Vita dhidi ya Corona aungwe mkono Prof. Bisanda

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,677
2,000
Mabibi na mabwana siyo siri kuwa kama taifa na kama wanadamu wenye kutamani kuishi, tunapita katika kipindi kigumu sana.

Katu haitusaidii hata kidogo katika kukataa kuwepo wa ugonjwa huu kwa musuli wa nguvu au ukubwa wa sauti zetu majukwaani.

Ieleweke kuwa hadi kufikia maprofesa nguli kama huyu kuvunja ukimya kwa namna hii ni ukweli ulio wazi kuwa hali si hali tena:


Profesa kama huyu asiye na kuangalia maslahi ya tumbo lake peke yake ni wa kupongezwa na kuungwa mkono na wapenda maisha wote kokote kule waliko.

"Profesa Bisanda umepasua MBARIKA. Kwa hakika wewe ni mpenzi wa Mungu."

Washindwe na walegee wote wale wanaojaribu kupambana na ukweli kwa kutumia hadaa, janja janja, ghiliba, na vyote vya namna hiyo hali maisha ya watu wasiokuwa na hatia yakipotea.

Mtu kama huyu angetufaa sana kwenye ile tume ya kupambana na ugonjwa huu.

Bahati mbaya kama ilivyo sasa hivi bila shaka nia yao na ile mijamaa ni kuona kuwa anatumbuliwa.

Tumemkosea nini sisi Mungu Ya Tabia.

Ninawasilisha.
 

kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,706
2,000
Akwende zake Tanzania haina corona kwani kabla ya Corona watu walikua hawafi tuacheni uzwazwa mi napenda sana msimamo wa rais kuliko kuzua taharuki kwenye jamii watu wa ulaya wenyewe walikuja kujifunza kwetu kuikubali Corona na kuishi nayo saizi wana kampeni ya corona the new normal so hakuna haja ya kuzua taharuki corona itakuwepo kama TB na UKIMWI haitatumaliza ila wale wazembe watakufa.
 

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
16,864
2,000
akwende zake Tanzania haina corona kwani kabla ya Corona watu walikua hawafi tuacheni uzwazwa mi napenda sana msimamo wa rais kuliko kuzua taharuki kwenye jamii watu wa ulaya wenyewe walikuja kujifunza kwetu kuikubali Corona na kuishi nayo saizi wana kampeni ya corona the new normal so hakuna haja ya kuzua taharuki corona itakuwepo kama TB na UKIMWI haitatumaliza ila wale wazembe watakufa
Natamani huyu mdudu akutembelee...
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,146
2,000
Ijapo sijasoma alichokiandika huyu profesa,ila kama alitaka kutuambia kuwa corona ipo,na kutaka kuanza kutishana,simuungi mkono hata kidogo.

Ni ugonjwa mbaya zaidi ya kuua,unaleta unnyanyapaa wa hali ya juu.Yeye kama hamuamini Mungu achukue tahadhari.Kuna watu hata akiamua kuchukua tahadhari wala hataweza kutokana na uhalisia wa gharama zinazotakiwa.Ni muujiza tu wa Mungu unaotuacha salama.

Kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa za vitenge ni sawa na kugeuka waigizaji wa bongo muvi.Huwezi kuifanyia maigizo corona ikakuacha.Unless unaiona corona kama mungu anayestahili kuabudiwa kwa kuvaa barakoa zozote
 

scooman

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,005
2,000
Akwende zake Tanzania haina corona kwani kabla ya Corona watu walikua hawafi tuacheni uzwazwa mi napenda sana msimamo wa rais kuliko kuzua taharuki kwenye jamii watu wa ulaya wenyewe walikuja kujifunza kwetu kuikubali Corona na kuishi nayo saizi wana kampeni ya corona the new normal so hakuna haja ya kuzua taharuki corona itakuwepo kama TB na UKIMWI haitatumaliza ila wale wazembe watakufa.
Hakika wewe ni screwball kama huyo unayemuunga mkono
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
9,802
2,000
Hivi mnataka serikali ifanye nini ili muone inapambana na hili gonjwa?

Hamueleweki kabisa mnachohitaji!
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,811
2,000
Mabibi na mabwana siyo siri kuwa kama taifa na kama wanadamu wenye kutamani kuishi, tunapita katika kipindi kigumu sana...
Wasomi wenye vyeti halisi huwa wako transparent sana ila wale wababaishaji ndiyo kama huyo anayepinga, tuwaunge mkono wasomi wanaojitambua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom