Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Lakini sema la ukweli first experience kwenyd ndege sio mchezo.
Kund msiba flani ulitokea Arusha wa mtu wa hapa ICTR-UN sasa yule bwana alikuwa mtu wa Congo ikabidi mama mmoja local nae akaenda huko Congo kumzika jamaa.

Shida ilikuja wakati mambo tayari ndege iko kwenye run way ndo inaacha ardhi mama alishikwa na tumbo la dharura yule alipiga yowe moja kilichofwata sina kumbukumbu nacho vyema

Kwani ilibidi pilot apige turn up kwa sababu za kiafya kwani hali haikuwa muhali hata kidogo me nlijuaga watu huwa wanatapika tu

Kwenye ndege lakini yule mmama alienda some extra Miles Jamani.
 
Mimi ilikuwa 1999,uelekeo nairobi, mke wangu akaniambia kwa uzoefu aliohadithiwa na babaake huko hewani mtu lazima usikie njaa sana, akaniandalia hotpot la makande, nasikitika sana maana lilibakia airport, kipindi hicho hakuna vifaa vizuri vya ku-detect madawa, kwa hiyo wakayafananisha na madawa!

Ushamba gunia la misumari, unarekebisha mmoja, tisa inakuchoma!!!
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

Mimi sikumbuki mara ya kwanza ilikuwaje kwa sababu nilikuwa napandishwa ndege tangu utotoni mno.

Kitu ambacho sisahau safari moja nilikaa siti ya karibu na mama mmoja alipanda na jogoo amemuweka kwenye mfuko wa plastik kichwa kiko nje nilikaa kwa tahadhari muda wote kuangalia yule jogoo asije kunidonoa.
 
Babu Dc, tupe nawe ushamba wako, mara ya kwanza kabisa kupanda ndege


Ya kwangu yamesha-expire kwa kweli....

Ila ni kweli kwamba huwa kuna changamoto sana siku ya kwanza kupanda ndege. Na tatizo kubwa ni kwamba mara nyingi tunashindwa kufuata maelekezo. Kila kitu ama husemwa na wahudumu au kipo kwenye safety cards. Ila kwa sababu ya kihoro na mazoea ya kutojitafutia taarifa/maarifa, tunaishia kutofuata maelekezo.

Na wahudumu wa ndege za ndani (hasa hasa hapa Tz) wanajifanya kama vile ama wao wamezaliwa kwenye ndege au wakiwa na ndege mkononi kama toy zao!
 
Mimi wakati ndege inapaa juu ili ikae sawa nikasikia kichefu chefu kikali mno na mate yakanijaa kibao mdomoni.

Kila nilipojaribu kufungua dirisha niteme mate nilishindwa mpaka nikajamba baada ya ku force kwa nguvu zote na kutoka kapa. Jamaa jirani yangu akanishika akaniambia ee bwana vipi mbona unataka kutua, wewe ni gaidi?

Kumuuliza kulikoni ndipo akaniambia kuwa madirisha ya ndege hayafunguliwi na kunipa sababu zake, nilisikia haibu na wala sikuongeat tena na watu mpaka nilipofika Uturuki via Tokyo.

Ushamba na mazoea ni vitu vingine jamani.
 
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibni, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahamu yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.

Hahahahahaha!!!
 
Back
Top Bottom