii Morocco ilikuwa ni 13M idadi ya watalii Kenya ilikuwa takribani 3.5M.

Ni wazi ukilinganisha vivutio na idadi ya watalii basi tuna hali mbaya.

Tukiongeza idadi ya hotel itafanya gharama za malazi kushuka na pia gharama za chakula. Tutapunguza vipi hizi gharama za hotel inabidi tuje na mpango maalum wa uwekezaji wa kwenye hotel tuuite labda HOTEL INVESTMENT FUND, ambapo serikali kupitia wizara ya Fedha au Utalii itawekeza fedha kwenye mfuko maalum kwa jili ya wawekezaji ambao wanahitaji kuwekeza kwenye hotel ili wapate mikopo hiyo kwa unafuu Zaidi na ichochee ujenzi wa hizi hotels.

Pili, tuondoe baadhi ya kodi kwenye hotel hizi hotels ili ziwe chachu ya kuwavutia wengi kuja kuwekeza kwa sababu watajikuta wanarudisha fedha zao za uwekezaji kwa haraka na kupata faida lakini itakuwa inakuza utalii.

Wastani wa hotel room standard ni TZS 150,000 hadi 300,000 lakini kwa Morocco ni wastani wa MAD400(mabapo ni TZS 70,000 hadi 250,000)

Pamoja na kwamba Mtalii atapenda Fukwe za Kwetu lakini gharama zetu zitamfukuza.

Tunapaswa kuacha kufikiri kwamba watalii ni watu matajiri sana kwahiyo kuwawekea gharama za juu ni haki yao. Tunakosea. Tushughulikie gharama zetu za utalii Tanzania.

Kuna vitu vingi vinaathiri utalii Tanzania yaani kama adui ambaye anakuja kukupiga kwako halafu anarudi kwake mfano gharama za ujenzi, na sera za kodi hawa huja kuwapiga UTALII halafu hawaonekani, wnawaachia msala utalii wenyewe wanapambana.

Suala lingine ambalo tunaweza kuamua kushughulika nalo ni michezo, nashauri kujenga viwanja vya kawaida ndani ya maeneo yetu ya vivutio. Mfano viwanja vya Mpira wa miguu na hostels zake ambapo team zinaweza kuja kuweka kambi za kimichezo.

Idadi ya watalii Rwanda inaongezeka kwa kasi kutuzidi kwa asilimia ya population na idadi hiyo wengine wanatoka Tanzania kwa sababu kuna utalii wa kujifunza mambo yanavyoenda kwa ustadi mkubwa na jinsi wanavyopiga hatua Zaidi katika mambo yao.

Tunaweza kuwapiku majirani tukitatua hii vita ya majira wa ndani dhidi ya utalii wetu wa Tanzania
 
Back
Top Bottom