Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

Inaendelea....SEHEMU YA SABA

Ndugu wasomaji
Watu wengi wamejitokeza katika uzi huu na kueleza kwa uchungu mno mikasa ya kishirikina waliyopitia na wanayopitia sasa! Hii inaonyesha wazi uchawi upo na watu wanaumia ila hawana pa kusemea walau kutoa nyongo zao, maana jamii ya leo imejaa dhihaka na ubishi usio na maana.

Katika Jamii zetu ndipo wanapopatikana wachawi hawa na wala si chini ya ardhi, hivyo tunaishi na watu waliowatoa wenzao kafara ili wajenge majumba na kuwa na maisha mazuri, wapo watu wanaowanga, wanaoumiza wenzao kwa uchawi na hata wanaoishi kwa kutumia nyota za wengine na kufanya kila hila za kichawi.

Hivyo msishangae kuona uzi huu unapigwa vita kwa udi na uvumba na baadhi ya watu, msishangae kuona mkipingwa mnapo hadithia dhulma za kichawi zilizowakuta, mjue wazi tumegusa maslahi ya watu hivyo muwe imara katika vita hii kwa uwezo wa Mungu.

Nimepitia majaribu mengi ya kiroho tangu nianzishe uzi huu nipo ndani ya vita haswa lakini tunaendelea kama kawaida...Kazwala Mkuu ni Fupa la fuvu.

Naaam Dada yule aliongea mengi kama mtu aliye changanyikiwa kwa kuwa jambo lile la kumtoa uhai mlengwa inaonyesha alilifanya kwa hasira za ghafla bila kufikiria na pale ilionyesha yupo katika majuto makuu!

Mganga akaona isiwe tabu na kujaziwa watu ikabidi arudi chini na kum'bembeleza yule dada kwamba hilo ni jambo dogo tu atalimaliza, na hapo dada akanyamaza na kuonyesha sura ya matumaini.

Dada akapatiwa dawa kadhaa juu ya mgonjwa wake na kuambiwa asirudi mpaka ziishe kwa siku maalum alizoambiwa na dada yule akaondoka.

Mgeni huyo alipoondoka nikamuuliza mganga iwapo huyo mgonjwa atapona na akanijibu; "aah! Nimemuondoa kijanja tu ila hawezi kupona ule uchawi wa Filamoyo utamuondoa tu, ibaki Rehma za Mungu tu.

Kama nilivyosema kuwa siku ile ilianza na kazi za mikosi mikosi, baada ya muda tukapokea ugeni mwengine wa vijana watatu wenye wajihi wa kufanana...wawili wanaume na mmoja ni mwanamke wakiwa na mama mtu mzima.

Kila nikitazama ramli hapa jibu linakuja mwenye matatizo ni mmoja baina yenu na matatizo yake ni maradhi na maradhi hayo yanatokana na kuandamwa na wachawi...na mgonjwa ni huyu mama" alisema mganga baada ya kufanya vipimo.

Yule mama akadakia; "ni kweli baba nateseka mwaka wa tatu huu nyumba pia inanishinda kukaa".

Yule dada nae akadakia; "msaidie mama yaani anaumwa sana na anazidiwa zaidi usiku yaani halali ni kulia tu japo kukipambazuka ni mzima!

Mganga akawatoa nje wote na kubaki yule mama pamoja na mimi ambae nilikuwa kama mtu wa karibu kusaidia maagizo.

Mganga akamuuliza yule mama, mbona unawahangaisha wanao?

Mama akajibu; nawahangaisha vipi kwani si nimewazaa mwenyewe hawapaswi kuniuguza baba?

Akaambiwa; ngoma umeiingia mwenyewe na umekula nyama za wanachama wenzako, vipi leo hutaki kumtoa mwanao mpendwa na hufiki tena uwanjani umewaruka wenzio, unafikiri watakuacha?

Mama; kimyaaaaa!!!

Itaendelea....
Unanikumbusha mbali sana, miaka ya "90" tulikuwa tukiishi kwa mama yetu mkubwa ila alikuwa ni mganga- mwanga. Yaani huku kwake ana kilinge cha uganga ila usiku ni mwanga. Aisee uadui uliokuwepo hapo nyumbani kwake ulikuwa si wa nchi hii , mama yangu akilala usiku anawaona wachawi wanakuja kabisa chumbani na kuna siku aliamka akajikuta amechanjwa chale, zilikuwa chale mbichi na aliyemchanja alimuona kabisa ni kibibi kizee kimoja rafiki wa huyo mama mkubwa. Walikuwa wanataka kumuingiza ktk genge la wachawi bila ya yeye kujua, akaamka asubuhi akampa makavu live. Mama mkubwa alikuwa akirudi kazini (alikuwa ni muuguzi wa hospitali) anakuja na mapande ya nyama yanapikwa hapo nyumbani ila tukaja kuambiwa kuwa hizo sio nyama za ng'ombe kama tunavyoziona bali ni nyama za watu. Tuliacha kula, ikatokea mama yangu na ma mdogo wanaumwa nusu ya kufa ila tatizo ni huyo mama mkubwa, ikabidi tuhame hapo kwake , kuna mganga akawa anawatibia,akasema kuwa hilo genge la wachawi linamfuata limpe pesa "kama rushwa" ili aache kuwatibia mama zangu. Akakataa basi wakamwambia kuwa amenunua vita dhidi yao,mganga alikuja kupewa kitu kizito nae akaumwa mpk ikabidi arudi kwao kwenda kujikinga upya. Mama zangu wakatafutiwa mgangs mwingine akawatibia wakapona kwa uwezo wa Mungu...sitasahau kipindi kile. Ila yule mama mkubwa alikuja kufa kifo kibaya sana, roho yake ilitoka kwa tabu mno kwa wale waliomshuhudia wakati wa umauti wake. Ilifikia kipindi wanawe hawataki hata kwenda kumuona hospitali kipindi amelazwa , wanasubiri simu kuambiwa kuwa amefariki maana waliambiwa na mganga kuwa katika nyakati zake za mwisho anatafuta mtu wa kumuachia mikoba yake ya uchawi kwahiyo yeyote atakaekwenda kumtazama atakabidhiwa shehena hiyo ya uchawi aendeleze alipoishia. Uchawi upo tusifanye maskhara na wachawi wapo ndani ya familia zetu.
 
Anayebisha kuwa uchawi hamna namuona bado hajapitia mahangaiko,Dunia hii tunayoishi unajua kwamba kuna watu wana maono ya kuona hadi message unazochart na mtu mwingine,kuna watu wana uwezo wa kuku scan na kujua hadi pesa utayolipwa kesho,Kuna watu wana maono ya kuona kuwa huko unapoenda ni hatari na hawaendi!!!
Ongeeni tu ila haya mambo yapo aisee!!

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Wasichokijua wengi ni kuwa Waganga wa kienyeji wanatumia majini ktk kuagua na wachawi wanaotumia majini vile vile kufanya ufisadi ktk ardhi wote mkuu wao ni mmoja nae si mwingine bali ni IBLIS(laana za Mungu ziwe juu yake).

Majini (mashetani) wanapokaa katika kichwa cha mtu na kufanya nae maagano ya kumfanya awe "tabibu" huwa na lengo kuu la kuzidi kuwapotosha wanaadamu kutoka ktk njia ya Mungu yaani wawe washirikina. Kivipi wanakuwa washirikina ni pale mwanadamu anapomuendea huyo mganga kwa lengo la kutibiwa kwanza hukaribishwa na RAMLI (mganga anaelezwa matatizo ya mgonjwa na mashetani wake kisha humpa taarifa mgonjwa kuwa anasumbuliwa na hiki na kile ), hali hii mashetani huitumia ili kujenga uaminifu na utii wa mwanadamu kwao wao.Mwanadamu anajiuliza inakuwaje huyu anajua matatizo yangu ili hali sijamwambia, au anajua nilipotoka, ndugu na jamaa zangu,mahala ninapofanyia kazi n.k pasi na kumwambia?? Ni lazima atakuwa mtaalamu tu. Kitendo cha mwanadamu kuikubali RAMLI tayari anakuwa amekufuru na kuwa MSHIRIKINA. Yaani imani ya kumuamini na kumtegemea Mungu inahama na kuelekea katika imani ya kumuamini na kumtii Ibilis (shetani).

Kinachofuata hapa ni kuyatii majini ambayo huwa na sifa ya kuwa mashetani kwa kila ambacho ataamrishwa mathalani kuyatolea sadaka ya kichinjo ( kumbuka kumchinja mnyama kwa jina la Mungu ni ibada) ila sasa ibada hii inatoka kuwa ibada kwa ajili ya Mungu na kuwa ibada ya kuchinja kwa ajili ya Shetani (iblis). Huu ndio USHIRIKINA.

KWA UPANDE WA WACHAWI

Wao wachawi wameamua kukufuru kwa uwazi zaidi kwani wao tofauti ya ushirikina wao na wa mganga ni kuwa ushirikina wao hauhitaji elimu nyingi kujua kuwa wamepotoka. Wachawi wao hufanya maagano na mashetani wa kijini kuwa watayatumikia na kuyatii ktk maisha yao yote ili tu shughuli zao ziende sawa .Na mchawi anapanda cheo kila ambapo anazidisha kufuru zake na ndipo ambapo mashetani wa kijini wanapozidi kumtumikia kufanikisha mambo yake.Mfano wa kufuru kubwa wanazofanya tofauti na waganga ni kuwa mganga yeye anayatolea sadaka mashetani ,kwa kuyachinjia wanyama kama ng'ombe ,mbuzi,ngamia,kondoo au ndege kama kuku wa rangi tofauti kama nyeupe,nyeusi au nyekundu wakati mchawi yeye anayatolea sadaka kubwa mashetani kama vile kumtoa mwanawe wa kumzaa, baba,mama au nduguye wa karibu. Hapa Mashetani hufurahi zaidi maana wanajua kuwa mwanadamu anapofikia hatua hiyo ni ngumu kurudi ktk imani ya kumuamini Mungu. Baada ya kuwatolea sadaka mashetani hayo ambayo waganga huyaita "walimu", ndio hutekelezewa kazi zao kama kuagua " ambapo kiuhalisia ni hadaa tu hufanyika baina ya mashetani wa upande wa wachawi na wale wa upande wa mganga" jinsi gani wanaekeana mikataba either wale wa upande wa wachawi wamwache mgonjwa ambae ameshakufuru nae ili aendelee kukufuru kwa kuyaamini zaidi mashetani ya mganga kuwa ndio yamemponya badala ya kumuamini Mungu.
 
Uchawi hauna nguvu kwa mtu anaemuamini na kumtegemea Mungu kisawasawa. Uchawi haumdhuru mtu mpk Mungu atake kumpa mja wake mitihani ya kidunia ili aone ukweli wa imani yake.

Kuna watu wanajiona ni wachamungu ila madhara (uchawi, magonjwa, kufilisika, kufiwa na watoto wake n.k) yakiwagusa kidogo tu hugeuka na kwenda kwa waganga kuangalizia (kupiga ramli) badala ya kukaa chini na kumuomba Mungu amuondoshee madhara hayo kama alivyofanya Ayubu.

Narudia tena kila anaekwenda kwa mganga kisha akapigiwa RAMLI na akayasadiki maneno ya mganga huyo hata kama akiona yana ukweli ndani yake ajue kuwa amekufuru na amefanya SHIRKI na amekuwa MSHIRIKINA.

Yeyote aendae kwa mganga kisha akaamrishwa apeleke kitambaa cheupe,cheusi,chekundu,jogoo mweusi au wa rangi yeyote , nazi,mayai,ndimu,sindano n.k kisha akamtii mganga au shetani wa mganga huyo ajue wazi kuwa amemtii iblis na amekuwa miongoni mwa WASHIRIKINA.

Hakuna dhambi kubwa mbele ya MUNGU kama ushirikina (Shirki). Mshirikina ni mtu muovu sana mbele ya Mungu kuliko Mzinzi, mwizi au muuaji. Mungu ana wivu sana na hapendi kushirikishwa na chochote au yeyote ktk ibada zake. Mtu ukifa hali ya kuwa ni mshirikina basi jichagulie makazi yako kabisa ndani ya moto wa jahannam.

Mungu atuepushe dhidi ya ushirikina ameen
 
nikuongezee mimea aina hio kuna mkunde pori pia ni kiboko huo mti hasa kama mnakokaa kuna viumbe wabaya na wamasumbua mtoto mchanga chukua majani mfikichie mtoto na mama yake ajifikichie hasa maziwa anayomnyonyeshea

ila baba lao ni mvuje, huo hasogei mtu mbaya wala kiumbe yoyote mbaya na inashauriwa sana mama anapojifungua amfunge mtoto kidonge mkononi na asikifungue mpaka kidondoke chenyewe ikiwa kitandoka ukakiona mvishe tena mpaka kiishe ikiwa hutakiona na bado mtoto mdogo mfunge mwengine au kiroweke na maji kina harufu mbaya sana mpake pake hayo maji
Mvuje (curry leaves) hauna harufu mbaya, majani yake ni kiungo kizuri sana kwenye michuzi. Huleta ladha na harufu nzuri kwenye mchuzi.
 
Hapa kuna elimu kubwa inahitajika.

Kwa ufupi
1. Wewe ndiye humpa nguvu zako mchawi ili akuroge. Ila hana nguvu za kukuroga labda akulishe madawa.
2. Mchawi huitumia nguvu ya Mungu kutenda huo uovu kama wewe unavyoweza kutumia nguvu ya Mungu kuiba au kuzini. (Roho)
3. Mungu katupatia uchaguzi wanadamu wa namna ya kuitumia nguvu yake. Kwa hiyo itumie vyema na atakuja kuhukumu na kuadhibu kwa wale walioitumia vibaya.

Kwa ufupi sana.
 
Hapa kuna elimu kubwa inahitajika.

Kwa ufupi
1. Wewe ndiye humpa nguvu zako mchawi ili akuroge. Ila hana nguvu za kukuroga labda akurishe madawa.
2. Mchawi huitumia nguvu ya Mungu kutenda huo uovu kama wewe unavyoweza kutumia nguvu ya Mungu kuiba au kuzini. (Roho)

Kwa ufupi sana.
Wasichokijua wanadamu wengi ni kuwa kila mwanadamu toka anazaliwa huwa ana rafiki wa kijini anaambatana bae maisha yake yote.Huyu ndie anaejua mambo yako yote,siri zako na mipangilio yako, ili ramli ya mganga ifanikiwe ni lazima mashetani wa mganga wawasiliane na shetani huyo unayeambatana nae...yeye ndie hutoa taarifa zako kwao na wao huzipitisha kwa mganga "kiti wao" ambae anakueleza wewe kuwa umekuja kwake una tatizo hili na lile. Ni mawasiliano tu ya kijini hufanyika na kwavile sisi tumewekewa pazia hatuwaoni basi tunayaona mashetani hayo ya kijini yanajua kila kitu ilihali hakuna ajuae ghayb (yaliyofichikana) isipokuwa Mungu peke yake.Hawa mashetani wanajua tu mambo ambayo yameshafanyika ila hawana uwezo wa kujua hata jambo litakalotokea dk moja baadae.

Na mara nyingi hutoa ramli chonganishi ili ndugu kwa ndugu wahasimiane au mtoto na mzazi wake wafarakane au mume na mke waachane au mtu na jirani yake wahasimiane.
 
Wasichokijua wanadamu wengi ni kuwa kila mwanadamu toka anazaliwa huwa ana rafiki wa kijini anaambatana bae maisha yake yote.Huyu ndie anaejua mambo yako yote,siri zako na mipangilio yako, ili ramli ya mganga ifanikiwe ni lazima mashetani wa mganga wawasiliane na shetani huyo unayeambatana nae...yeye ndie hutoa taarifa zako kwao na wao huzipitisha kwa mganga "kiti wao" ambae anakueleza wewe kuwa umekuja kwake una tatizo hili na lile. Ni mawasiliano tu ya kijini hufanyika na kwavile sisi tumewekewa pazia hatuwaoni basi tunayaona mashetani hayo ya kijini yanajua kila kitu ilihali hakuna ajuae ghayb (yaliyofichikana) isipokuwa Mungu peke yake.Hawa mashetani wanajua tu mambo ambayo yameshafanyika ila hawana uwezo wa kujua hata jambo litakalotokea dk moja baadae.

Na mara nyingi hutoa ramli chonganishi ili ndugu kwa ndugu wahasimiane au mtoto na mzazi wake wafarakane au mume na mke waachane au mtu na jirani yake wahasimiane.
Hapa dunia kila kitu kimeungana na kingine kiroho. Usishangae mganga akajua mambo yako kwani hiyo nguvu unayoisema ameungana nayo.

Wengi wasichojua ni kwamba pale unapoamini jambo fulani kuwa kweli unakuwa sehemu ya jambo hilo hapo utaona kila jambo duniani lianendana na hiyo imani yako. Amini uchawi utaunganisha na mambo ya kichawi na utauona ulimwengu wa wachawi katika kila jambo. Ndio maana utashangaa mnakaa mtaa mmoja huyu anasubuliwa na wachawi mwingine hapana.
 
Sasa tunatambua kiroho zaidi kila kitu ni kimoja haijalishi ni kibaya au kizuri. Ubaya na uzuri ni maneno tu yaliyowekwa kuwakilisha matokeo ya kile afanyacho binadamu. Ikiwa yanafaa kwa matumizi ya binadamu basi ni mema na kinyume chake ni maovu au mabaya. Lakini jiulize nini kinatangulia matendo? Sasa utaelewa kwanini wachawi unawapa nguvu za kukuroga au waganga kukueleza mambo yako kabla haujasema.

Waganga na wachawi wapo mbele (adavnced) zaidi katika ulimwengu wa roho kushinda hata maaskofu, wachungaji, masheikh, maalim, mapadri, makasisi na wengine walio wengi. Wanaitumia vizuri elimu hiyo kwani wanarithishana kwa vitendo zaidi ya nadharia. Muulizeni Mshana Jr na wengine watakufahamosheni.

Tuepuke kutoa nguvu zetu kwa wachawi.
 
Sasa tunatambua kiroho zaidi kila kitu ni kimoja haijalishi ni kibaya au kizuri. Ubaya na uzuri ni maneno tu yaliyowekwa kuwakilisha matokeo ya kile afanyacho binadamu. Ikiwa yanafaa kwa matumizi ya binadamu basi ni mema na kinyume chake ni maovu au mabaya. Lakini jiulize nini kinatangulia matendo? Sasa utaelewa kwanini wachawi unawapa nguvu za kukuroga au waganga kukueleza mambo yako kabla haujasema.

Waganga na wachawi wapo mbele (adavnced) zaidi katika ulimwengu wa roho kushinda hata maaskofu, wachungaji, masheikh, maalim, mapadri, makasisi na wengine walio wengi. Wanaitumia vizuri elimu hiyo kwani wanarithishana kwa vitendo zaidi ya nadharia. Muulizeni Mshana Jr na wengine watakufahamosheni.

Tuepuke kutoa nguvu zetu kwa wachawi.
Hakuna ukweli wowote kuwa wachawi wapo mbele katika ulimwengu wa kiroho kuliko wachamungu.

Mchawi yeyote anaishi maisha ya kitumwa katika uhai wake wote ,anaishi kwa kuyatumikia mashetani ambayo yana demand afanye kufuru kila uchwao. Ni maisha dhalili na ya tabu sana kuliko watu wanavyodhani.Wachawi wanaishi maisha ya dhiki sana hapa duniani na hawana amani ya moyo.
 
Hakuna ukweli wowote kuwa wachawi wapo mbele katika ulimwengu wa kiroho kuliko wachamungu.

Mchawi yeyote anaishi maisha ya kitumwa katika uhai wake wote ,anaishi kwa kuyatumikia mashetani ambayo yana demand afanye kufuru kila uchwao. Ni maisha dhalili na ya tabu sana kuliko watu wanavyodhani.Wachawi wanaishi maisha ya dhiki sana hapa duniani na hawana amani ya moyo.
Hicho ulichokanusha na kile umeeleza ni vitu viwili tofauti. Umeelezea matokeo ya matendo ya wachawi kuwa yanafanya uzoefu wa maisha yao uwe wa kitumwa. Ni sawa na mtumwa wa pombe na au pengine sigara au ngono. Hayo ni matokeo. Lakini pamoja na matokeo hayo hakumfanyi mchawi ashindwe kuwa mbele kiroho kushinda wale wanaosema wachaMungu kwa nadharia walio wengi. Wachawi wana ujuzi mkubwa wa kiroho kwa matumizi hasi kiyume na maadili ya Mungu na wanadamu.

Kumbuka sijasema wana nguvu kubwa. Nasema UJUZI kwa maana nyingine UELEWA au ELIMU KWA VITENDO. Nguvu anawapa mhusika anayerogwa.
 
Ipo hivi.
Hakuna nguvu mbili duniani. Nguvu ni moja tu ambayo ni ROHO ya Mungu. Shida inaanza pale kwenye UHURU tuliopewa kuchagua. Kila mmoja wetu ana uhuru wa kuchagua nini anataka. Sasa Shetani anaingia na kukupendekezea mambo yake kupitia milango mitano yaani macho, pua, mdomo, masikio na ngozi ya mwili. (NB. Mimi sio mwanasayansi mtanisamehe sijui nimetumi maneno sahihi). Hivyo kwa hila kupunguza kufanya chaguzi kwa uhuru kwa sababu ya msukumo wa ibilisi.

Sasa tukirudi upande wa uchawi. Hawa wanajua vyema utendaji wa nguvu ya Roho japo shetani kajiingiza kati hapo na kuuteka mfumo hizo nguvu zikaelekezwa mahali pa uharibifu. Kuna viongozi na waalimu wengi hujiita wa kiroho au dini (lakini sio wote) hawana ufahamu wa utendaji wa ulimwengu wa Roho kitu ambacho kila mchawi lazima ajue. Wanautumia vibaya.
 
Anayebisha kuwa uchawi hamna namuona bado hajapitia mahangaiko,Dunia hii tunayoishi unajua kwamba kuna watu wana maono ya kuona hadi message unazochart na mtu mwingine,kuna watu wana uwezo wa kuku scan na kujua hadi pesa utayolipwa kesho,Kuna watu wana maono ya kuona kuwa huko unapoenda ni hatari na hawaendi!!!
Ongeeni tu ila haya mambo yapo aisee!!

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Kuna wengine wanapiga faraq Hadi Mke wa kuowa yaani wanaangalia ktk hiyo familia hakuna aliyewahi kuugua ukichaa, hakuna kipofu, hakuna vbaka mateja mashogaaa ndipo wanaowa ikiwa hayo makandokando hakuna.
 
Back
Top Bottom