Vipindi kama hiki kwenye TV vinamlenga nani?

Vipindi kama hiki kwenye TV vinamlenga nani?

Chagua wimbo ....

Mahaba ya, siku hiziii, maridadi saaana, maridadi saaana, maridadi sana

Tara ntara ntara.Sigara mdomoni.

Tara ntara ntara. Tai shingooni.

Tara ntara ntara.

Lakini hawana fedha mfukoooni.

Vijanaa wa, siku hizi, maridadi saana, maridadi saana, maridadi saana.
 
Kijijini kwa kina Nyani Ngabu. Hapa mjini ujinga wako hata ukiuongea kwa Kiarabu, utapata watu wa kuutafsiri na kueleweka ni ujinga.

In short hicho kipindi ni Generali on Monday, UJINGA MTUPU!

Mkuu, hicho kipindi ni chs TBC1; This week in perspective na Adam Simbeye.
Chanel Ten wana Hamxa Kassongo hour ns Hamza Kassongo, na Shall we Make it? na Makwaia wa Kuhengr ambaye huwa na kipindi kama hicho kwa Kiswahili; Je, Tutafika?
Jenerali on Monday ni makini sana na ni Kiswahili isipokuwa pale anapomwalika mgeni asiyezungumza Kiswahili.
 
Last edited by a moderator:
Mahaba ya, siku hiziii, maridadi saaana, maridadi saaana, maridadi sana

Tara ntara ntara.Sigara mdomoni.

Tara ntara ntara. Tai shingooni.

Tara ntara ntara.

Lakini hawana fedha mfukoooni.

Vijanaa wa, siku hizi, maridadi saana, maridadi saana, maridadi saana.

😛ound:

You are so wrong for this
 
Kidogo nimekupata.
Kwahiyo pale watu wako mazoezini?
Kimsingi issue hapo ni majadiliano ya kinachoendelea nchini kwa wale ambao wanaitumia hii lugha, lakini kwa upande mwingine ni mazoezi kiana (japo si rasmi) kwetu sie watz wote wasikilizaji na wazungumzaji maana hapo panatumika kama forum ya kujadiliana kwa mapana na marefu kwa lugha ya kigeni hasa ukizingatia mengi yanayozungumzwa huwa tayari tumeyapata kwa kiswahili hapo inakuwa fursa ya kuyapata kwa lugha nyingine na kuboresha uwezo wetu wa kuelewa hiyo lugha ambayo kwa namna moja nyingine ni muhimu pia

Pia aAngalau na wao warushe japo kipindi kimoja kwa kithungu kutimiza msemo wa lugha za mawasiliano kwa nchi yetu ambazo ni kithungu na kiswahili kingine nadhani kuna wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wapo Tz bahati mbaya lugha yetu hawaijui sio vibaya kama wakipata mambo yanayoendelea nchini kwa kusikia moja kwa moja angalau mara moja kwa wiki nao waka tune Tv zetu za ndani badala ya kubaki BBC, CNN etc wakati wapo Tz hasa ukizingatia huwa wanasoma magazeti machache ambayo yameandikwa kwa kithungu.
 
😛ound:

You are so wrong for this

Sweets for my sweet, sugar for my honey
If I say I love you baby what will you do?
Roses are red and violets are blue
Public display of affection for a love that's true
 
Sweets for my sweet, sugar for my honey
If I say I love you baby what will you do?
Roses are red and violets are blue
Public display of affection for a love that's true

You are on fiyah today.

Umeota nini?

Au niulize umeotwa nini?

:laugh:
 
Hiyo habari ya mazoezi hata mie nishaitumia kuhalalisha kutumia Kiingereza mbuzi hapa JF.

Hivi tutategemeaje a young executive ambaye anaanza kupata mialiko kwenye conferences za kimataifa aweze kuongea Kiingereza kama expert wa Tanzania, South Africa huko, kama hajaanza kuongea Kiingereza hapa Tanzania?

I would like to say that these executives should be comfortable in their communication skills already, but sadly that's not the case. Plus the added atmosphere of TV debate/ discussion adds to it. Labda wanatoa changamoto kwa wengine kujifunza kiingereza. Tukae tukijua pia kwamba tunapata wageni wengi tu wasiojua Kiswahili na wadogo zetu wanatakiwa kuona mfano wa Tanzania inayojifungua zaidi kimataifa.

Kuna uncle wangu mmoja alikuwa anasema jumbe za Tanzania zikienda nchi za nje mara nyingine watu wa nje wana crack jokes (a "cracking the ice" ritual for any seasoned business person/ globetrotter), sasa kuna watu fulani kiingereza kimewapita kushoto hawaelewi jokes, kucheka kwao kunakuwa kwa kufuata mkumbo tu akiona mtu anacheka na yeye anacheka.

Was it Nyerere who said "Kiingereza ndiyo Kiswahili cha dunia"?

Hivi siku hizi shule zetu bado zinaendeleza debate societies?

Mkuu, vipi ule mkakati wa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia mpaka chuo kikuu?
Hatuwezi kuwa tunajikanganya?
 
We anakuweza papaa Kiranga.

Papa Kiranga ananiweza wapi wakati anakwenda tangentially? :lying:

Jokes aside,

Kuwauliza watu wengine wanaotumia Kiingereza kufikisha ujumbe wao sehemu kama hii ni njia moja inayokubalika kisayansi katika kukaribia jibu lako

Watu wenye ushawishi katika jamii kupitia maandishi yao, wanapoandika kwa Kiingereza baadhi ya makala zao wanakuwa na lengo gani?

Ukijua hilo ninadhani unaweza kufanya makadirio ya sababu za vyombo vyengine vya habari
 
Mkuu, vipi ule mkakati wa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia mpaka chuo kikuu?
Hatuwezi kuwa tunajikanganya?

Tuanze na mkakati wa kufundisha Kiswahili shule ya msingi kwanza.

I was reading from this piece in the current "Foreign Affairs", it made extensive references to Tanzania

Many governments struggle to provide basic services: teachers in Tanzania's public primary schools are absent 23 percent of the time,

And I feel they were being overly generous!

http://www.rich.co.ke/rcfrbs/docs/FA_MayJune2013-Devarajan-Fengler-Africa.pdf
 
Kimsingi issue hapo ni majadiliano ya kinachoendelea nchini kwa wale ambao wanaitumia hii lugha, lakini kwa upande mwingine ni mazoezi kiana (japo si rasmi) kwetu sie watz wote wasikilizaji na wazungumzaji maana hapo panatumika kama forum ya kujadiliana kwa mapana na marefu kwa lugha ya kigeni hasa ukizingatia mengi yanayozungumzwa huwa tayari tumeyapata kwa kiswahili hapo inakuwa fursa ya kuyapata kwa lugha nyingine na kuboresha uwezo wetu wa kuelewa hiyo lugha ambayo kwa namna moja nyingine ni muhimu pia

Pia aAngalau na wao warushe japo kipindi kimoja kwa kithungu kutimiza msemo wa lugha za mawasiliano kwa nchi yetu ambazo ni kithungu na kiswahili kingine nadhani kuna wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wapo Tz bahati mbaya lugha yetu hawaijui sio vibaya kama wakipata mambo yanayoendelea nchini kwa kusikia moja kwa moja angalau mara moja kwa wiki nao waka tune Tv zetu za ndani badala ya kubaki BBC, CNN etc wakati wapo Tz hasa ukizingatia huwa wanasoma magazeti machache ambayo yameandikwa kwa kithungu.

Mkuu, umeeleza vizuri. Kama kipindi kinalenga hayo si mbaya.
Gaijin nadhani haya yaweza kuwa malengo yao hao "wenye tv"
 
Kwahiyo tunajidanganya tukisema tunawezakuitegemea lugha ya kiswahili pekee na ukweli ni kwamba kiingereza hakiepukiki?

Hata kama tunaweza kuitegemea lugha ya Kiswahili pekee, kwa nini tuji limit?

Nikikaa na Waingereza/ Wamarekani wanaojua kuongea lugha moja tu, yao ya Kiingereza, na mimi najua mbili moja yangu Kiswahili, nyingine yao Kiingereza, nishapata advantage kwao. Hata fikra zangu zimekuwa enriched na kujua lugha zaidi. Kuna methali na misemo ya Kiswahili huwezi kuipata katika Kiingereza.

Kwa nini iwe either/or ? Why is this a question that needs to be mutually exclusive?

Kwa nini tusiweze kufanya mambo kwa lugha zaidi ya moja kwa mpigo?

I was talking with Brian Greene on the possibility of translating "The Elegant Universe" into Swahili. Around ten years ago now.

Nika conclude Kiswahili si tu hakina msamiati wa kutosha kutafsiri kitabu hicho, bali pia hakina hata taasisi za kutosha na utamaduni wa sayansi wa kutosha kufanya hata utunzi wa maneno mapya ueleweke vizuri.

I concluded the whole exercise was futile.Those who will delve into that stuff probably already know english sufficiently to read in english, and those who do not know english sufficiently would probably not grasp the material even in Swahili.

A cynical but realistic assesment that will give me the doubt of debt to the few young fellows who need the right inspiration.
 
Kwahiyo tunajidanganya tukisema tunawezakuitegemea lugha ya kiswahili pekee na ukweli ni kwamba kiingereza hakiepukiki?

Katika ulimwengu wa leo Kiingereza hakiepukiki.

Sasa hilo ongezea na ukweli wa sisi kuwa maskini ndiyo inakuwa balaa kabisa. Kiswahili pekee kitatutenga sana.

Kwa ujumla lugha nchini mwetu ni janga.

Si Kiswahili, si Kiingereza, na si vilugha vya makabila, kote kote hatuna ujuzi na ufahamu wa kutosha.

Ndiyo maana unakuta mpaka leo neno sahihi kati ya "onyesho" na "onesho" wengi hawalijui.

Jiulize tu ni watu wangapi wenye maktaba zao za nyumbani wana hata kamusi moja ya Kiswahili sanifu.
 
Back
Top Bottom