Vita ya Gazeti la Mwananchi na Joshua Nassari- Limekosa hoja

Siasa ni kazi kweli kweli hasa pale unapotamani kila ukifacho ama kiandikwacho juu yako basi kiwe kinakusifia tu.

Ni vyema tuwe tunajaribu kuogelea kwenye ukweli japo once in a blue moon! Haiwezekeni kila mara mtu uwe unaonekana mtakatifu tu hell no. Sometimes we have to accept critics as our friend by doing so it will help us to know our fault. Si kila lisemwalo tu tuone kana kwamba wakusemao nia yao ni mbaya.

Muanzisha thread umekiri vyema kwamba wakati wa Kampeni hili gazeti lilikuwa likimwandika Nassari vizuri labda nikuulize kwani aliyekuambia kuwa Mwananchi wameingia mkataba na Nassari ili aendelee kuandikwa vizuri ni nani?? Hilo ni moja lakini la pili nakumbuka wakati flani alishawahi kuandika Kubenea kwamba si yeye wala gazeti analoliongoza limeingia ama lina Mkataba na mtu yeyote juu ya namna ya kuandikwa mtu huyo bali wao wataandika kila kipaswacho kuanidkwa period.

Nakubaliana vyema na wengine waliosema sifa za gazeti la Mwananchi (nami ndilo gazeti langu ofcourse) na namna ambavyo wamekuwa wakiandika na kujumuisha habari zao katika ueledi wa hali ya juu na nazidi kusisitiza ifikie mahali tukubali kukosolewa ili tujue tunajipangaje. Kauli ya Nassari hakuna namna tunaweza kuitetea kama ni kuitetea sharti tuikemee ila isijirudie tena.

Nasema hatuna namna tunaweza kuitetea manake naamini kabisa Mhe. Mbowe alipoamua kusimama na kuifuta ile kauli ya kwanza kwa busara zake hakuwa kichaa wala si kwamba alikosea bali alijua athari na madhara yake katika jamii na namna ambavyo watu wanaweza kuitafsiri.

Sasa cha kushangaza tena mtu unasema wewe ni mdogo hivyo huwezi kumzui Rais. Unajua nakumbuka hadithi ya zamani nilipata kusikia jinsi Tembo alivyosumbuliwa na sisimizi jamaa wakaamua kukaa kikao sisimizi akaulizwa iikuwaje ukamwangusha Tembo sisimizi huku akicheka akajibu hivi kweli ndugu zangu na udogo huu wote mimi naweza mwangusha Tembo kweli??? Haya ndiyo anayotaka kutuaminisha Nassari??

Swala si udogo wa umri ni kauli inayotokana na ULIMI wako! Biblia imeandika Ulimi ni kiungo kidogo sana lakini madhara yake ni makubwa. Kauli huwa na athari kubwa na nzito kuliko hata umbile la mtu. Mathalan unapomtamkia mtu ntakuua haijalishi ulivyo kiumbo, kimaumbile ama tendo lenyewe bali ile nia (kama wasemavyo "actus non facit reum nisi men sit rea.")

Kwa hiyo katika hili hatuna haja ya kumumunya maneno na kuanza kutuhumu vyombo vya habari ambavyo vile vile sidhani kama vina Mkataba ama na Chama au mtu yeyote yule bali ni kumwelezea mtu ukweli ili ajipange na zaidi aweze kujirekebisha na ni uungwana kukiri kosa na kuiomba radhi jamii ili kuonesha ukovu wako kiuongozi.

Halafu napata taabu sana na namna ambavyo watu tumekuwa mstari wa mbele kufananisha kauli ya Nassari na za viongozi wengine mathalan Lusinde Nassari atabaki kuwa Nassari na ndiyo maana aliwashinda hao kina Lusinde why are we applying restrospective rules kwenye hili??

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF

MEITINYIKU L. Robinson
 
Nataka nitofautiane kwa mbali na mashambulizi aliyofanya mhariri wa gazeti la Mwananchi dhidi ya Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nassari. Kauli aliyotoa Nassari siyo kauli mbaya kuliko zote kutolewa na kiongozi wa kisiasa kiasi cha Mhariri kutumia maelezo mengi kumdhalilisha mbunge huyu eti "alikuwa hajajipanga kuwa Mbunge". Huu ni unafiki mkubwa na chuki binafsi kwani the same gazeti kwa kipindi chote karibu mwenzi mzima wa Kampeni za ubunge huko Arumeru liliweza kusikiliza na kuripoti kampeni za Nassari vizuri kabisa na wakati mwingi kumsifia. Mwezi huo ulikuwa unatosha kueleza wanayoeleza leo kwani si rahisi kama mtu hana busara au zimtoshi kuweza kuzificha kwa mwenzi mzima. Mfano mzuri ni Livingistone Lusinde alivyodhihirisha utaalam wa matusi na utomvu wa nidhamu kwa muda mfupi alioshiriki katika kampeni. Leo hii Joshua anateleza kidogo Gazeti la mwananchi linamshambulia eti anatakiwa afundwe, na alikuwa hajajipanga kuwa mbunge. Hili gazeti nasema limetumwa na inawezekana ndio mwanzo wa kupoteza dira na heshima iliyojijengea.

Hivi ni mara ngapi mkuu wa nchi anatoa kauli mbaya na hata za iabu kuliko Nassari na hamsemi anahitaji kufundwa au hajajiandaa kuwa rais?

Ni mara ngapi Mawaziri wanatoa kauli ambazo zinatia kichefuchefu na iabu kwa taifa na humuandiki?

Iweje leo mtumie karibu ukurasa mzima kumshambulia Mbunge wa Arumeru.

GAZETI LA MWANANCHI LIMEKWENDA MBALI SANA KWANI MAJUMUISHO YA MHARIRI YANATAKA KUAMINISHA WASOMAJI KWAMBA NASSARI HAJUI AFANYALO, HAJATULIA, HAJAKOMAA NA HANA UWEZO WA KUONGEA MAJUKWAANI.
Mimi natofautiana nanyi kutokana na chuki binafsi mliyoonyesha kuicheza ngoma msiyoijua sawsawa.

Acha kutetea upumbuvu. Hii tabia ya kutetea uovu kwa kulinganisha na uovu imeshakemewa sana humu janvini. Kubali Nasari alichemka na anapasa kujutia alichokisema. Anapaswa kutuomba Radhi wanachadema an watanzania wengine.

Tuwaachie viongozi wetu wawe ndo watetezi zaidi wa kauli zao chafu wanazozitoa ili waoneshe ukomavu walio nao kisiasa , tukianza kuwakingia kifua eti kwa sababu ni jamaa, ndugu, rafiki yako au kwa sababu anatoka chama unachoshabikia, hakika tunatengeneza viongozi vilaza. Hata hili la NASSARI nalo ni la kumtetea kweli? anashindwa kujitokeza mwenyewe kwenye media akatwambia msimamo wake ni nini kuhusiana na kauli yake? Tusiwalee vijana hawa kama mayai baadaye yatakuwa mayai viza.

hujasikia utetezi wa Nassari, au akina Lusinde hamjui ule usemi wa "nyani haoni....."
 
Hili gazeti linatumiwa na ZITTO na Usalama wa Taifa (AKA) ZOKA. Nani asiyejua uhusiano wa Mhariri wa gazeti hilo, Denis Msaki na Zitto? Nani asiyejua uhusiano wa MSAKI, ZOKA NA ZITO?

NANI asiyejua kuwa Zitto anataka kuonekana yeye ndiyo mwanasisa makini na bora ndani ya CDM kuliko wengine.

GAZETI LA MWANANCHI limetia aibu katika hili. Linakubali kutumiwa na watu wenye maslahi binafsi tena kwenye tahariri? Uandishi gani huu usiyofuata maadili? Vyombo vya dola vimetangaza kufanya uchunguzi juu ya matamshi ya NASARI, KABLA YA UCHUNGUZI HAUJATOKA, gazeti linaandika tahariri? Aibu!

Brother TIDO hapa unaharibu sifa yako. Je, ikiwa Nasari atafikishwa mahakamani mtaweza vipi kujitetea kuwa TAHARIRI yenu hamkushinikiza polisi kuchukua hatua hiyo? Je, akipelekwa mahakamani na akashinda kesi, mtakuwa tayari kulipa fidia kwa mliyosababisha? Mbona mnataka kutumiwa kama KONDOM kwa maslahi ya kundi fulani - ZOKA NA ZITO kupitia kwa MSAKI?

Nawasilisha.

kaka umemaliza,nataka kuamini kuwa zitto hata hukumu ya lema yupo nyuma yake,anataka aonekane star peke yake cdm..nasary kauli yako mbona ya kawaida tu.ZITTO MTU HATARI CDM.
 
Acha kutetea upumbuvu. Hii tabia ya kutetea uovu kwa kulinganisha na uovu imeshakemewa sana humu janvini. Kubali Nasari alichemka na anapasa kujutia alichokisema. Anapaswa kutuomba Radhi wanachadema an watanzania wengine.

Hujui unachokisema.
 
Nataka nitofautiane kwa mbali na mashambulizi aliyofanya mhariri wa gazeti la Mwananchi dhidi ya Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nassari. Kauli aliyotoa Nassari siyo kauli mbaya kuliko zote kutolewa na kiongozi wa kisiasa kiasi cha Mhariri kutumia maelezo mengi kumdhalilisha mbunge huyu eti "alikuwa hajajipanga kuwa Mbunge". Huu ni unafiki mkubwa na chuki binafsi kwani the same gazeti kwa kipindi chote karibu mwenzi mzima wa Kampeni za ubunge huko Arumeru liliweza kusikiliza na kuripoti kampeni za Nassari vizuri kabisa na wakati mwingi kumsifia. Mwezi huo ulikuwa unatosha kueleza wanayoeleza leo kwani si rahisi kama mtu hana busara au zimtoshi kuweza kuzificha kwa mwenzi mzima. Mfano mzuri ni Livingistone Lusinde alivyodhihirisha utaalam wa matusi na utomvu wa nidhamu kwa muda mfupi alioshiriki katika kampeni. Leo hii Joshua anateleza kidogo Gazeti la mwananchi linamshambulia eti anatakiwa afundwe, na alikuwa hajajipanga kuwa mbunge. Hili gazeti nasema limetumwa na inawezekana ndio mwanzo wa kupoteza dira na heshima iliyojijengea.

Hivi ni mara ngapi mkuu wa nchi anatoa kauli mbaya na hata za iabu kuliko Nassari na hamsemi anahitaji kufundwa au hajajiandaa kuwa rais?

Ni mara ngapi Mawaziri wanatoa kauli ambazo zinatia kichefuchefu na iabu kwa taifa na humuandiki?

Iweje leo mtumie karibu ukurasa mzima kumshambulia Mbunge wa Arumeru.

GAZETI LA MWANANCHI LIMEKWENDA MBALI SANA KWANI MAJUMUISHO YA MHARIRI YANATAKA KUAMINISHA WASOMAJI KWAMBA NASSARI HAJUI AFANYALO, HAJATULIA, HAJAKOMAA NA HANA UWEZO WA KUONGEA MAJUKWAANI.
Mimi natofautiana nanyi kutokana na chuki binafsi mliyoonyesha kuicheza ngoma msiyoijua sawsawa.

Mimi ni mmojawapo wa walihudhuria mkutano huo wa CHADEMA ambao Nasari anadaiwa kutoa kauli hizo. Kwa kiasi kikubwa kauli za Nasari zinapotoshwa na pia kuongezewa chumvi. Sijaona popote ktk magazeti yakieleza chanzo cha Nasari kutoa kauli hiyo. Mengi yamekurupuka tu. Fuatilieni kwanza habari kisha muhoji pande zote zinazohusika na sio kuandika unavyotaka au kufikiri wewe. Mwananchi limenitia kichefuchefu!!!
 
Hili ni gazeti majitaka haiwezekani mhariri kutenga kurasa maalum kushambulia chama na mtu mmoja tena kwenye suala linaloshughulikiwa kisheria.Ni gazeti lisilo hata na chembe ya kutenda haki.

Hata kama amekosea najua angekusea mtu mwingine kama EL mwananchi isingethubutu kumchmbua kihivyo kwani pale maji ni marefu. Mhariri wa Mwananchi amechukua ugeni wa kisiasa wa Joshua kumshambulia, kumsuta kana kwamba ameua ili hali ameteleza kama wanavyoteleza hata marais, viongozi wa dini n.k
 
Nataka nitofautiane kwa mbali na mashambulizi aliyofanya mhariri wa gazeti la Mwananchi dhidi ya Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nassari. Kauli aliyotoa Nassari siyo kauli mbaya kuliko zote kutolewa na kiongozi wa kisiasa kiasi cha Mhariri kutumia maelezo mengi kumdhalilisha mbunge huyu eti "alikuwa hajajipanga kuwa Mbunge". Huu ni unafiki mkubwa na chuki binafsi kwani the same gazeti kwa kipindi chote karibu mwenzi mzima wa Kampeni za ubunge huko Arumeru liliweza kusikiliza na kuripoti kampeni za Nassari vizuri kabisa na wakati mwingi kumsifia. Mwezi huo ulikuwa unatosha kueleza wanayoeleza leo kwani si rahisi kama mtu hana busara au zimtoshi kuweza kuzificha kwa mwenzi mzima. Mfano mzuri ni Livingistone Lusinde alivyodhihirisha utaalam wa matusi na utomvu wa nidhamu kwa muda mfupi alioshiriki katika kampeni. Leo hii Joshua anateleza kidogo Gazeti la mwananchi linamshambulia eti anatakiwa afundwe, na alikuwa hajajipanga kuwa mbunge. Hili gazeti nasema limetumwa na inawezekana ndio mwanzo wa kupoteza dira na heshima iliyojijengea.

Hivi ni mara ngapi mkuu wa nchi anatoa kauli mbaya na hata za iabu kuliko Nassari na hamsemi anahitaji kufundwa au hajajiandaa kuwa rais?

Ni mara ngapi Mawaziri wanatoa kauli ambazo zinatia kichefuchefu na iabu kwa taifa na humuandiki?

Iweje leo mtumie karibu ukurasa mzima kumshambulia Mbunge wa Arumeru.

GAZETI LA MWANANCHI LIMEKWENDA MBALI SANA KWANI MAJUMUISHO YA MHARIRI YANATAKA KUAMINISHA WASOMAJI KWAMBA NASSARI HAJUI AFANYALO, HAJATULIA, HAJAKOMAA NA HANA UWEZO WA KUONGEA MAJUKWAANI.
Mimi natofautiana nanyi kutokana na chuki binafsi mliyoonyesha kuicheza ngoma msiyoijua sawsawa.
Mkuu haya mawazo yako yako kishabiki wa kisiasa zaidi kuliko ufahamu wa kisiasa.

Gazeti la Mwananchi ni moja ya magazeti mahiri katika medani za kiuandishi na mara zote uandishi wake umekuwa makini.
Gazeti hili haliko biased kama magazeti kwa mfano Tanzania Daima au Uhuru katika kuandika habari.

Unajichanganya katika hii submission yako kwanza kwa kusema "Vita ya gazeti la Mwananchi na Joshua Nassari".
Hiyo vita imeanza lini?
Au ni imagination yako tu.
Na unajichanganya zaidi kwa kusema wakati wote wa kampeni gazeti la Mwananchi lilimsifia Nassari , sasa kakosea KIDOGO(are you serious?).
Mkuu, kuchezea utaifa na kuingiza vichwani mwa watu uwezekano wa Arumeru kujitenga ,kwako ni kitu kidogo?

Huku nyuma Mwananchi walimsifia, kakosea kidogo basi ni vita!
Mkuu una matatizo!

Mbaya zaidi unatukumbusha uozo wa Lusinde na kudai kama yeye(Lusinde) alitukana basi na huyu Nassari kuibua hoja ya kujitenga inabidi iwe ruksa, what an analogy.
Na hapo ndio nasema unasukumwa na upenzi kwa mtu ambaye kimsingi bado hajakomaa kama comments zako zilivyo too raw to be taken with any seriousness.
 
nataka nitofautiane kwa mbali na mashambulizi aliyofanya mhariri wa gazeti la mwananchi dhidi ya mbunge wa arumeru mh. Joshua nassari. Kauli aliyotoa nassari siyo kauli mbaya kuliko zote kutolewa na kiongozi wa kisiasa kiasi cha mhariri kutumia maelezo mengi kumdhalilisha mbunge huyu eti "alikuwa hajajipanga kuwa mbunge". Huu ni unafiki mkubwa na chuki binafsi kwani the same gazeti kwa kipindi chote karibu mwenzi mzima wa kampeni za ubunge huko arumeru liliweza kusikiliza na kuripoti kampeni za nassari vizuri kabisa na wakati mwingi kumsifia. Mwezi huo ulikuwa unatosha kueleza wanayoeleza leo kwani si rahisi kama mtu hana busara au zimtoshi kuweza kuzificha kwa mwenzi mzima. Mfano mzuri ni livingistone lusinde alivyodhihirisha utaalam wa matusi na utomvu wa nidhamu kwa muda mfupi alioshiriki katika kampeni. Leo hii joshua anateleza kidogo gazeti la mwananchi linamshambulia eti anatakiwa afundwe, na alikuwa hajajipanga kuwa mbunge. Hili gazeti nasema limetumwa na inawezekana ndio mwanzo wa kupoteza dira na heshima iliyojijengea.

Hivi ni mara ngapi mkuu wa nchi anatoa kauli mbaya na hata za iabu kuliko nassari na hamsemi anahitaji kufundwa au hajajiandaa kuwa rais?

Ni mara ngapi mawaziri wanatoa kauli ambazo zinatia kichefuchefu na iabu kwa taifa na humuandiki?

Iweje leo mtumie karibu ukurasa mzima kumshambulia mbunge wa arumeru.

Gazeti la mwananchi limekwenda mbali sana kwani majumuisho ya mhariri yanataka kuaminisha wasomaji kwamba nassari hajui afanyalo, hajatulia, hajakomaa na hana uwezo wa kuongea majukwaani.
Mimi natofautiana nanyi kutokana na chuki binafsi mliyoonyesha kuicheza ngoma msiyoijua sawsawa.

....ni kweli nassari hajakomaa kisiasa kama mwenzake lema, mbpna kina zitto,mnyika,mbowe,mdee hawajawai kutoa kauli za hivyo kwani sio wanasiasa wazuri,cdm kaeni naye huyo mtu hasije kuwaaribia chama,bado ana maziwa mdomoni,na ndo maana mbowe kasema nassari ana mawazo ya kitoto ni kweli kabisa
 
kaka umemaliza,nataka kuamini kuwa zitto hata hukumu ya lema yupo nyuma yake,anataka aonekane star peke yake cdm..nasary kauli yako mbona ya kawaida tu.ZITTO MTU HATARI CDM.

Mwishowe utaamini kua hata kukosekana kwa mvua kunatokana na Zito. Hizo habari hata hapa CHADEMA iwaonye Nassari, Heche (mhariri ni A.Kibanda mmiliki Mh. F.A. Mbowe) zimeongelewa lakini cha kushangaza umeibuka na Zito. Wanaandika wengine unawatuhumu wengine. Jaribu kubadilika chuki hazijengi badala yake zinabomoa(japo yawezekana ikawa ndo lengo lako).
 
Hili gazeti linatumiwa na ZITTO na Usalama wa Taifa (AKA) ZOKA. Nani asiyejua uhusiano wa Mhariri wa gazeti hilo, Denis Msaki na Zitto? Nani asiyejua uhusiano wa MSAKI, ZOKA NA ZITO?

NANI asiyejua kuwa Zitto anataka kuonekana yeye ndiyo mwanasisa makini na bora ndani ya CDM kuliko wengine.

GAZETI LA MWANANCHI limetia aibu katika hili. Linakubali kutumiwa na watu wenye maslahi binafsi tena kwenye tahariri? Uandishi gani huu usiyofuata maadili? Vyombo vya dola vimetangaza kufanya uchunguzi juu ya matamshi ya NASARI, KABLA YA UCHUNGUZI HAUJATOKA, gazeti linaandika tahariri? Aibu!

Brother TIDO hapa unaharibu sifa yako. Je, ikiwa Nasari atafikishwa mahakamani mtaweza vipi kujitetea kuwa TAHARIRI yenu hamkushinikiza polisi kuchukua hatua hiyo? Je, akipelekwa mahakamani na akashinda kesi, mtakuwa tayari kulipa fidia kwa mliyosababisha? Mbona mnataka kutumiwa kama KONDOM kwa maslahi ya kundi fulani - ZOKA NA ZITO kupitia kwa MSAKI?

Nawasilisha.
kwenye kauli ya Nassari zitto anaingiaje au zitto ndio alimtuma dogo janja aropoke ili kuimarisha kambi yake.? Mwananchi wapo sahihi haiwezekani kuwa na viongozi ambao hawawezi kukosolewa. Chadema wengi tunakipenda kwa kuamini ndio mkombozi wa mtanzania lakini haimaanishi viongozi wake wanapokosea wasikolewe huo sio uongozi.! Dogo janja akubali amekosea aombe msamaha kwa watanzanzia. Watanzania wanahuruma watamsamehe na itamjenga huko mbeleni kuwa ni kiongozi ambaye yupo tayari kuwajibika kwa faida ya taifa.!
 
Acha kutetea upumbuvu. Hii tabia ya kutetea uovu kwa kulinganisha na uovu imeshakemewa sana humu janvini. Kubali Nasari alichemka na anapasa kujutia alichokisema. Anapaswa kutuomba Radhi wanachadema an watanzania wengine.

Usifikiri kwa gazeti kuandika ndo kumsaidia Nassari ili aweze kuwa mbunge mwadilifu na competent. Alishaelewa aliteleza na akakiri then iweje mhariri kwa uroho tu wa kuuza gazeti anaanza kufufua habari ambayo mwenye kuitoa alisha clarify.
Mbaya zaidi kusema Nassari hana uzoefu ni sawa na kusema newly wed couple wapate uzoefu kwanza ndo waoane. Huku ni kuwakashifu watu wa Arumeru ambao tangu 2010 walitaka kumchagua.
 
Kwa hili la Nassari kwa hata sie wengine wapenda mageuzi amepotoka sana, na njia nzuri ya kumnyoosha na kumkomaza mwanasiasa ni kumkosoa tena hata kwa nchi zilizoendelea baadhi ya magazeti huwa yanawa-provoke wanasiasa makusudi wanawaona wanaweza kuongoza ili kupima uvumilivu na namna wanavyo-handle serious issues.

Sioni kwa nini Mwananchi washambuliwe......hayo ni maoni yao kama chombo cha habari kinachoheshimika kuweka tahadhari hata kama walienda hatua moja zaidi.

Gazeti la Mtanzania waliwasema na kuwakashfu akina Slaa na Mbowe kwa mambo mengi tu ya uongo kwa zaidi ya miaka 4, kama wangekasirika na kupa-nic na kuanza maneno ya piga nikupige leo wananchi wasingemuona Slaa kama mtu makini. Na sasa Mtanzania ni tofauti.

Gazeti la Mwanachi wamekuwa fair sana kwa kipindi chote hicho lakini leo wamemkosoa mtu mmoja na sio chama tunang'aka,je ingekuwa chama?

Chadema msipoteze viazi vya leo kwa ahadi ya mkate wa kesho!
 
Nassari makosea na lazima afundishwe kwa kukosolewa,tusifikiri kwa upendeleo,Mwananchi limetimiza wajibu,tusepende kupambwa siku zote ata pale tunapoteleza
 
Kweli tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya Kifikra. Yaani CCM habari nzuri ni ile inayosema "mafanikio" ya serikali yake. Na CHADEMA nao habari "nzuri" ni ile inayoishutumu CCM na serikali yake. Hivi CHADEMA au CCM huwa hawakosei?
Kuna hoja ya ajabu kabisa eti kwanini kwanza wasimseme Lusinde kabla ya kumsema Nassari!!
 
dogo ana miaka 28 he's yet to mature...mvumilieni

Kwani maturity inapimwaje? Hivi tunataka kuwafanya vijana wawe na akili za kizee namna gani?. Juhudi za mwananchi za kumfunika Nassari kwa blanketi jeusi si nzuri kwani pamoja na uhuri lazima uwe na mipaka lakini mtu kutoa comments zake ni ruksa.
 
Back
Top Bottom