Bado ni tetesi, kwamba gazeti la mwananchi itatumiwa kuchafua chadema kwa kuandika habari ambazo itawafanya wananchi kuwa na hisia mbaya na chadema,tangu wakati wa uchaguzi wa arumeru mwandishi wao mmoja alikuwa anatumia jina la bandia kwa taarifa zake,na inapangwa baada ya kuona mwananchi inawasomaji wengi......lakini mwanachi kuwa katika siasa kwa upande mmoja,inatia shaka kwa wasomaji wao hao wengi
Na ndiyo maana sasa hivi gazeti mwananchi linajikomba kwa watawala kwa kutenga kurasa za gazeti lake kutukana wapinzani.
Nataka nitofautiane kwa mbali na mashambulizi aliyofanya mhariri wa gazeti la Mwananchi dhidi ya Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nassari. Kauli aliyotoa Nassari siyo kauli mbaya kuliko zote kutolewa na kiongozi wa kisiasa kiasi cha Mhariri kutumia maelezo mengi kumdhalilisha mbunge huyu eti "alikuwa hajajipanga kuwa Mbunge". Huu ni unafiki mkubwa na chuki binafsi kwani the same gazeti kwa kipindi chote karibu mwenzi mzima wa Kampeni za ubunge huko Arumeru liliweza kusikiliza na kuripoti kampeni za Nassari vizuri kabisa na wakati mwingi kumsifia. Mwezi huo ulikuwa unatosha kueleza wanayoeleza leo kwani si rahisi kama mtu hana busara au zimtoshi kuweza kuzificha kwa mwenzi mzima. Mfano mzuri ni Livingistone Lusinde alivyodhihirisha utaalam wa matusi na utomvu wa nidhamu kwa muda mfupi alioshiriki katika kampeni. Leo hii Joshua anateleza kidogo Gazeti la mwananchi linamshambulia eti anatakiwa afundwe, na alikuwa hajajipanga kuwa mbunge. Hili gazeti nasema limetumwa na inawezekana ndio mwanzo wa kupoteza dira na heshima iliyojijengea.
Hivi ni mara ngapi mkuu wa nchi anatoa kauli mbaya na hata za iabu kuliko Nassari na hamsemi anahitaji kufundwa au hajajiandaa kuwa rais?
"Ni mara ngapi Mawaziri wanatoa kauli ambazo zinatia kichefuchefu na aibu kwa taifa na humuandiki?"
Iweje leo mtumie karibu ukurasa mzima kumshambulia Mbunge wa Arumeru.
GAZETI LA MWANANCHI LIMEKWENDA MBALI SANA KWANI MAJUMUISHO YA MHARIRI YANATAKA KUAMINISHA WASOMAJI KWAMBA NASSARI HAJUI AFANYALO, HAJATULIA, HAJAKOMAA NA HANA UWEZO WA KUONGEA MAJUKWAANI.
Mimi natofautiana nanyi kutokana na chuki binafsi mliyoonyesha kuicheza ngoma msiyoijua sawasawa.
Tido Mhando bosi wa Mwananchi alikuwa mtumishi mtiifu wa magamba kwa muda mrefu kwa hiyo gamba halijavuka vizuri kwa hiyo usishangae gazeti kupoteza muelekeo. Mbona alichoongea Nassary ni kidogo mno ukilinganishwa na yanayozungumzwa na RADIO IMAAN kila siku. Hii Radio inaongelea kuwabagua watanzania na kuwagawa mchana kweupe lakini si gazeti la Mwananchi au polisisiem waliolaani hiyo radio
Mbona JK kamteua Mbatia kutimiza yale waliyokubaliana na Cameroun kuhusu haki za "Makundi mengine" ndani ya jamii lakini hawasemi kwamba amekosea!
Mwananchi ni Gazeti makini sana Tanzania.
kwa maoni yale....mwananchi linaanza kupoteza mwelekeo
Nimeisoma hiyo habari binafsi sijaona tatizo na makala hiyo zaidi ya ushauri tena uliotolewa wakati muafaka.
Chadema ni chama kinachotarajia kuchukuwa dola na kimekuwa na mvuto hivyo watu wanakichukulia kwa uzito ndiyomàna kauli za viongozi wake zinapaswa kuwa makini sana màna watu wanazichukulia kwa uzito wake laiti kauli kama hiyo angeitoa mtu wa ccm wala isingekuwa hoja maàna wamezoea.
Kama iliwalazimu kumwandika Joshua kwa sababu za kuwa neutral je ingekuwa aliyekosea ni Tido Mhando mkurugenzi wa Mwananchi wangemweka kwenye tahariri kwa kina namna ile? Hebu Mhariri wa mwananchi try to be fair. Kwa kuandika vile ni ujumbe gani unataka kuwapa watu wa Arumeru waliomchagua Nassari?
kupambana na Nassari ni sawa na kujaribu kukinga mkuki kwa kutumia shuka.