In the end, USA will win big
Sadly
Hii vita Marekani hatashinda na ni vita ngumu sana Kwa marekani.
Sababu zangu ni hizi.
Amini usiamini nyuma ya Iran Kuna nguvu kubwa mno haitakubali Irani ianguke.
-Kuna BRICS.
-Urusi,China,Korea kaskazini.
-Kushindwa Kwa Iran ni pigo kubwa kwa Urusi na china.
-wameumia sana Maduro kutekwa
-waliumia sana Assad kuangushwa.
Urusi.
-Huyu ameptata nafasi ya kulipa kisasi Kwa marekani alichomfanyia Ukraine.
-Urusi alishasema zamani kua nae atakua anatoa silaha Kali kwa maadui wa west (USA) baada ya wao kumpa Ukraine silaha Kali,Sasa kapata mtu sahihi.
China.
-Huyu ameinvest Hela nyingi Iran.
-Amepata nafasi ya kumdhoofisha USA ili atakapoenda kuikamata Taiwan asipate upinzani mkali kutoka USA.
-amepata nafasi ya kumdhoofisha USA kiuchumi na kijeshi Ali awe na amani.
-usa amekua anaichukia sana china baada ya kuona china inakaribia kiuchumi,amekua akiiwekea china vikwazo,hivyo china amepata nafasi nae ya kumuumiza USA.
Korea kaskazini
Huyu amekua akitishiwa sana na USA Kwa sababu ya makombora yake ya masafa marefu ICBM,zuio la kumiliki nyukilia analopewa Iran hata yeye anapewa hivyo hivyo.
Kwa hiyo hayuko tayari kuona Iran inaanguka kwa sababu anajua atakae fuata ni yeye.
Kwa ujumla
Ikiwa USA alishindwa kuwashinda Watalaban ambao hawakua wanasaidiwa na nchi yoyote hapa duniani,Leo atawezaje kuwashinda Wa Iran wanaopata misaada kutoka nchi zenye nguvu kabisa kijeshi duniani?
Changamoto.
Kwa mara ya kwanza baada ya Miaka mingi sana kupita Marekani anajukuta Hana mshirika kabisa katika vita hii.
NATO wamemkatalia.
Kwa mara ya kwanza Israel haikuwahi kupigwa katika ardhi yake Kwa kipigo inachopigwa safari hii au kipindi hiki.
Vita hii kwa upande wa USA na Israel haiungwi mkono na raia zaidi ya Nusu ya Wamarekani wote,EU wote na sehemu kubwa ya Dunia.
Watu sehemu kubwa ya Dunia wanaombea USA ishindwe.
Ushahidi haijawahi kutokea katika nchi yoyote duniani Majenerali zaidi ya 12 kutokubaliana na Amiro Jeshi Mkuu wao.
Hizo sio dalili nzuri.
Ushindi pekee wa USA ni kupiga bomu la nyukilia,hata hiyo Urusi na china zimetoa onyo kwa Israel au USA zisijaribu kutumia nyukilia.