Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Nina mjua sana huyu Bibi Kalembwana na waganga wengine akina mangungu

Nikiwa Maenei hayo ya kilombero Niliwahi kuona uchawi ambao sitasahau.

Kuna kijana mmoja aliombwa aangue nazi kutoka kwenye mnanzi wa mzee fulani, Jamaa akavaa kamba miguuni akapanda akashusha nazi za kutosha.

Wakati anaendelea na hararakati zake za ukwezi juu ya mnazi mara akaanguka.

Ikapigwa yowe mara majirani wakaja kuanza kusaidia jamaa akawa kafa, wakati watu wanazidi kuongezeka kwenye Tukio mara vipande vya Sabuni ya mche vikaanza kuanguka toka juu ya huo mnazi,

Watu walihisi kitu wakakausha. Next day wakazika. ni ile misiba inakuwaga na wahuni wengi wa vijiweni na stand, so wakenda wakamzika mwana.

Jamaa wakarudi kijiweni wakaanza njama za kwenda kumdifit yule mzee mwenye mnazi ambae ndie alisadikika amemchujua jamaa KIMASKHARA

Wahuni wakapanga mission mambo yakaenda.

Siku moja mzee kaamka asubuhi ana mtindo wa kuzunguka kwenye compaund yake Akatahamaki Hamaaaaad watu hawa hapa wamejaa nje.

Mshikeni mshikeni huyo asiingine ndani anaenda kuurudisha uchawi wake, mshikeni tumpeleke kwa kalembwana.

Baada ya hapo wakaagiza Guta ( Baiskeli ya pedili ya miguu mitatu) Wakamfunga na manati safari ikaanza kwenda kwa Bibi Kalembwana

Kelele zikawa kubwa mji mzima jamaa anapelekwa kwa Bibi kalembwana kwenda Kunyolewa.

Huyu ni bibi mganga alishakufa tayari, siku hizi wapo wajuu zake ndio wanafanya uganga

Yeye alikuwa mtaalam wa kuneutralize uchawi

Let say mm nimekuhisi au nimekukamata ww kuwa mchawi, basi tunatoka wote tunaenda kwa kalembwana yeye anatunyoa nywele zote, kichwani kwapani kila sehemu ananyoa hadi Vuzi, hadi Vuzy Mku.ndu anafyeka bila huruma

Kisha anakupakaa Dawa kama unga mweupe unalala hapo kwake kama siku mbili.

Pia yule alie mkamata mwenzake uchawinhuwa anatakiwa aende na kuku. Huyu kuku anachinjwa anapikwa kwa ajili ya kuliwa na wale mahasimu wawili waliopelekana kwa Bibi

Mara zote yule mchawi hawezi kula chakula. Akilenga tonge mdomoni linakimbia linaenda shavuni, yani hawezi kula kabisa,

Safari ikawa inaendela ya kwenda kwa kalembwani huku Guta linaendeshwa kwa nguvu watu wanalikimbiza nyuma

Yule mzee hakufanikiwa kuuacha uchawi wake alikuwa nao wakati anapelekwa kunyokewa

Wakati wapo njiani wamefika sehemu moja sijui kunaitwa wapi ila ni njia panda ya kwenda sijui ni wapi(Mnisahihishe) Babu akazua nongwa

Mara Guta likapata pancha safari ikawangumu wakapata sehemu wakaziba, mara mbele kidogo pancha tena, kumbe yule mzee ndio alikuwa anasababisha zile pancha kichawi

Jamaa walivyojua jua kuwa ni yeye walichuma viboko wakampiga Mbarati za kufa mtu
Akalia kinyama hadi huruma
ikabidi yule mzee kujiokoa akaiziba ile pancha kichawi mara tairi ikawa na upepo safari ikaendelea.

Wakati Wamefika karibia kwa mganga guta ikapata tena pancha. Hii ilikuwa pancha ya ukweli kabisa ya kukanyaga msumari,

Wahuni wawakujali wakampiga tena fimbo hatari mzee jinsi alivyokuwa nguli akaziba na hiyo pancha

Wakifika kwa kalembwana akaanza kuleta makeke baada ya kujulikana ni mchawi akawa hataki kunyolewa, kalembwana akasema muacheni alale atanyolewa kesho

Kesho yake akaamka akiwa kashanyokewa tayari mwili mzima na kapakazwa dawa, akaruhusiwa aondoke

Aliona aibu kurudi na watu ikabidi aende kuomba msaada kwa watu ahidhiwe akapelekwa mzee moja kwenye Mila sijui za wapogoro au wandamba wa huko kilombero na ulanga wanamuita "Mbuyi"

Huyo mbuyi ndio akamhifadhi kwake kwa siku kadhaa kisha akamsafirisha kimazingara hadi kwenye vichaka karibu na kwake

Ni wazee wa kimila huko kilombero na ulanga na malinyi.
Hawa wazee ni zaidi ya wachi.
Kwanza hawakai kwenyw nyumba za bati ni mwiko kabisa, hata akiwa na nyumba ya bati lazima atajenga ya nyasi pembeni na ataishi hapo

pia Mambuyi huwa hawavai kitu chochote mguuni. huwa wapo peku mda wote

Mbuyi akitaka kusafiri Let say Dar to Moro anatembea kidogo tuu anaingia Kichakani anapaa anaenda kutua Moro chaaap Dk. 0 Kwenye kichaka kingine anaendelea na mishe zake

Mtu yoyote alie kaa maeneo ya kilombero, Mlimba, Malinyi, Ulanga/ Mahenge lazima atakua anajua ligi za mambuyi

Mwisho.
Kuna yule msanii mtu wa Moro ambaye havaagi viatu.
Anavaa nguo za vitenge za bei mbaya lkn miguuni peku.

Kuumbeh
 
Hao wajukuu zake nasikia wengine wako sehemu moja inaitwa mwaya ukipita mahenge kwa mbele huko,wanakula hela za watu hatari,na wapogolo wa kule wanavyowaamini sasa huwaambii kitu!!
Mangungu yupo kiberege .....wakike yupo malinyi mkuu.Uncle wangu alikuwa mbui mkubwa sana alikuwa bado kijana na yeye habari kutembea peku na kuvaa kaniki muda wote pamoja kuwa na kibwenzi mbele na nyuma akaona michosho akaacha akawa anaenda church mizimu ikapita nae..alifanya kazi kipindi kifupi hila alikuwa hatari kweli kweli..Mimi nilikuwa nikienda busy na pombe ya mpunga basi sina muda kuomba dawa
 
umenikumbusha kuna mbuyi mmoja anaitwa Mateka yupo malinyi.
huyo hakai kwenye nyumba ya bati yeye anakaa kwenye ya nyasi
 
Nina mjua sana huyu Bibi Kalembwana na waganga wengine akina mangungu

Nikiwa Maenei hayo ya kilombero Niliwahi kuona uchawi ambao sitasahau.

Kuna kijana mmoja aliombwa aangue nazi kutoka kwenye mnanzi wa mzee fulani, Jamaa akavaa kamba miguuni akapanda akashusha nazi za kutosha.

Wakati anaendelea na hararakati zake za ukwezi juu ya mnazi mara akaanguka.

Ikapigwa yowe mara majirani wakaja kuanza kusaidia jamaa akawa kafa, wakati watu wanazidi kuongezeka kwenye Tukio mara vipande vya Sabuni ya mche vikaanza kuanguka toka juu ya huo mnazi,

Watu walihisi kitu wakakausha. Next day wakazika. ni ile misiba inakuwaga na wahuni wengi wa vijiweni na stand, so wakenda wakamzika mwana.

Jamaa wakarudi kijiweni wakaanza njama za kwenda kumdifit yule mzee mwenye mnazi ambae ndie alisadikika amemchujua jamaa KIMASKHARA

Wahuni wakapanga mission mambo yakaenda.

Siku moja mzee kaamka asubuhi ana mtindo wa kuzunguka kwenye compaund yake Akatahamaki Hamaaaaad watu hawa hapa wamejaa nje.

Mshikeni mshikeni huyo asiingine ndani anaenda kuurudisha uchawi wake, mshikeni tumpeleke kwa kalembwana.

Baada ya hapo wakaagiza Guta ( Baiskeli ya pedili ya miguu mitatu) Wakamfunga na manati safari ikaanza kwenda kwa Bibi Kalembwana

Kelele zikawa kubwa mji mzima jamaa anapelekwa kwa Bibi kalembwana kwenda Kunyolewa.

Huyu ni bibi mganga alishakufa tayari, siku hizi wapo wajuu zake ndio wanafanya uganga

Yeye alikuwa mtaalam wa kuneutralize uchawi

Let say mm nimekuhisi au nimekukamata ww kuwa mchawi, basi tunatoka wote tunaenda kwa kalembwana yeye anatunyoa nywele zote, kichwani kwapani kila sehemu ananyoa hadi Vuzi, hadi Vuzy Mku.ndu anafyeka bila huruma

Kisha anakupakaa Dawa kama unga mweupe unalala hapo kwake kama siku mbili.

Pia yule alie mkamata mwenzake uchawinhuwa anatakiwa aende na kuku. Huyu kuku anachinjwa anapikwa kwa ajili ya kuliwa na wale mahasimu wawili waliopelekana kwa Bibi

Mara zote yule mchawi hawezi kula chakula. Akilenga tonge mdomoni linakimbia linaenda shavuni, yani hawezi kula kabisa,

Safari ikawa inaendela ya kwenda kwa kalembwani huku Guta linaendeshwa kwa nguvu watu wanalikimbiza nyuma

Yule mzee hakufanikiwa kuuacha uchawi wake alikuwa nao wakati anapelekwa kunyokewa

Wakati wapo njiani wamefika sehemu moja sijui kunaitwa wapi ila ni njia panda ya kwenda sijui ni wapi(Mnisahihishe) Babu akazua nongwa

Mara Guta likapata pancha safari ikawangumu wakapata sehemu wakaziba, mara mbele kidogo pancha tena, kumbe yule mzee ndio alikuwa anasababisha zile pancha kichawi

Jamaa walivyojua jua kuwa ni yeye walichuma viboko wakampiga Mbarati za kufa mtu
Akalia kinyama hadi huruma
ikabidi yule mzee kujiokoa akaiziba ile pancha kichawi mara tairi ikawa na upepo safari ikaendelea.

Wakati Wamefika karibia kwa mganga guta ikapata tena pancha. Hii ilikuwa pancha ya ukweli kabisa ya kukanyaga msumari,

Wahuni wawakujali wakampiga tena fimbo hatari mzee jinsi alivyokuwa nguli akaziba na hiyo pancha

Wakifika kwa kalembwana akaanza kuleta makeke baada ya kujulikana ni mchawi akawa hataki kunyolewa, kalembwana akasema muacheni alale atanyolewa kesho

Kesho yake akaamka akiwa kashanyokewa tayari mwili mzima na kapakazwa dawa, akaruhusiwa aondoke

Aliona aibu kurudi na watu ikabidi aende kuomba msaada kwa watu ahidhiwe akapelekwa mzee moja kwenye Mila sijui za wapogoro au wandamba wa huko kilombero na ulanga wanamuita "Mbuyi"

Huyo mbuyi ndio akamhifadhi kwake kwa siku kadhaa kisha akamsafirisha kimazingara hadi kwenye vichaka karibu na kwake

Ni wazee wa kimila huko kilombero na ulanga na malinyi.
Hawa wazee ni zaidi ya wachi.
Kwanza hawakai kwenyw nyumba za bati ni mwiko kabisa, hata akiwa na nyumba ya bati lazima atajenga ya nyasi pembeni na ataishi hapo

pia Mambuyi huwa hawavai kitu chochote mguuni. huwa wapo peku mda wote

Mbuyi akitaka kusafiri Let say Dar to Moro anatembea kidogo tuu anaingia Kichakani anapaa anaenda kutua Moro chaaap Dk. 0 Kwenye kichaka kingine anaendelea na mishe zake

Mtu yoyote alie kaa maeneo ya kilombero, Mlimba, Malinyi, Ulanga/ Mahenge lazima atakua anajua ligi za mambuyi

Mwisho.
Duuh! Dunia na watu wake
 
Wakuu, kuna uzi niliwahi kuuona humu JF, nilishausahau heading(title), nakumbuka content pekee.

Content ya uzi ilikuwa inaongelea kuhusu mama zetu wazazi, asilimia mia kuwa ni wachawi lakini wakihakikisha watoto(wa kiume) hawatambui Hilo, na uchawi wao huurithisha kwa wajukuu.

Mahitaji kuurudia kuusoma, nimeutafuta kwa muda Sana lakini siupati maana hata mwandishi nilishamsahau. Uzi wenyewe niliuona around 2016-2018.

CC. Mshana Jr
Habari mkuu, ulipata title ya Uzi wenyewe naomba kuupitia kama ulifanimjwa
 
Inaendelea...SEHEMU YA NANE

Mganga; hawa wenzako ndiyo wanaokupa maradhi ili ujirudi na kukubali kumtoa mwanao kikoa ila kadri unavyokiuka kiapo na kupingana nao mwisho wa siku watakula nyama wewe.

Yule mama kwa sura ya huruma na majuto akasema kwa sauti ya chini; "naomba unisaidie baba ndio maana nimekuja kwako mwanangu.

Hapa itabidi nikuague maradhi yako kwanza lakini lazima iambatane na kufutwa muhuri au chale ya uchawi katika paji la uso wako maana hiyo ndiyo alama inayofanya wajue ulipo kirahisi lakini pia ni utambulisho, na kisha itabidi nikukinge haswa ili wasikuweze wala kukuona tena katika vipimo vyao...upo tayari? Mganga aliuliza.

Mama akajibu; "nipo tayari, baba.

Mganga; lazima ujue ukiwanga au kuroga tena utakufa maana nitakulisha usembe.

Mama; mmh haya sawa tu.

Ndugu msomaji baadae yule mama shughuli yake ilifanyika na alipata uzima na hata nyumbani kwao hali ilitulia maana inasemekana kulikuwa na vimbwanga.

Baada ya siku mbili tatu alikuja yule binti wa kisa cha kwanza, akiwa na afya njema kidogo na kushukuru kuwa hajambo ila bibi yake alipatwa na upepo wa jini na alifia kwa mganga wao wa ukoo akitibiwa.

Baada ya hapo nikafunga safari na kurudi nyumbani kwangu nikiwa nimepata kujua mengi katika ulimwengu wa giza.

MWISHO

NB.

Nimemaliza nilichotaka kueleza katika visa nilivyowahi kuviona, nimemaliza nikiwa sijachukua shilingi ya mtu kwa namna yoyote ile hivyo asije mtu akatapeliwa humu akanihusisha au kusema ni Id yangu nyingine!

Lengo langu ilikuwa ni kuchangia nilichonacho moyoni hivyo sitahusika na lawama lolote, nasema hivi kwa kuwa nimeona watu wakiombana namba za waganga na kuelekezana hivyo sitahusika na lawama lolote na pia nisifuatwe kuombwa namba ya mganga wala ushauri wa kiganga pm.

Nimetoa angalizo tangu mwanzo wa thread na sasa narudia tena maana sipendi lugha zisizofaa au kuvunjiana heshima pasi na sababu.

MUNGU ATUSAIDIE

Alamsiki.
Many thanks to you i salute ,Ahsante Tislam.
 
Back
Top Bottom