Vita Vikuu vya Nafsi Yangu

Vita Vikuu vya Nafsi Yangu

de Gunner

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
10,236
Reaction score
20,390
Wakuu naombeni mnisaidie hivi mtu unashindaje vita ndani ya nafsi?

Mimi Nahisi imenishinda? Kuna vitu vimetokea maishani na siwezi kuvisahau, Kuna watu wameniumiza na siwezi kusamehe, hasa hasa kujisamehe mwenyewe.

Naona wwngine wakipitia magumu Zaid yangu ila wanakuwa Sawa na maish yanaendelea, ila kwangu imekuwa tofauti, nimetunza vitu ndani yangu kwa miaka 20 na siwezi kuvi acha. Nimejaribu meditation, nimesali sana, nimejifungia ndani kukaa na silence ila wapi.

Wakuu nifanye nini, ladha ya maisha inapotea kila siku, natembea ila mimi ni mfu nayesubiri kuzikwa tu. Nafsi yangu imekosa mwanga na nuru.

Nimeleta hii Mada ili nipate kitu cha kuondoa Maumivu, huenda mtu akaonggea jambo likaniponya, au huenda mtu akaniambia maneno machafu ili tu niache kulia Lia. Yote kheri maana ninechoka kukaa na haya Maumivu.
 
Mkuu Kwa bahati mbaya JF imekuwa sehemu mmoja toxic sana.

Sio rahisi kupata ushauri mtu ambae ana stress za kugombezwa na shemeji za kuvunja glass.

Kuwa makini utakayoambiwa humu.

Wamebakia wapuuzi humu weng
Sawa mkuu nitalizingatia hilo
 
Pole sana
Kusamehe sio rahisi kama wengi wanavyosema

Ila ujiulize mwenyewe kama huwezi kusamehe je unataka kulipa kisasi?

Kama hutaki kulipa kisasi unadhani ni nani anaeumia zaidi yako mwenyewe

Sikiliza kama utagundua kama hakuna anaejali kuhusu maumivu yako wala hisia zako utaanza kujipa mwenyewe kipaumbele na kujisamehe mwenyewe

Na kiufupi wakati unajilaumu na kujihukumu wala watu hawatojali wanaendelea na maisha yao kama kawaida

Muhimu amua kwanza kua mbinafi kujipenda wa kwanza kujikubari wa kwanza kujisamehe wa kwanza

Usije ukawaza kujiua maana hata usipo jiua kifo kiko pale pale

Kama unakuywa beer 🍺 kunywa
Choma nyama furahia maisha

Mwisho kabisa usijipe umuhimu kwa watu 🙏🙏
 
Nashukuru kwa ushauri ulio tukuka,

Inabidi nianze kujipa furaha mwenyewe.

Mawazo na mambo yalivyo tokea huko nyuma yalisha pita hata kama nitatoa visasi kama bado sijawa na upendo wa dhati kujipenda mimi haina maana.

Naomba hii komenti ikawe chapa mpya ndani ya nafsi yangu. Ni kitu rahisi sana, maamuzi ila wengi tunapoteza muda kuuliza na kutaka mtu mwingine aseme.
 
Wakuu naombeni mnisaidie hivi mtu unashindaje vita ndani ya nafsi?

Mimi Nahisi imenishinda? Kuna vitu vimetokea maishani na siwezi kuvisahau, Kuna watu wameniumiza na siwezi kusamehe, hasa hasa kujisamehe mwenyewe.

Naona wwngine wakipitia magumu Zaid yangu ila wanakuwa Sawa na maish yanaendelea, ila kwangu imekuwa tofauti, nimetunza vitu ndani yangu kwa miaka 20 na siwezi kuvi acha. Nimejaribu meditation, nimesali sana, nimejifungia ndani kukaa na silence ila wapi.

Wakuu nifanye nini, ladha ya maisha inapotea kila siku, natembea ila mimi ni mfu nayesubiri kuzikwa tu. Nafsi yangu imekosa mwanga na nuru.

Nimeleta hii Mada ili nipate kitu cha kuondoa Maumivu, huenda mtu akaonggea jambo likaniponya, au huenda mtu akaniambia maneno machafu ili tu niache kulia Lia. Yote kheri maana ninechoka kukaa na haya Maumivu.
Appetite ya kula ipo au haipo?
Kama ipo basi mambo yatakaa sawa.
 
Nashukuru kwa ushauri ulio tukuka,

Inabidi nianze kujipa furaha mwenyewe.

Mawazo na mambo yalivyo tokea huko nyuma yalisha pita hata kama nitatoa visasi kama bado sijawa na upendo wa dhati kujipenda mimi haina maana.

Naomba hii komenti ikawe chapa mpya ndani ya nafsi yangu. Ni kitu rahisi sana, maamuzi ila wengi tunapoteza muda kuuliza na kutaka mtu mwingine aseme.
Naturahi kunielewa ❤️
Fanya hivyo halafu utaona

Nyongeza tu wakati una safisha akili na roho na nafsi yako

Kua makini usiingize tena negative energy tena kuanzia sasa ukiona kitu au mtu au mazingira ya nayoweza kukurudishia kumbu kumbu mbaya za zamani epuka kabisa

Ila ila changamoto hazitakosekana ila kabiliana nazo
 
Kushinda vita ndani ya nafsi yako kunaanza kwa kukubali kwa dhati uwepo wa mapambano hayo, huku ukitambua kuwa hii ni vita ya kiroho inayohitaji silaha za kiungu na si za kibinadamu pekee.

Hatua inayofuata ni kulinda lango la akili yako kwa kuchuja kila wazo linaloingia, ukiyakataa mashaka na sauti za giza zinazokuhukumu, na badala yake kujisemea maneno ya unabii, faraja, na ushindi yanayohuisha roho yako.

Uponyaji wa kweli unahitaji ujifunze kujisamehe mwenyewe na kuachilia vinyongo dhidi ya wengine, ukijua kuwa msamaha ni ufunguo unaofungua vifungo vya kiroho vinavyozuia baraka zako na kuchosha nafsi.

Ili kulinda amani yako, ni lazima uweke mipaka madhubuti dhidi ya mazingira au watu wanaofifisha nuru yako, na badala yake utengeneze madhabahu ya utulivu moyoni mwako kupitia maombi ya dhati, kufunga, au kutafakari neno linalolisha utu wako wa ndani.

Mwishowe, unapaswa kukabidhi mapambano yako mikononi mwa Muumba na kuishi kwa imani katika wakati uliopo sasa—bila hofu ya kesho wala majuto ya jana—ukiamini kuwa nguvu ya kiungu inakupa wepesi, na pale unapohisi kuelemewa, kutafuta ushauri kwa viongozi wa kiroho au marafiki wacha Mungu kutakupa ngao ya ziada ya kushinda kabisa.
 
Cha kuongezea hakuna mtu anayejua maisha perfectly ila ni vile tunaamua kuachilia mizigo ili muda usonge kumbuka ili uweze kusonga ni lazima uachilie baadhi ya vitu moyoni mwako ikiwezekana kupoteza marafiki au watu wako wa karibu hii itakusaidia kurejesha mindset yako ya mwanzo before kuingia kwenye faulting. Kingine anza kula vyakula vinavyozalisha HAPPY HORMONES mf.fish,Almond na Aromatic foods
 
Attachments

  • Screenshot_20260529_135856_Instagram.jpg
    Screenshot_20260529_135856_Instagram.jpg
    133.3 KB · Views: 7
Naturahi kunielewa ❤️
Fanya hivyo halafu utaona

Nyongeza tu wakati una safisha akili na roho na nafsi yako

Kua makini usiingize tena negative energy tena kuanzia sasa ukiona kitu au mtu au mazingira ya nayoweza kukurudishia kumbu kumbu mbaya za zamani epuka kabisa

Ila ila changamoto hazitakosekana ila kabiliana nazo
Hakika mkuu, negative energy na spiral ya mawazo machafu ndo imekuwa changamoto kubwa kwangu. Nitalizingatia hilo.
 
Kushinda vita ndani ya nafsi yako kunaanza kwa kukubali kwa dhati uwepo wa mapambano hayo, huku ukitambua kuwa hii ni vita ya kiroho inayohitaji silaha za kiungu na si za kibinadamu pekee.

Hatua inayofuata ni kulinda lango la akili yako kwa kuchuja kila wazo linaloingia, ukiyakataa mashaka na sauti za giza zinazokuhukumu, na badala yake kujisemea maneno ya unabii, faraja, na ushindi yanayohuisha roho yako.

Uponyaji wa kweli unahitaji ujifunze kujisamehe mwenyewe na kuachilia vinyongo dhidi ya wengine, ukijua kuwa msamaha ni ufunguo unaofungua vifungo vya kiroho vinavyozuia baraka zako na kuchosha nafsi.

Ili kulinda amani yako, ni lazima uweke mipaka madhubuti dhidi ya mazingira au watu wanaofifisha nuru yako, na badala yake utengeneze madhabahu ya utulivu moyoni mwako kupitia maombi ya dhati, kufunga, au kutafakari neno linalolisha utu wako wa ndani.

Mwishowe, unapaswa kukabidhi mapambano yako mikononi mwa Muumba na kuishi kwa imani katika wakati uliopo sasa—bila hofu ya kesho wala majuto ya jana—ukiamini kuwa nguvu ya kiungu inakupa wepesi, na pale unapohisi kuelemewa, kutafuta ushauri kwa viongozi wa kiroho au marafiki wacha Mungu kutakupa ngao ya ziada ya kushinda kabisa.
Mshana ulizaliwa kuwapa maarifa wengine .... kwa jamiiforums wewe ni namba 1
 
Nashukuru Sana mkuu,
Hii komenti imejaaa madini, hekima na busara ambazo wachache katika Dunia hii uliyo jaa husda wanayo. Nitaisoma kila asubuhi niamkapo Asante sana mkuu.
Pia mimi ni Wale wahusika nilikua napinga uwepo wa Mungu, ila kila kukicha ananikumbusha mimi si kitu, majivuno na kutaka watu wengine wanipende ni kuangamiza ukuu alio weka ndani yangu.
 
Back
Top Bottom