Vipindi kama hiki kwenye TV vinamlenga nani?

Vipindi kama hiki kwenye TV vinamlenga nani?

"mimi binafsi" binafsi siwezi kulifananisha hilo gazeti na tbc1.
Ile inaitwa ya taifa, inapatikana nchi nzima mpaka vijijini, kabla ya digital/analog thing karibu kila mtanzania aliweza kutazama tbc, vipi kuhusu hilo daily news?
Kwanini basi siku moja kiongozi wetu mkuu asitumie kiingereza kuongea na wananchi?
Usipotaka kujifunza lugha mbalimbali, utakosa mengi.
 
Hatari.

Mie sio Mwanakijiji, kama Marx Groucho kijiji chochote kitakachonikubali ntakikataa kwa kunikubali chizi kama mie.

Ha ha haaa! Hilo jina lako tu latosha kukuelezea mkuu, nadhani ulitulia sana kulipata hilo jina.
 
Tatizo ni masoko pia, kina marehemu Hammie Rajab waliandika hadithi za kichawi.Miujiza ya mlima kolelo ni hadithi ya kichawi na iliuzika.
Kisiwa cha hazina, masaibu ya ndugu Jero na mabepari wa Venisi ni hadithi na tamthilia zilizotafsiriwa kiswahili successfully.
Nimeisoma Greek Mythology moja inaitwa Antigone, ambayo ni tamthilia iliyokuwa scripted karne tano kabla ya kuzaliwa Yesu, ikatafsiriwa kiingereza. It took a lot of work kuiweka kwenye hadhi yake ya kiasili na ni moja ya tamthilia inayotumiwa vyuoni US kujifunza Rhetoric. Inaweza kutafsiriwa kiswahili, ila marketability itawafanya publishers ku-hesitate.
Soko ni kitu muhimu kwa sababu hivi vitu ni gharama kuvifanya.
Ila nakubali kuwa culture ya kujisomea is almost dead kwa jamii zinazoongela kiswahili, na hii ndiyo sababu kuu ya kutotafsiri baadhi ya vitabu muhimu.

Mimi naona interest imepungua, lakini vitabu kama
1.Kisima cha Giningi ( sikumbuki if it was a full book or chapter )
2.Visa vya umslopogaas
3.Mfalme Suleiman na machimbo ya ajabu
4.Mzimu wa watu wa kale

Na vingine vingi nilivisoma enzi nikiwa primary na vilitungwa vizuri sana, sasa hivi huko facebook naona riwaya za mapenzi nyiingi ambazo nikianza kusoma mwanzo tu najua mwisho itakuwaje...

Interest imeisha na kisha wale magwiji wa fasihi na watunzi wamezidi kufifia

Nilijitahidi kumtafuta bwana Mohamed Shaffi ( yule mwenye local sleuth Bwana Msa ) sadly aliniambia vitabu vyake sasa vingi vyachapishwa Nairobi

I would really like to get hold of those great books...
 
fomu ya kujaza masomo ya shahada ya kiswahili UD inajaza kwa kingereza hata PhD za kiswahili wanaandika kwa kingereza.Askimwambie mtu ukitaka mshichana mzuri mlimani city ongea kingereza,ukitaka kazi jua kingereza
 
Hatufanyi biashara ya samaki, hata ya vitumbua imetushinda.

Kung'ang'ania Kiswahili ndicho kile kinachoitwa "putting the cart before the horse".

Tengenezeni uchumi mzuri, mtaona Wachina wenyewe wanaanzisha vyuo vya kujifunza Kiswahili Beijing kabla hata nyie hamjaanza kuki promote.

Hata tukijua Kiswahili kizuri wooote, kama hatuna uzalishaji hicho Kiswahili kitatusaidiaje katika biashara ya kimataifa?

Lazima uitwe msaliti.
 
Mimi naona interest imepungua, lakini vitabu kama
1.Kisima cha Giningi ( sikumbuki if it was a full book or chapter )
2.Visa vya umslopogaas
3.Mfalme Suleiman na machimbo ya ajabu
4.Mzimu wa watu wa kale

Na vingine vingi nilivisoma enzi nikiwa primary na vilitungwa vizuri sana, sasa hivi huko facebook naona riwaya za mapenzi nyiingi ambazo nikianza kusoma mwanzo tu najua mwisho itakuwaje...

Interest imeisha na kisha wale magwiji wa fasihi na watunzi wamezidi kufifia

Nilijitahidi kumtafuta bwana Mohamed Shaffi ( yule mwenye local sleuth Bwana Msa ) sadly aliniambia vitabu vyake sasa vingi vyachapishwa Nairobi

I would really like to get hold of those great books...
Hizo translations zilikuwa funded na wakoloni, na baadhi ya mashirika ya kimataifa na vimesaidia sana kupanua mawazo ya vizazi husika.

Kwa mfano sasa hivi, Siri ya Mtungi umedhaminiwa na John Hopkins, na una English subtitles ... huwezi jua, siku moja kunaweza kuwa na kitabu cha kiingereza cha mchezo huo.
Ukiwa na mtu kama Mulugo, utajua tu vision yake haioni kabisa umuhimu wa hivi vitu. Wamekazania per diems na makongamano yasiyo na maana .... we're lost!!
Chuo cha ualimu Chang'ombe wana maktaba nzuri sana!!!, try it utapata vitabu vizuri vya kiswahili.
 
fomu ya kujaza masomo ya shahada ya kiswahili UD inajaza kwa kingereza hata PhD za kiswahili wanaandika kwa kingereza.Askimwambie mtu ukitaka mshichana mzuri mlimani city ongea kingereza,ukitaka kazi jua kingereza

Huh! Hayo ya hizo fomu ni ya kweli?
 
Lazima uitwe msaliti.

Kama kutaka maendeleo ya uchumi kabla ya kuweka mbele maendeleo ya utamaduni ni usaliti basi mie msaliti namba moja.

The Italian Renaissance which fueled European awakening did not arise because the Italians were writing wonderful plays in Italian.

The Italians were able to write wonderful plays in Italian, and stock the universities with good books, an patronize the arts and medicine (Medicine is a derivative of Medici, from the Italian patrician family of that name, that is how influential economic patronage was) because of economic affluence.

So you do not get cultural dominance without economic dominance and affluence. Cultural dominance comes after economic dominance, almost automatically.

This is why the Iranians and Egyptians have a story telling culture spanning millenia but Hollywood - at least until very recently- has been dominating at the movies worldwide.

Sie tunataka tuanze na utamaduni wa kung'ang'ania Kiswahili wakati hatuna hata printing presses za maana na watu wetu hawanunui vitabu!
 
Lugha.
Mnaangalia tamthilia za kikorea, lakini hamuoni umuhimu wa kuangalia mahojiano ya kiingereza.
It makes no sense at all!!

Ntaangaliaje mijadala ya kiingereza wakati siwezi hata kuomba maji kwa hiyo lugha?
Pengine hukuelewa swali.
Swali lilikuwa kipindi kinamlenga nani?
Ila nashukuru kuna waliolielewa wametoa mtazamo wao na nimewaelewa kiasi chake.
Rejea mada mkuu.
Pengine nimeuliza swali kwaniaba ya wengi mkuu.
 
Kama kutaka maendeleo ya uchumi kabla ya kuweka mbele maendeleo ya utamaduni ni usaliti basi mie msaliti namba moja.

The Italian Renaissance which fueled European awakening did not arise because the Italians were writing wonderful plays in Italian.

The Italians were able to write wonderful plays in Italian, and stock the universities with good books, an patronize the arts and medicine (Medicine is a derivative of Medici, from the Italian patrician family of that name, that is how influential economic patronage was).

So you do not get cultural dominance without economic dominance and affluence. Cultural dominance comes after economic dominance, almost automatically.

This is why the Iranians and Egyptians have a story telling culture spanning millenia but Hollywood - at least until very recently- has been dominating at the movies worldwide.

Sie tunataka tuanze na utamaduni wa kung'ang'ania Kiswahili wakati hatuna hata printing presses za maana na watu wetu hawanunui vitabu!

Huo uchumi wenyewe kuujenga kwa kujitegemea, hatuwezi mpaka tuwezeshwe na wakubwa wa dunia, mikataba inaandikwa kwa lugha za wakubwa na hata misaada tunaomba kwa kutumia lugha ya malkia. Naunga mkono hoja. Uchumi kwanza, utamaduni baadaye.
 
Kesho nitakuja na jina la kipindi fulani, nacho ninaona hakiendani na maudhui yake.
Nikatika kuboresha tu.
Constructive criticism.
 
Nyerere aliwahi kusema anayedharau utamaduni wake ni mtumwa! Wasomi wetu wamekuwa watumwa wa utamaduni wa magharibi! Mbona rais wa China analiongea Kichina? Akawepo mkarimani alipokuja Tanzania. Cha kushangaza Rais wetu akaongea Kiingereza! Tuache hii tabia! Asante kiongozi. Tuache mbwembwe za kisomi kuongea kiingereza kwa waswahili.(UDASA) Waliongea kiswahili kwenye kongamano juu ya elimu ya Tanzania itv walirusha kongamano kwa kiswahili.
 
Kijijini kwa kina Nyani Ngabu. Hapa mjini ujinga wako hata ukiuongea kwa Kiarabu, utapata watu wa kuutafsiri na kueleweka ni ujinga.

In short hicho kipindi ni Generali on Monday, UJINGA MTUPU!

Mwana mtoka Pazuri (tumboni kwa mama). Kile kipindi kinaitwa This week in persp...! perspect.............! Perspecti......! perspectifuuuuuu!......persipectiv......... sory mate yamekauka mdomoni maana hizi lugha ni kwa faida yao.
 
Back
Top Bottom