Bikirajohola
JF-Expert Member
- Jun 11, 2022
- 356
- 632
Mkuu wa Wilaya ya Bunda (DC), Joshua Nassari ameeleza magumu anayokutana nayo katika kutekeleza majukumu yake hali inayomlazimu wakati mwingine kutoa amri ya kukamtwa kwa watu mbalimbali ambao wanaonkena kuwa kikwazo cha yeye kutumiza wajibu wake.
Akizungumza kwenye kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi kwaajili ya kuongea na makandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali mkoani Mara, Nassari amesema kuwa awali kabla hajawa mkuu wa wilaya alikuwa anawashangaa wakuu wa wilaya na mikoa waliokuwa wakitoa amri ya kuwaweka watu ndani.
"Bahati nzuri au mbaya mimi nimefanya siasa nikiwa mpinzani nilikuwa nawashangaa sana wakuu wa mikoa na wilaya waliokuwa wakitoa amri za kuwakamata watu nikawa naona kama huo sio utawala bora kumbe nilikuwa sijui kuna nini" amesema.
Nassari ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa makandarasi wawili ambao ni Nodica na CYM wanaotekeleza miradi ya barabara chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini ( Tarura) wilayani Bunda ambao wameshindwa wa kutekeleza miradi yao kwa mujibu wa mikataba hali iliyomlazimu kutoa amri ya makamdarasi hao kukamtwa na polisi.
"Huyu mzee wa CYM ni mtu mzima umri wa baba yangu lakini ilifika hatua nikaamuru awekwe ndani baada ya kushindwa kutekeleza mradi wake wa Sh300 milioni ingawa kabla ya hapo nilimtafuta nikaongea naye zaidi ya mara mbili na kumpa maelekezo nini anatakiwa kufanya lakini hakuna alichokifanya zaidi ya kuendelea kusumbua tu" amesema Nassari.
Amesema kuwa amelazimika kumzuia mkandarasi mwingine wa kampuni ya Nodica kutotoka wilayani Bunda hadi atakapokamilisha mradi wake wenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni ambao tayari upo nyuma ya muda na kwamba maamuzi hayo ameyafikia baada ya mkandarasi huyo kukaidi wito wake na hivyo kulazimika kutumia jeshi la polisi kumtafuta na kumuweka ndani.
Chanzo: Mwananchi