Natumai ni wazima..
Lengo la kuanzisha uzi humu ni kutaka msaada wetu wa mawazo jinsi ya kuishi na mume mkali.
Nina miaka minne kwenye ndoa na watoto wawili.
Kwa kweli nampenda mume wangu na yeye najua ananipenda lakini napata mawazo ya kuomba talaka sababu tokea niolewe hajabadilika kabisa anaweza nifokea hata mbele ya wazee wake kisa mtoto kaumia bahati mbaya. Yaani hata mtoto akiamka usiku akalia anatoka sana anasema namfanyia fujo makusudi!
Nikisahau kitu kama chupa ya maji kwenye gari yake anafoka hadi kuishia kuniita ukuta na kutaka kunipiga.
Naumia sana ndugu zangu naombeni ushauri.