Mabibi na mabwana siyo siri kuwa kama taifa na kama wanadamu wenye kutamani kuishi, tunapita katika kipindi kigumu sana.
Katu haitusaidii hata kidogo katika kukataa kuwepo wa ugonjwa huu kwa musuli wa nguvu au ukubwa wa sauti zetu majukwaani.
Ieleweke kuwa hadi kufikia maprofesa nguli kama huyu kuvunja ukimya kwa namna hii ni ukweli ulio wazi kuwa hali si hali tena:
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21
Profesa kama huyu asiye na kuangalia maslahi ya tumbo lake peke yake ni wa kupongezwa na kuungwa mkono na wapenda maisha wote kokote kule waliko.
"Profesa Bisanda umepasua MBARIKA. Kwa hakika wewe ni mpenzi wa Mungu."
Washindwe na walegee wote wale wanaojaribu kupambana na ukweli kwa kutumia hadaa, janja janja, ghiliba, na vyote vya namna hiyo hali maisha ya watu wasiokuwa na hatia yakipotea.
Mtu kama huyu angetufaa sana kwenye ile tume ya kupambana na ugonjwa huu.
Bahati mbaya kama ilivyo sasa hivi bila shaka nia yao na ile mijamaa ni kuona kuwa anatumbuliwa.
Tumemkosea nini sisi Mungu Ya Tabia.
Ninawasilisha.