Tathmini: Yanayojiri EA katika vita dhidi ya Corona

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,846
35,852
Corona ni ugonjwa hatari unaouwa na pia kuambukiza kwa haraka sana.

Study nyingi kuhusu huu ugonjwa zimetupa ufahamu wa kujua unaambukizwa vipi na kwa kiasi kikubwa kufahamu namna ya kuweza kuudhibiti.

Pana mataifa yaliyofanikiwa kabisa kuutokomeza kabisa makwao kiasi cha kuuweka msingi wa mafanikio kuwa wazi.

EU imetoa picha ya mwelekeo wa nani anaelekea kufanikiwa na nani wafanye zaidi kuboresha hali zao. Kwenye list ya EU kila nchi itavuna ilichopanda na inachopanda.

Kongole kwenu Rwanda, Zambia, na Uganda kwa hakika jitihada zenu za kiubinadanu zilizotukuka zimewalipa!

Katika ukanda wetu tunabakia sisi, wenzetu Kenya na Burundi.

Kwa takwimu zilizopo Kenya na Burundi maambukizi yangali yanaongezeka kwa kasi. Kwa Tanzania, ajuaye ni baba mola.

Kenya: mapambano yanaendelea, masomo na shughuli za mikusanyiko, kwa sasa rasmi kuendelea kusubiria hadi mwakani ili kuipa nafasi ya kupambana vilivyo na ugonjwa huu kwanza.

Ban ya EU itaendelea kuwahusu hadi pale utakapokuwapo na uthibitisho wa wazi wa kuwa wanafanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu.

Uganda na Rwanda: Mashule bado yanaendelea kufungwa na mikusanyiko inaendelea kuwa na udhibiti kiasi. Maisha mengine yameanza kurejea katika hali ya kawaida japo mipaka bado imefungwa.

EU imetambua jitihada na mafanikio yao. Hawana ban ya EU. Ni wazi kuwa kiutalii wako katika nafasi nzuri zaidi.

Burundi: jana katika kuadhimisha siku yao ya uhuru, Rais wao mpya katamka wazi kuwa awamu hii inaanza rasmi na vita dhidi ya Corona kama agenda #1. Tutegemee hatua kali kuudhibiti ugonjwa huu huko Burundi.

Aisifuye mvua basi itakuwa imemnyea vilivyo. Hawa pana kitu kizito kitakuwa kimewasibu hawa ndugu zetu hivi karibuni kuhusiana na ugonjwa huu. Pana uwezekano mkubwa kuwa kile kifo cha yule bwana mkubwa kina cha kufanya na hii mabadiliko ya moyo ya hivi sasa. Yawezekana kuwepo kwa kifo kile kunawaweka wawe na sababu na nia thabiti zaidi ya kupambana vilivyo na ugonjwa huu sasa.

Hadi pale watapothibitisha kuwa wanafaulu, EU wataendelea kuwa wanaisikia kwenye bomba peke yake.

Tanzania: huku ni kwa baba lao. Kwa baba la baba. Huku shughuli zote za masomo, mikusanyiko nk, ruksa. Kivyetu vyetu corona haipo tena!

Kivyetu vyetu kupima Corona si dili. Kwetu hupima maendeleo ya ugonjwa kwa kuulizana kwa maneno:

"Nani kauguliwa au kufiwa ndugu kwa Corona?"

Bahati mbaya bila kujali kama watu wote nchi nzima wamesikika swali hilo kwa wakati mmoja, wala kujali kama majibu nayo yamesikika yote, hitimisho hutolewa kijima jima, kama swali lilivyokuja: "Corona kwishney!"

Kwetu kupima ni mwiko na hasa kama marehemu ameshakufa tayari.

Kwa mwendelezo huu hadi beberu atakapogundua dawa, si mbaya kutambua, sisi kwa EU ni "'persona non grata." Yaani kwa kiswahili hatutakiwi kuonekana huko!

Athari zake katika utalii naamini daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu, "Mheshimiwa kabisa Kigwangala" anaweza zielezea vyema zaidi.

Hapa ndipo tulipo kama ukanda, sisi na jirani yetu mshirika mwenzetu kibiashara - mwana Chipolopolo.

Burundi makes Major U-turn on COVID-19 - Opera News Official
 
Mbona takwimu za mabeberu kuwa Tanzania imeingia katika uchumi wa kati mmeziamini?Kwa hiyo mnabagua kipi cha kuamini kipi cha kutokuamini?

Kumradhi, nilikuwa sijakusoma mkuu.

Tukisifiwa mshirika. Tukikosolewa Beberu.

Kuwa msukule ni kipaji.
 
Corona ni ugonjwa hatari unaouwa na pia kuambukiza kwa haraka sana.

Study nyingi kuhusu huu ugonjwa zimetupa ufahamu wa kujua unaambukizwa vipi na kwa kiasi kikubwa kufahamu namna ya kuweza kuudhibiti.

Pana mataifa yaliyofanikiwa kabisa kuutokomeza kabisa makwao kiasi cha kuuweka msingi wa mafanikio kuwa wazi.

EU imetoa picha ya mwelekeo wa nani anaelekea kufanikiwa na nani wafanye zaidi kuboresha hali zao. Kwenye list ya EU kila nchi itavuna ilichopanda na inachopanda.

Kongole kwenu Rwanda, Zambia, na Uganda kwa hakika jitihada zenu za kiubinadanu zilizotukuka zimewalipa!

Katika ukanda wetu tunabakia sisi, wenzetu Kenya na Burundi.

Kwa takwimu zilizopo Kenya na Burundi maambukizi yangali yanaongezeka kwa kasi. Kwa Tanzania, ajuaye ni baba mola.

Kenya: mapambano yanaendelea, masomo na shughuli za mikusanyiko, kwa sasa rasmi kuendelea kusubiria hadi mwakani ili kuipa nafasi ya kupambana vilivyo na ugonjwa huu kwanza.

Ban ya EU itaendelea kuwahusu hadi pale utakapokuwapo na uthibitisho wa wazi wa kuwa wanafanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu.

Uganda na Rwanda: Mashule bado yanaendelea kufungwa na mikusanyiko inaendelea kuwa na udhibiti kiasi. Maisha mengine yameanza kurejea katika hali ya kawaida japo mipaka bado imefungwa.

EU imetambua jitihada na mafanikio yao. Hawana ban ya EU. Ni wazi kuwa kiutalii wako katika nafasi nzuri zaidi.

Burundi: jana katika kuadhimisha siku yao ya uhuru, Rais wao mpya katamka wazi kuwa awamu hii inaanza rasmi na vita dhidi ya Corona kama agenda #1. Tutegemee hatua kali kuudhibiti ugonjwa huu huko Burundi.

Aisifuye mvua basi itakuwa imemnyea vilivyo. Hawa pana kitu kizito kitakuwa kimewasibu hawa ndugu zetu hivi karibuni kuhusiana na ugonjwa huu. Pana uwezekano mkubwa kuwa kile kifo cha yule bwana mkubwa kina cha kufanya na hii mabadiliko ya moyo ya hivi sasa. Yawezekana kuwepo kwa kifo kile kunawaweka wawe na sababu na nia thabiti zaidi ya kupambana vilivyo na ugonjwa huu sasa.

Hadi pale watapothibitisha kuwa wanafaulu, EU wataendelea kuwa wanaisikia kwenye bomba peke yake.

Tanzania: huku ni kwa baba lao. Kwa baba la baba. Huku shughuli zote za masomo, mikusanyiko nk, ruksa. Kivyetu vyetu corona haipo tena!

Kivyetu vyetu kupima Corona si dili. Kwetu hupima maendeleo ya ugonjwa kwa kuulizana kwa maneno:

"Nani kauguliwa au kufiwa ndugu kwa Corona?"

Bahati mbaya bila kujali kama watu wote nchi nzima wamesikika swali hilo kwa wakati mmoja, wala kujali kama majibu nayo yamesikika yote, hitimisho hutolewa kijima jima, kama swali lilivyokuja: "Corona kwishney!"

Kwetu kupima ni mwiko na hasa kama marehemu ameshakufa tayari.

Kwa mwendelezo huu hadi beberu atakapogundua dawa, si mbaya kutambua, sisi kwa EU ni "'persona non grata." Yaani kwa kiswahili hatutakiwi kuonekana huko!

Athari zake katika utalii naamini daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu, "Mheshimiwa kabisa Kigwangala" anaweza zielezea vyema zaidi.

Hapa ndipo tulipo kama ukanda, sisi na jirani yetu mshirika mwenzetu kibiashara - mwana Chipolopolo.
😀😀😀😀 unahangaika we endelea kupiga ramli ila lazima maisha ya endelee.

Unaona UK wanataka kurudi kule kule tulipoanzia sisi.
 
Wa jamaa unachekesha ujue, kwani EU ndio nani wewe, EU this, EU that, WTF brother?!

Inasikitisha kuwa umeshindwa kushirikisha ubongo wako kuweza kuelewa. No wonder hata umepata ujasiri wa kucheka. Uliwasikia watoto wa Nuhu waliopata ujasiri wa kumcheka baba yao aliyekuwa uchi?

Kigwangala ni EU?

Si jiwe, kabudi, wala Kigwangala faraghani wanakubaliana na ulichoandika hapo.
 
Wapi umeona ibada yoyote kwenye bandiko langu tokea pande za dongobeshi?

Kama vile haitoshi naona wanielekeza nielekee YouTube. Dongobeshi na YouTube wapi na wapi?

Dadavua ueleweke, bila kuusahau kusoma title na contents za uzi kujiridhisha kuwa bandiko lako lina relevance na uzi husika.
Kiukweli unatia uvivu, achana na huu upuuzi wa Covid-19, this topic has expired, tujadili BRT phase 3 kwenda mbagala
 
Maisha ni muhimu kuliko mali. Kimsingi mali ni upuuzi kulinganisha na maisha. Ndiyo maana misahafu inaandika:

"Ni heri ya mbwa anayeishi kuliko mfalme aliyekufa."

Ndiyo maana hata hawa machampioni wetu wamefika mahali na kushika brake kidogo kujitathmini. Pana kitu hakiko sawa:

Sweden's prime minister orders an inquiry into the failure of the country's no-lockdown coronavirus strategy
 
Back
Top Bottom