Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,304
Jiulize tu ni watu wangapi kwenye maktaba zao za nyumbani wana hata kamusi moja ya Kiswahili sanifu.
Unakadiria asilimia ngapi ya Watanzania wana maktaba zao za nyumbani?
Jiulize tu ni watu wangapi kwenye maktaba zao za nyumbani wana hata kamusi moja ya Kiswahili sanifu.
Unakadiria asilimia ngapi ya Watanzania wana maktaba zao za nyumbani?
Papa Kiranga ananiweza wapi wakati anakwenda tangentially? :lying:
Jokes aside,
Kuwauliza watu wengine wanaotumia Kiingereza kufikisha ujumbe wao sehemu kama hii ni njia moja inayokubalika kisayansi katika kukaribia jibu lako
Watu wenye ushawishi katika jamii kupitia maandishi yao, wanapoandika kwa Kiingereza baadhi ya makala zao wanakuwa na lengo gani?
Ukijua hilo ninadhani unaweza kufanya makadirio ya sababu za vyombo vyengine vya habari
Kiranga
Na ukitaka utafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza "sanaa/sayansi ya uchawi" hutapata maneno ya kutosha kufikisha ujumbe wako
Misamiati ya Kiswahili imesheheni kwenye suala hilo
Ndumba, urogi, dawa, giningi, kirambi, kikoa, mchawi, kigagula, fundi, mganga, babu, msukule, ......
Duh! Kama inafika hata 0.9 nitashangaa sana.
Wewe je?
Wewe mtu unakwenda kujadili katiba, na tofauti ya jurisprudence, jurisdiction, sovereignty, state, nation, citizenship, nationality etc etc.
Vitu ambavyo mtu aliyepitia mambo hayo -ambayo mazungumzo yanakuwa relevant kwake- ukimtajia tu anavijua, utake kuanza kusema Kiswahili wakati maneno yenyewe Kiswahili mpaka uyavute kutoka "secondary memory device" kama sio tertiary, wapi na wapi?
Tumetengeneza a mongrel of a diction.
Kiswahili hatujui, lugha za makabila hatujui, kiingereza hatujui. Kwa hiyo mtu akisema yuko more comfy na Kiingereza, I realize it may prove exclusivist, lakini poa tu.
Labda ndo wengine watajifunza.
Tukisema ni asilimia 1 tu ya watu wote wa Tanzania, maana yake tunazungumzia watu 440,000 ambazo ni kaya 110,000
Nna wasi wasi hata 0.5 percent ni kubwa mno
Status is a relative term...Hayo magazeti yana-status ya hiyo tv husika?
Hahaha,
Hii ni habari ya propaganda za wazungu. Wazungu wana uchawi mpaka umekubalika kuwa katika popular culture a la "Harry Potter".
Jaribu kuandika kitabu cha uchawi Kiswahili kama hatujakutoa macho.
Halafu sie sie ndo wa kwanza kushabikia Harry Potter!
Waafrika kwa hypocrisy. Uchawi mbaya wa muafrika, wa mzungu sanaa na sayansi.
Hata kama tunaweza kuitegemea lugha ya Kiswahili pekee, kwa nini tuji limit?
Nikikaa na Waingereza/ Wamarekani wanaojua kuongea lugha moja tu, yao ya Kiingereza, na mimi najua mbili moja yangu Kiswahili, nyingine yao Kiingereza, nishapata advantage kwao. Hata fikra zangu zimekuwa enriched na kujua lugha zaidi. Kuna methali na misemo ya Kiswahili huwezi kuipata katika Kiingereza.
Kwa nini iwe either/or ? Why is this a question that needs to be mutually exclusive?
Kwa nini tusiweze kufanya mambo kwa lugha zaidi ya moja kwa mpigo?
I was talking with Brian Greene on the possibility of translating "The Elegant Universe" into Swahili. Around ten years ago now.
Nika conclude Kiswahili si tu hakina msamiati wa kutosha kutafsiri kitabu hicho, bali pia hakina hata taasisi za kutosha na utamaduni wa sayansi wa kutosha kufanya hata utunzi wa maneno mapya ueleweke vizuri.
I concluded the whole exercise was futile.Those who will delve into that stuff probably already know english sufficiently to read in english, and those who do not know english sufficiently would probably not grasp the material even in Swahili.
A cynical but realistic assesment that will give me the doubt of debt to the few young fellows who need the right inspiration.
Awepo mzee kifimbo cheza kunyoosha kiswahili maana hizi R na L mixing hata kwenye magazeti, vitabu ( by the way mwanakijiji not sure he's same person as you,) ila hata hicho kitabu cha majeruhi nacho kiko affected na hizo R na L mix
TBC wakiandika habari sasa hivi tu naglance hapo wameandika 'wapiga RAMRI Mbeya kuona cha moto' yaani baadae kizazi kinachofuata kitayapokea hayo makosa na kuyanakshi kwa xaxa xawa...
Maktaba za nyumbani wakati watu hawajala?
Watanzania wangapi wana vitabu zaidi ya 20 ambavyo si Biblia, Kuran (na vya dini kama nyimbo etc) au vya shule?
Wakuu, Kiranga na Nyani Ngabu kama mlibahatika kufuatilia mjadala wa elimu uliorushwa live na ITV, mtakuwa mliwasikia baadhi ya wasomi wetu, akiwemo doctor mmoja maarufu sana akitetea matumizi ya kiswahili ili tuwe kama wachina na wajapani kwa kutegemea lugha zao. Alisema "hatufanyi biashara ya samaki jamani, kwanini tusiienzi lugha yetu?"
Wana fj nimekuwa nikijiuliza hili bila majibu.
Kuna kipindi fulani kwenye tv fulani, mara nyingi huusisha wasomi na wanazuoni mbali mbali na kuongozwa na mwenye kiti wao ila lugha ambayo imekuwa ikitumika ni kiingereza wakati wageni wake karibu mara zote huwa watanzania,tena wakati mwingine unahisi wazungumzaji hawako huru kutumia lugha hiyo.
Naomba kufahamu kipindi kama hiki kinamlenga nani?
Hatari.
Mie sio Mwanakijiji, kama Marx Groucho kijiji chochote kitakachonikubali ntakikataa kwa kunikubali chizi kama mie.
Tatizo ni masoko pia, kina marehemu Hammie Rajab waliandika hadithi za kichawi.Miujiza ya mlima kolelo ni hadithi ya kichawi na iliuzika.Wazungu uchawi wao mpaka watunge maneno mapya kuuelezea wakati wetu sisi una maneno ya kuchagua, uchoke wewe tu.
Tatizo ukiandika kuhusu uchawi, tena kitabu cha watoto, utaitwa wewe mchawi.
Si hasha hata ukafukuzwa kwenye nyumba za ibada
Lakini tatizo kubwa zaidi ni kuwa Waafrika sisi wenyewe hatuandiki chochote tunasubiri Mzungu aje atuandikie kwa mtazamo wake ikisha tulalame
Status is a relative term...
Sioni tofauti ya Daily News na TBC.
Halafu, vipindi vya TV na Redio huwa vinanunuliwa sometimes. Huwezi kujua contract ya Jenerali au Kasongo na hizo TV stations.Nilipoenda nyumbani kuna siku nilimuona ndugu yangu wa kike akilia sebuleni, nikashtuka nikamuuliza kulikoni?
Akanijibu tamthilia, kuna mwanamke ameonewa sana .. kuangalia, ni wachina/Korea na lugha hata sikuelewa.
Media ni biashara, Kuna vipindi vya Tv vinakuwa syndicated regionally na unalipwa hela nzuri tu, sometimes without affiliation na local radios/tv ... Howard Stern, Fareed Zacharia,David Letterman ETC...
Oprah is syndicated worldwide ...