Vita dhidi ya Corona, Bunge sitisheni vikao sasa

Vita dhidi ya Corona, Bunge sitisheni vikao sasa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,060
Wamesikika kina Mwigulu bungeni wakiitisha taarifa za wagonjwa wa Corona kufichwa. Hii ni kwa manufaa ya nani?

Ndugu wabunge mnaoendelea na vikao hapo bungeni nyote kabisa bila kujali vyama vyenu hamuoni kuwa mnatusaliti sisi wananchi wenu? Mwalimu (RIP) alisema kwa hivi: "nyote nani ga nyanja".

Je ni malipo ya posho au gratuity mnazolipwa au kuzisubiria ndivyo vinavyowaweka hapo kimya na sasa mkisikia wagonjwa wanaoongezeka mnastuka kuwa zinawaharibia agenda zenu za mapato?

Mikusanyiko yote bila ya kujali jina lake kuendelea wakati huu ambapo hata mashule yamefungwa ni jambo la kushangaza na la aibu sana.

Wabunge sitisheni shughuli zenu mara moja mje tuungane sote kuhitaji hatua thabiti za kupambana na ugonjwa huu. Hizi za kumwomba Mungu ni hatua za watu binafsi ambazo haipo wala haja ya kujuzana wala kualikana.

Sauti za kuhitaji mikusanyiko yote bila kujali majina yake, kutaka zikiwamo ibada, masoko, usafiri wa umma, vikao vyovyote nk zisimame mara moja zinapaswa kupazwa vilivyo.

Msipoyafanya haya sasa hakika nyote aliyezembea ugonjwa huu ukaingia nchini na wanaoendelea kutokuchukua hatua stahiki wakati ugonjwa ukisambaa, nyote "maji ga nyanja".

Nyote kabisa, yenu yatakuwa ni yale yale. Mmetanguliza maslahi yenu peke yenu mbele wala hamna chembe ya uzalendo mioyo mwenu.

Kwani uzalendo au usaliti tuliouhubiriwa muda wote tokea shule za msingi maana yake nini?

Jitendeeni haki wenyewe na msidhani kuwa sisi wananchi hatuwaoni.

Vinginevyo you shall be there there to pay.

Hatudanganyiki!
 
Kama ukitaka kuona wabunge wa CCM na Chadema wanaungana pamoja kwa nguvu zote ongelea kuhusu suala hilo la kusitisha vikao wakati wao wanafikiria mambo ya posho zao.
 
Kama ukitaka kuona wabunge wa CCM na Chadema wanaungana pamoja kwa nguvu zote ongelea khs suala hilo la kusitisha Vikao wkt wao wanafikiria mambo ya posho zao.

Maneno yako yanathibitishwa na ukimya wao.

Haya wako kimya tuwaamini kwa yapi? Ya kwenda kumpokea Mbowe au ya kuunga mkono juhudi?

Ni vyema wakajitafakari kama kweli wako huko kwa niaba yetu.
 
Mojawapo ya kazi za wabunge ni kujadili na kupitisha bajeti na ndiyo kazi wanayofanya sasa. Unataka wasifanye kazi wewe hufanyi kazi?
 
Mojawapo ya kazi za wabunge ni kujadili na ndiyo a kupitisha bajeti na kazi wanayofanya sasa. Unataka wasifanye kazi wewe hufanyi kazi?

Ukisema "nataka" unakuwa hujanitendea haki.

Ninapendekeza watoke huko waondoe mkusanyiko. Cha muhimu sasa si bajeti tena.

Pana suala la maisha na kifo mheshimiwa mbunge.
 
Ukisema "nataka" unakuwa hujanitendea haki.

Ninapendekeza watoke huko waondoe mkusanyiko. Cha muhimu sasa si bajeti tena.

Pana suala la maisha na kifo mheshimiwa mbunge.
Bungeni hakuna msongamano
Angalia bunge utaona walivyokaa
Misongamano ipo kwenye ma dala dala, sokoni, fery, makanisani nk
 
Bungeni hakuna msongamano
Angalia bunge utaona walivyokaa
Misongamano ipo kwenye ma dala dala, sokoni, fery, makanisani nk

Mkuu hakuna niliposema msongamano. Nimesema 'mkusanyiko' kumbuka shule zimefungwa kupisha mikusanyiko si kupisha misongamano.

Mikusanyiko iko pia kwenye ibada, masoko, safiri za umma, bungeni, misiba, nk. Tushirikiane sote kuhakikisha mikusanyiko kwa jina lolote inakoma kwa sasa.

Usisahau pia ugonjwa huu ungali mgeni sana. Ajuaye fika kuhusu ugonjwa huu hapa kwetu ni yupi kama si kupambana na ukuta tu? Sisi letu hapa ilikuwa kuupiga vita siyo nitty gritty za ugonjwa huu.

Au vipi mkuu?
 
Yaani Bunge lisitishwe halafu posho zao watalipwa kama kawaida au na zenyewe zitasitishwa? Kama watalipwa basi watakubali! Ila kama zitasitishwa, aisee hao jamaa hawatakubali.

Hao jamaa wana umoja wa kipekee linapokuja suala la maslahibyao. Huwezi kumuona Mbunge wa Ccm akimpinga yule wa Chadema kwenye suala linalohusu maslahi yao.
 
Yaani Bunge lisitishwe halafu posho zao watalipwa kama kawaida au na zenyewe zitasitishwa? Kama watalipwa basi watakubali! Ila kama zitasitishwa, aisee hao jamaa hawatakubali.

Hao jamaa wana umoja wa kipekee linapokuja suala la maslahibyao. Huwezi kumuona Mbunge wa Ccm akimpinga yule wa Chadema kwenye suala linalohusu maslahi yao.

Hawa jamaa ni muhimu wakajua hivi:

1. Msukuma, na wenzio wa CCM,

2. Mdee, Lema na wenzenu wote wa upinzani,

kwenye hili la kuendelea na mikusanyiko ya vikao vya bunge hatuwaungi mkono.

Tungefarijika mno pesa zinazolipwa hapo bungeni kwa sasa zikawemo kwenye kuwaunga mkono walio wahitaji zaidi wakati nchi ikienda kwenye hatua stahiki za kuudhibiti ugonjwa huu, ya kwanza ikiwa wakazi wa dar kusalia majumbani.

Pesa zingine za kuelekezwa huku mara moja ni za ruzuku za mwezi kwa mwezi za vyama.

Hizi zikiwa hatua za mwanzoni kabla ya kufikia kwenye kukata mishahara ya watu binafsi wakiwemo wa ngazi za juu serikalini.

Mbona Kenya, Rwanda na Uganda wameweza?
 
Back
Top Bottom