Vita vya Kagera tulipigana na Libya (Gadafi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita vya Kagera tulipigana na Libya (Gadafi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana wa Mungu, Sep 4, 2009.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nafikiri watu wengi hapa mnakumbuka vita vya Kagera. wengi walijua tulikuwa tunampiga nduli idi amini peke yake. ila kwa wale wanaokumbuka, Gadafi ndo aliyetuma majeshi toka Libya, ambayo tulikuja kuyanyuka, nakumbuka miaka ile wanajeshi wengine walifungwa vitambaa wakapelekwa hadi kule kwa wakwe zangu Iringa, walitembezwa sokoni wakaaibishwa, wanajeshi wa kiarabu.

  Gadafi alipoona ameshindwa kumsapoti nduli idi amini, ndo akaanza kupiga kampeni kwa mataifa ya waarabu,mnakumbuka kipindi kile hata mafuta yalikuwa shida hapa kwetu kwasababu yeye alipiga kampeni kule. why did he do this, kwasababu alikuwa anataka kuexpand uislam, just because dada idi amini opss! sory, Idi amini DaDa, alikuwa mwislam.

  The same Gadafi anakuja leo kumpa kikwete zawadi za mibenzi, ili apate uenyekiti. sijui labda ilikuwa zawadi ya kawaida tu.

  Amekuja sasa, anataka Africa iungane iwe nchi moja leo..hahaha, ndoto za mchanga.

  Anataka waafrica wafunge balozi za israel leo. ndoto ya mchana.

  anataka waafrica wawe marafiki wa waarabu tu, ila si israel, ndoto ya mchana.

  anataka waafrica waelekezee uchumi wao kwa waarabu. hapo hajataja hata mataifa yaliyoendelea kama japan, china,korea kusini etc. anataka tu kwa waarabu.

  hivi hafai kupelekwa kwenye clinic ya matahira huyu, yaani kule mirembe? hivi anafikiri kila mtu anawaabudu waarabu tuuu, ati? just because someoen is an arab, basi umwabudu. sijui nisemeje kwakweli.

  na kikwete naye, anajipendekeza kwake? for what? unakumbuka walivyompokea yule gaidi juzi, mtu aliyeua watu wengi kwenye ndege? hawana hata huruma mioyoni? hivi ndivyo tulivyomchagua kikwete abehave? subiri mwakani. utakiona.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha mbali bwashee, vita vile waarabu kweli walikamatwa na wanajeshi wetu. huyu jamaa ni mtu hatari sana, na ni ajabu kwamba Tanzania inaenda naye kama rafiki. sisi hatutafunga ubalozi wa libya ile tutakuwa nao makini tu. naomba punguza munkari, usihofu, watz hatuwezi kuburuzwa naye, hata kama kikwete ataburuzwa naye, kwasababu ni msuni mwenzie.
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Unaweza kuwa na HOJA lakini ulivyoiweka umechanganya mambo mengi na mengine umepotoka sana. Nadhani haina haja hata kuijadili maana umeweka vitu vingi vya kuvuruga. Nadhani ni vyema ukai edit kama kweli unapenda mada yako ijadiliwe vyema. Uondoe element ya ubaguzi wa aina zote, ili iwe na mantiki ya kisiasa na kidiplomasia.
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Remember the Battle of Lukaya!
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini hoja ipo kwamba gadaffi anashauri waafrika waitenge Israel. Ila mimi kwa hili napendekeza tumpe israel miradi ya maji ziwa victoria atuletee maji na mto nile ukose maji ili waarabu nao watutambue kuwa tunajeuri.
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mzee acha ombaomba. Maji yapo pale kwa karne nyingi.
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Battle gani watu walikuwa wanapigana kwa virungu.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,757
  Likes Received: 4,976
  Trophy Points: 280
  ..Gaddafi alishaomba radhi na tukamrudishia mateka wa Kiarabu waliokamatwa vitani.

  ..vilevile yeye na Mwalimu walifikia kuwa marafiki na Gaddafi ametoa msaada mkubwa sana kwa Waislamu wa Butiama.

  ..pia Libya imetusaidia Tanzania kwa wakati mbalimbali.
   
 9. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Jokakuu:

  Ni afadhari umewaondolea uvuvi watu hapa. Maanake dots zingine zinaunganishwa kwa kulazimishwa sasa mpaka raha ya kuwa JF inakosekana.

  Vita vile vilikuwa kati ya Tanzania na Uganda. Na kwa bahati mbaya aliyefaidika alikuwa Mchina, Mrusi na Myugoslavia kwa sababu hao wali-supply zana za kivita pande zote mbili.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  In our standard, that was one of the toughest battle and infact it was one of defining moments for Kagera war.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,757
  Likes Received: 4,976
  Trophy Points: 280

  ..hii habari aliituma X-PASTER hapa jamii forums.   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Sep 4, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Heheheheheee....next atakuja na mambo ya Mfecane War! Companero bana.....
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hawakuwa Libya peke yao - Wapalestina na waarabu kutoka sehemu mbali mbali walishiriki katika vita kutetea mwanachama mwenzao katika OIC kushambuliwa. (Waislamu mtanisamehe) lakini ilidaiwa kuwa nchi yenye kiongozi Muislamu, Uganda, imeshambuliwa na nchi yenye kiongozi Mkristo, Tanzania. Ni Field Marshall, Dr. Al Haj Idi Amin Dada aliyeiingiza Uganda OIC mwaka 1974. Ajabu ni kwamba nchini Uganda Waislamu hawafiki asilimia kumi lakini Wakatoliki wanazidi asilimia sabini. Habari ndiyo hiyo.
   
 14. K

  Koba JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...mfecane...hahah haha haha haa wewe unaonekana somo ulilokuwa unajua ni history tuu ya darasa la sita mengine yote ulikuwa kipunga!
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Namuogopa Gadhafi sana. Ni kigeugeu sana and he always pursues his intentions wisely. Fighting the west with Arabs has become almost impossible because of some members' aliance with west eg such Saudi Arabia, Egypt and Kuwait's. Now he turns to African brothers for support. In the past he was funding those called revolutinaries and caused huge chaos in the continent. Mimi kama mimi napata shida kuamini kama ni kweli amebadilika. Najipa muda kuondoa shaka zangu
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Sep 4, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nasikia dingi yako alikuwa koplo wakati wa vita vya Amin....
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..jamani dunia imebadilika na Gaddafi hana influence yeyote na sisi na hawezi kutulazimisha chochote,na mkumbuke ana haki ya kusema chochote hata kama hatuamini ni mawazo yake...time to move on tuache blah blah za vita ya Kagera ili kuendelea kuchukia watu kama kina gaddafi hayo yalipita na alishaomba msamaha...dawa sasa ni kuwashughulikia mafisadi maana ni sumu kuliko Gadafi!
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ZK na NN tatizo lenu mko huko kwenye maboksi, wenzenu tunaadhimisha miaka 45 ya Jeshi letu sisi Wananchi. Na pia kuisha kwa Vita vya Kumtoa Nduli Idi Amini Dada. Hiyo haikuwa vita kati ya Tanzania na Uganda bali vita kati ya Wananchi Wazalendo wa Tanzania na Uganda dhidi ya Nduli.

  Majuma machache yaliyopita tuliangalia mkanda mzito kuhusu mpambano huo, hasa hilo Vagi la Lukaya lililowaacha hoi watoto wa Kanali Kadafi. Vita sio jambo la kuliombea. Ni balaa linalopaswa kuepukwa kwa njia yoyote ile. Ila ikilazimu basi tunaishia kuungana na Mwalimu wetu Mkuu kusema kwa msisitizo:

  NIA YA KUMPIGA TUNAYAYO.SABABU YA KUMPIGA TUNAYO. UWEZO WA KUMPIGA TUNAO - TUTAMPIGA...!
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Companero ana-selective nostaglia. Anakumbuka Lukaya tu lakini hakumbuki maduka yalikuwa hayana vitu baada ya vita.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Sep 4, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hilo nalo unaliita jeshi? Ungesema militia ningekusikiliza. Eti jeshi letu...ahahahahahahahaaa....mgambo tu hao ndugu
   
Loading...