Vipindi kama hiki kwenye TV vinamlenga nani?

Vipindi kama hiki kwenye TV vinamlenga nani?

Tiger

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2007
Posts
1,747
Reaction score
387
Wana Jf,

Nimekuwa nikijiuliza hili bila majibu. Kuna kipindi fulani kwenye tv fulani, mara nyingi huusisha wasomi na wanazuoni mbali mbali na kuongozwa na mwenye kiti wao ila lugha ambayo imekuwa ikitumika ni kiingereza wakati wageni wake karibu mara zote huwa watanzania.

Tena wakati mwingine unahisi wazungumzaji hawako huru kutumia lugha hiyo.

Naomba kufahamu kipindi kama hiki kinamlenga nani?
 
Kiingereza kinaongeza hadhi.

Ukiwa unakijua vya kutosha utaonekana msomi, mstaarabu, utaoneakana una mambo ya kizungu, utaonekana una akili hata kama unachoongea ni pumba na utumbo, kama ni mwanaume basi utashobokewa na wasichana pamoja na wanawake na wakati mwingine hata wanaume wenzako watakushobokea.
 
Kijijini kwa kina Nyani Ngabu. Hapa mjini ujinga wako hata ukiuongea kwa Kiarabu, utapata watu wa kuutafsiri na kueleweka ni ujinga.

In short hicho kipindi ni Generali on Monday, UJINGA MTUPU!
 
Last edited by a moderator:
Ndo mana wanamwita kila siku Bansen Bana kuongelea muktakabali wa taifa.
 
Kijijini kwa kina Nyani Ngabu. Hapa mjini ujinga wako hata ukiuongea kwa Kiarabu, utapata watu wa kuutafsiri na kueleweka ni ujinga.

In short hicho kipindi ni Generali on Monday, UJINGA MTUPU!

Afadhali ya hicho, huwa wanaongea na watu wasio kifahamu kiswahili vizuri(mara kadhaa), na nimeshaona wazungu kadhaa kwenye hicho ulichokitaja.
Ila kuna tv nyingine, kwa kweli mara zote nilizokitazama, huwa nawaona watanzania wenzetu.
 
Last edited by a moderator:
Kiingereza kinaongeza hadhi.

Ukiwa unakijua vya kutosha utaonekana msomi, mstaarabu, utaoneakana una mambo ya kizungu, utaonekana una akili hata kama unachoongea ni pumba na utumbo, kama ni mwanaume basi utashobokewa na wasichana pamoja na wanawake na wakati mwingine hata wanaume wenzako watakushobokea.

Mkuu, ukiwasikiliza hao jamaa, wengi wao wanachapia mbaya.
Ila naomba any positive idea yenye kufanya hicho kipindi kifanyike kwa lugha ya kigeni.
Tafadharini jamani pengine ipo sababu ya msingi.
 
Hicho kipindi kinawalenga Wasomi. Mambumbumbu hawana chao hapo, mpaka kifike kile kipindi cha zecom... Cha wale jamaa wanaopenda kujifanya mademu.
 
Hicho kipindi kinawalenga Wasomi. Mambumbumbu hawana chao hapo, mpaka kifike kile kipindi cha zecom... Cha wale jamaa wanaopenda kujifanya mademu.

Hao wasomi wa studio na wasomi watazamaji hawawezi kufikiri kwa kiswahili?
Vp kuhusu hadhi ya hiyo tv husika, unaifahamu nafasi yake katika jamii?
 
Hicho kipindi kinawalenga Wasomi. Mambumbumbu hawana chao hapo, mpaka kifike kile kipindi cha zecom... Cha wale jamaa wanaopenda kujifanya mademu.

Si tunaambiwa lugha za mawasiliano nchini kwetu ni Kiswahili na Kithungu, nadhani lengo la hicho kipindi ni kujadiliana kwa kithungu ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi watu wasisahau sana maana tunasoma kwa Kithungu kuanzia form 1 mpaka chuo tukija maofisini tunafanya kazi kwa kiswahili na wengine report wanaandika kwa kithungu hivyo inatumika kama forum ya kujipambanua kuhusu hiyo lugha maana kuna watu tangu wamalize shule hawajawahi pata forum ya kutumia hiyo lugha pamoja na kwamba waitumia kwenye elimu sekondary na chuo hasa sie tuliopo huku maeneo ya Maligisu tunakutana na wananzengo tu hata kiswahili ni nadra kutumia
 
Kiingereza kinaongeza hadhi.

Ukiwa unakijua vya kutosha utaonekana msomi, mstaarabu, utaoneakana una mambo ya kizungu, utaonekana una akili hata kama unachoongea ni pumba na utumbo, kama ni mwanaume basi utashobokewa na wasichana pamoja na wanawake na wakati mwingine hata wanaume wenzako watakushobokea.

To buttress your point.

My crew was into hip hop/ dancehall, magazines, books, MTV etc and therefore it wasn't unheard of to jive in English.

Way back in the days narudi kutoka Coco Beach na washkaji basi kuagana of course, talk to you later nyiingi, say hi to so and so nyiingi, yeah yeah nyiingi, basi washkaji walikuwa wanampa lift shawty mmoja wa Kinokino.

Shawty si akashindwa kujizuia akasema "huyu ana kiingereza kizuuuri".

Kama vipi mtu unaselebuka kisa Kiingereza tu.

But I digress.

On the one hand naweza kusema vipindi hivi ni elitist, exclusivist, uppity and even self defeatist.

On the other hand, wabongo tunatakiwa kuongea kiingereza zaidi ili kuji integrate vizuri na dunia, kwa hiyo labda vitasaidia kuonyesha kwamba si ajabu watu Watanzania kuongea Kiingereza.

There is no reason we should not have these shows in both Swahili and English.
 
Si tunaambiwa lugha za mawasiliano nchini kwetu ni Kiswahili na Kithungu, nadhani lengo la hicho kipindi ni kujadiliana kwa kithungu ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi watu wasisahau sana maana tunasoma kwa Kithungu kuanzia form 1 mpaka chuo tukija maofisini tunafanya kazi kwa kiswahili na wengine report wanaandika kwa kithungu hivyo inatumika kama forum ya kujipambanua kuhusu hiyo lugha maana kuna watu tangu wamalize shule hawajawahi pata forum ya kutumia hiyo lugha pamoja na kwamba waitumia kwenye elimu sekondary na chuo hasa sie tuliopo huku maeneo ya Maligisu tunakutana na wananzengo tu hata kiswahili ni nadra kutumia

Kidogo nimekupata.
Kwahiyo pale watu wako mazoezini?
 
Wanaoanzisha mijadara kwa lugha hizo wanasababu zao na mtu kufanya hivyo hapa jf hainipi shida maana aliyeweka uzi anajua anamlenga nani? Ila kwa kuwa bado sijajua wale wa kwenye "ile tv" wanamlenga nani ndo maana nikauliza.

Hizo sababu zao labda ndio hizo hizo sababu "zao" za wenye TV
 
Kidogo nimekupata.
Kwahiyo pale watu wako mazoezini?

Hiyo habari ya mazoezi hata mie nishaitumia kuhalalisha kutumia Kiingereza mbuzi hapa JF.

Hivi tutategemeaje a young executive ambaye anaanza kupata mialiko kwenye conferences za kimataifa aweze kuongea Kiingereza kama expert wa Tanzania, South Africa huko, kama hajaanza kuongea Kiingereza hapa Tanzania?

I would like to say that these executives should be comfortable in their communication skills already, but sadly that's not the case. Plus the added atmosphere of TV debate/ discussion adds to it. Labda wanatoa changamoto kwa wengine kujifunza kiingereza. Tukae tukijua pia kwamba tunapata wageni wengi tu wasiojua Kiswahili na wadogo zetu wanatakiwa kuona mfano wa Tanzania inayojifungua zaidi kimataifa.

Kuna uncle wangu mmoja alikuwa anasema jumbe za Tanzania zikienda nchi za nje mara nyingine watu wa nje wana crack jokes (a "cracking the ice" ritual for any seasoned business person/ globetrotter), sasa kuna watu fulani kiingereza kimewapita kushoto hawaelewi jokes, kucheka kwao kunakuwa kwa kufuata mkumbo tu akiona mtu anacheka na yeye anacheka.

Was it Nyerere who said "Kiingereza ndiyo Kiswahili cha dunia"?

Hivi siku hizi shule zetu bado zinaendeleza debate societies?
 
Back
Top Bottom