Ndo mana wanamwita kila siku Bansen Bana kuongelea muktakabali wa taifa.
bansen bana.....ha ha ha
Ndo mana wanamwita kila siku Bansen Bana kuongelea muktakabali wa taifa.
Nilijitahidi kumtafuta bwana Mohamed Shaffi ( yule mwenye local sleuth Bwana Msa ) sadly aliniambia vitabu vyake sasa vingi vyachapishwa Nairobi
Mwana mtoka Pazuri (tumboni kwa mama). Kile kipindi kinaitwa This week in persp...! perspect.............! Perspecti......! perspectifuuuuuu!......persipectiv......... sory mate yamekauka mdomoni maana hizi lugha ni kwa faida yao.
Hapa umewachanganya waandishi watatu tofauti
1. Muhammed Said Abdulla (Bwana Msa) ndie aliyetunga vitabu kama Kosa la Bwana Msa, Duniani Kuna Watu, Mzimu ya Watu wa Kale, Mwana wa Yungi Hulewa, Siri ya Sifuri......
Huyu alifariki kwenye miaka ya 90 huko.
2. Shafi Adam Shafi ndie aliyetunga vitabu kama Kuli, Kasri ya Mwinyi Fuad, Vuta ni Kuvute na Haini (kinachozungumzia Mapinduzi ya Zanzibar)
Huyu nae kitabu chake hicho Haini amekichapishia Kenya lakini Tanzania nako kinapatikana
3. Muhammed Said Ahmed ndie aliyetunga Asali Chungu, Utengano,.....
Licha ya kuwa jina lake linafanana na la "Bwana Msa", huyu yuhai na anachapisha kazi zake nyingi Kenya
Kuna kipindi kingine cha hivi karibuni, mara nyingi kimekuwa kikiendeshwa na mtangazaji mmoja mwenye mbwembwe kidogo linapokuja swala la matamshi na matumizi ya lugha yetu.
Hiki kipindi kinaitwa "*** ya jirani" Naomba kukiri kwanza kuwa mimi si mtaalamu wa lugha na niko tayari kusahihishwa lakini ukikiita kipindi ...ya jirani wakati humo ndani kuna maudhui ya hapa hapa ndani, nini mantiki yake? Kwanini basi tusichague jina tofauti na hilo?
Nimeshaligeuza hilo jina kila upande ila sipati picha.
Muongozo tafadhari.
Hicho kipindi jina lake ni tusi?
Maana naona asterisks nyingi
Nimerekebisha bana ila sijaweka jina kamili ili mchangiaji awe anafahamu kwanza ninazungumzia kitu gani, siyo tu mtu adandie gari kwa mbele.
Hicho kipindi cha ".... ya jirani" kishawahi kuonyesha maudhui gani ya ndani ya nchi zaidi ya yahusuyo Zanzibar?
Hamna bana, mbona juzi niliwaona nyota wa bongo muvi wakizungumzia filamu zetu?
Cha ajabu kingine, muhtasari wa kipindi unasema, Afrika ni moja na kwambwa tutakua tukiangazia nchi mbali mbali barani Afrika, ila hiyo juzi walikuwa wakizungumzia miaka 100 ya filamu za kihindi ikipewa uzito wa kutosha katika kipindi, sasa sijui India iko Afrika au vipi?
Wajipange bana.
Nyumba ya jirani imefika mbali kidogo hadi mtaa wa saba!
Lakini labda waliangazia sana suala hilo kwa sababu filamu za Kihindi zimekuwa ndani ya utamaduni wa Kitanzania kwa muda mrefu.
Pia kwa kuwa inaweza kuwa an inspiration kwa wacheza filamu wetu
Lakini kama ulivyosema, haiingii akilini kutangaza "Africa ni moja" na "nyumba ya jirani" ikisha ukatoka nje mno ya mipaka hiyo uliyojiwekea na kuwawekea watazamaji
Ubora wa vipi kwenye TV zetu bado uko chini, kunahitajika maboresho, makubwa tena wala si madogo
nimekukubalije..!!!!!!hii htread iko too low..mbona maskuli na vyuoni tunasoma kidhungu,presentesheni kidhunguMbona kuna magazeti ya kiingereza?
nimekukubalije..!!!!!!hii htread iko too low..mbona maskuli na vyuoni tunasoma kidhungu,presentesheni kidhungu
asa icho kidhungu tuongee wapi ka sio k'enye kichupa cha video..