Vipigo vya AFCON ni machozi ya wachezaji wazalendo waliopambana kuipigania nchi kufuzu kisha wakawekwa pembeni kuwapisha wapya

Na nisiwe mnafki naomba hili liwe fundisho kwa nia ya dhati kabisa natamani tujifunze kwa maumivu maana wagebga walisema kusikia kwa kenge ni mpaka apigwe na kitu kizito kichwani famu zimtoke masikioni, haya maamuzi yaliyofanyika ya kuleta wachezaji wengine hayana tofauti sana na ukenge.

Mechi zooooote tupigwe, hizi mbili zilizobaki kina Mayele wateteme na kina Chama wafanya non stop target practice.

Kuna wachezaji waliwinda nyama mlimani ajabu wameshuka nayo, ajabu wanaoila ni wachezaji wengine kisa wanacheza nje, hao walikuwa wapi mda wenzao wanapambana ? wanujua uchungu waliopata wenzao ? wana ule moto waliokuwa nao wenzao ?.

Wachezaji waliopitia msoto wa kutafuta nafasi ya kufuzu AFCON ndio walikuwa na usongo wa kuendeleza mapambano ya kumaliza deni ya safari waliyoanza, kuwaleta wengine matokeo yake ni vipigo tu. hata hao waliobakizwa wanakosa chemistry nzuri na hao wapya maana kisaikolojia wapo tofauti.

Kwa akili ya kawaida hata punda akipandisha mlima na mizigo akiona anakaribia kileleni anaongeza bidii sababu anaujua msoto aliopitia na kuwa na usongo wa kumaliza kazi, hio bidii huwezi ipata kwa kumbembesha mizigo punda mwengine na pengine anaweza kuporomoka.

Kwa kauli alizotoa kocha jana nikahitimisha without doubt kocha ni wa mchongo.

Nachoona wachezaji hawa wengi walioletwa wamebebwa, hawana uchungu wala hawajui mziki wa kutafuta from scratch, wanachukulia poa haya mashindano.
Hata wangeenda hao wachezaji walioachwa, bado mngefungwa tu.
 
Back
Top Bottom