passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,578
- 3,148
Kheri ya mwaka mpya wakuu?
Mimi binafsi mtaani nilipopanga na ninapoishi naitwaga mshamba na washkaji sababu nikitoka asubuhi kwenye mishe zangu kariakoo kurudi saa3 usiku au saa2 nikiwahi.
siku ya mwaka mpya hapa mtaani kuna vijana wengi walioshindwa kusoma, wasio na kujua nini wanataka kwenye maisha yao.
Hawa vijana walinunua visungura vingi sana sijui idadi kamili. Walianza kunywa mida ya saa4 usiku mpaka saa6 mwaka mpya unafika kilichokuwa kikiendelea ni kusikia tu k....ma wewe, unato...bwa na mengine mengi.
Baada ya muda kidogo tukasikia kama ugomvi tukajua kama kawaida yao, ugomvi ulipoendelea baadae tukasikia mmoja analia akasema UNANIUA!!
Kumbe yale matusi tuliyoyasikia na pombe zilizonywewa pale tayar zipo kichwani, wakawa wanabishana kuhusu mademu, mmoja mkubwa wao pale akamchoma visu vtatu tumboni.
Baada ya kuona mwenzake anagugumia maumivu dogo akakimbia na pikipiki ya jamaa mmoja pale mtaani huwa anampaga dogo deiwaka.
Kumbe pikipiki imefungwa gprs wakamkuta dogo kaanguka mtaroni na pikipiki imeharibika sababu ya ulevi kuwa mwingi kichwani.
Dogo yupo nyuma ya nondo mpaka sasa, pamoja na wenzake na mwenzao mmoja kachomwa visu na amepoteza maisha.
Naomba nitoe rai kwa vijana wenzangu, hizi kismart, visungura vinamaliza sana vijana.
sasahiv wanapewa mpaka ya kupima ili waendelee kumaliza vijana.serikali yetu tunaomba iliangalie hili hivi vidude vinamaliza vijana mitaani.
Victim wengi wakiwa ni vijana miaka kuanzia miaka15_ 25
Sikatai kweli ni starehe na nimekua nikiongea baadhi na vijana wenzangu ila nimeishiwa kuonekana mshamba.
Serikali yetu kuna vitu huwa vinapotezea lakini vijana ndio taifa la kesho, pombe ni starehe hatukatai lakini hii sasa ni harmful
Naomba vyombo husika na serikali litazame hili kwa jicho la tatu.
Nawasilisha.