Ni kweli kabisa hapa panaonekana ni ubaguzi mtupu,hivi mnataka usema Tanzania haikuwa imesaidiwa katika vile ? Kama haitoshi ni nani alikuwa akiwaonyesha WaTz njia,wakati tuliingia kule Uganda hata njia na ramani za tunakokwenda hatuna ? Ulizeni msiwe mnafuata propaganda za mpiga picha,maana vita ile nilikuwemo ndani kama mtu wa mawasiliano kuna wakati tulizachapa wenyewe kwa wenyewe kwenye nyasi ndefu,friendly fighting not fire,kama kuna kusaidiwa wakati wa ile vita basi tukubali hata Tz walikuwa na msaidizi ,tuwache ubaguzi ,kwanza tukubalianeni kuwa vita vilipiganwa kati ya Tz na Uganda maana mkisema sana wengine tunaweza kuja na hoja nzito hapa ,ili kuonyesha kuwa vita ile ilianzishwa na Tanzania na hakuna sehemu ambayo ilivamiwa na Uganda au mtabisha ?
Kama zilivyokuwa propaganda za kuivamia Iraqi ndivyo zilivyosukwa propaganda za kuivamia Uganda !! Mnashangaa kitu gani ? Au mnataka kupinga hapa tuanze kufundishana ni nani alipanga vita ile ? Afu kama mlizunguka na kuivaa Uganda mpaka kwenye mipaka ya Sudan na Zaire mbona mpaka leo kuna rasta yule mlokole
Joseph Kony anatesa na hakuna anaemuingilia katika anga zake,semeni alianza 1986 ,hivi mlisafisha kitu gani zaidi ya kuweka utawala alioutaka Nyerere pale Kampala nao ukatimuliwa na kuchawanyika hata wale mliowaweka leo hii hawajulikani wapo wapi ?
Vita ile msitake kuipamba sana maana kusema kweli hakuna sababu hata moja ya kupigana au kushiriki ila siasa za ujamaa ndizo zilizowapeleka ndugu na jamaa zetu wengi tu kupoteza maisha ,hivi kuna mtu alihoji ni waTanzania wangapi walipoteza maisha katika vita ile ? Je Serikali iliwafanyia nini wafiwa ? Je mnajua mpaka leo kuna watu hawajalipwa chochote ? Ni nani amewaulizia na kuwadaia chochote kutoka kwa serikali zinazopokezana vijiti za CCM ,wait & see once CUF ikikamata dola itahakikisha wale wote ambao hawajalipwa wanalipwa na wale ambao ndugu na jamaa zao walifariki nao wanapewa chochote ,ndio mashujaa wanavyokumbukwa sio kukaa na kuwakusanya uwanja wa Taifa mkiwacheza kwata na wengine kuwapeleka nchi za nje eti kwenda kusimamia amani na wanapopata maafa huko hakuna anaewakumbuka zaidi ya siku mbili za mwanzo ,zaidi ya viongozi tulio nao ni kujikurupusha na wakiendewa kudaiwa malipo hupiga watu tarehe.