Aeleza walivyokubaliana na mume wake kutafuta watoto nje ya ndoa

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
4,580
2,000
Dar es Salaam. Mkazi wa Tabata Liwiti, Magreth Silaeli (37) ameieleza Mahakama ya Mwanzo Buguruni kuwa walikubaliana na mume wake, Raymond Kulaya (44), waachane kwa muda ili kila mtu akatafute watoto “anapopajua” baada ya kuishi miaka mitano bila kupata mtoto.

Magreth sasa anaiomba mahakama itoe hati ya talaka, ili aweze kuolewa na mwanaume anayeishi naye, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya.

Alidai mbele ya hakimu Matrona Luanda kuwa yeye na Kulaya walitengana tangu mwaka 2011.

Alidai alifunga ndoa ya Kikristo na Kulaya mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano bila kupata watoto.

Magreth alidai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na watoto na kumwomba watengane ili kila mtu aende akatafute watoto.Alidai katika kipindi walichoishi pamoja, familia ya ndugu wa mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na watoto na kuwasababishia

“Mimi nilikuwa naumia sana kwa kuwa nilikuwa sijapata mtoto, angalau mwenzangu nilimkuta na watoto wawili, mwishowe mume wangu aliniambia tutengane kwa muda ili kila mtu aende akatafute watoto anakojua,”alidai Magreth

Aliiambia mahakama kuwa kutokana na kutopata mtoto, Kulaya alimweleza kuwa ni bora kila mtu aende upande mwingine kwani atakapoleta mwanamke mwingine ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja hataweza kumuelewa.

“Mimi nilienda kuishi na mwanamume niliyenaye leo na tumebarikiwa kupata watoto wanne,” alisema.

Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata mtoto.

“Kwa kuwa mwanaume ninayeishi naye alinikubali na aliniliwaza wakati nikiwa katika hali ya unyonge na nimezaa naye watoto wanne, naiomba mahakama hii itoe talaka ili mimi niweze kufunga ndoa na mwanaume niliyezaa naye,”alidai Magreth.

Kwa upande wake, Kulaya ameieleza mahakama kuwa aliishi na mke wake Magreth kwa miaka mitano na hawakujaliwa kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 yeye na Magreth walijadiliana na kukubaliana watengane kwa muda ndipo mke wake alipata mwanaume ambaye alizaa naye watoto wanne huku yeye akizaa na mwanamke mwingine watoto watatu.

“Yaani mimi nipo tayari hata leo hii mke wangu nirudiane naye na sina chuki naye na ninawakubali watoto wake nitawapokea, hivyo naiomba mahakama hii itakapotoa maamuzi yake itumie busara kwa hili,”alidai Kulaya. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 17, 2021 kwa ajili ya hukumu.
 
THE BROKER

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
366
500
Kumbuk
Hapo kuna kimbembe, hizi ndoa haki ya Mungu, halafu hao watoto jumla watakuwa tisa sasa, Kama wasipovunja ndoa, hapo ndoa inapaswa kuvunjwa kwa maoni yangu,kwa ustawi wa malezi tu ya watoto..
Kumbuka walikubaliana kufanya hivyo. Kwa maoni yangu naona hakimu awaamuru wakakae tena kujadili matokeo ya makubaliano yao ya mwaka 2011. Wapitishe maamuzi mapya kwa pamoja then mahakama ije kuyabariki
 
Malcolm X5

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,496
2,000
Kumbuk
Kumbuka walikubaliana kufanya hivyo. Kwa maoni yangu naona hakimu awaamuru wakakae tena kujadili matokeo ya makubaliano yao ya mwaka 2011. Wapitishe maamuzi mapya kwa pamoja then mahakama ije kuyabariki
Ni uamuzi wa busara,ila mpaka hapo wako mahakamani kuna shida,mwanamke amegoma kurudi,teyari kaishaanzisha familia na mtu mwingine,na anavyompamba sasa,ndoa inapaswa kuvunjwa tu
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,823
2,000
Kesi ngumu hii,ila kuna kifungu kinachosema kama wanandoa wameshakaa zaidi ya miaka 3 bila ya kuwa pamoja,ndoa inaweza kuvunjwa,sasa sijajua hapo wanasheria wanadadavua vipi.Ila hapa kuna cha kujifunza kuwa michezo mingine sio ya kujaribu...
 
fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,581
2,000
Na wasiwasi hao watt wa mume wa ndoa walotengana kwa hiari sio wake atakua kashikiziwa. Kesi ngumu hii..Na je baada ya kuachana kwa muda huyo mume wa ndoa yy alibahatika kupata watt tena?.maybe Husband anajua tatizo lake thats why aliweza mruhusu mkewe akatafute wtt nje kwa sbb ni ngumu sana maamuzi kama hayo.
muwe mnasoma kwa umakini ,ushaambiwa mume naye kapata watatu nje
 
Malume

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
605
1,000
Dar es Salaam. Mkazi wa Tabata Liwiti, Magreth Silaeli (37) ameieleza Mahakama ya Mwanzo Buguruni kuwa walikubaliana na mume wake, Raymond Kulaya (44), waachane kwa muda ili kila mtu akatafute watoto “anapopajua” baada ya kuishi miaka mitano bila kupata mtoto.

Magreth sasa anaiomba mahakama itoe hati ya talaka, ili aweze kuolewa na mwanaume anayeishi naye, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya.

Alidai mbele ya hakimu Matrona Luanda kuwa yeye na Kulaya walitengana tangu mwaka 2011.

Alidai alifunga ndoa ya Kikristo na Kulaya mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano bila kupata watoto.

Magreth alidai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na watoto na kumwomba watengane ili kila mtu aende akatafute watoto.Alidai katika kipindi walichoishi pamoja, familia ya ndugu wa mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na watoto na kuwasababishia

“Mimi nilikuwa naumia sana kwa kuwa nilikuwa sijapata mtoto, angalau mwenzangu nilimkuta na watoto wawili, mwishowe mume wangu aliniambia tutengane kwa muda ili kila mtu aende akatafute watoto anakojua,”alidai Magreth

Aliiambia mahakama kuwa kutokana na kutopata mtoto, Kulaya alimweleza kuwa ni bora kila mtu aende upande mwingine kwani atakapoleta mwanamke mwingine ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja hataweza kumuelewa.

“Mimi nilienda kuishi na mwanamume niliyenaye leo na tumebarikiwa kupata watoto wanne,” alisema.

Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata mtoto.

“Kwa kuwa mwanaume ninayeishi naye alinikubali na aliniliwaza wakati nikiwa katika hali ya unyonge na nimezaa naye watoto wanne, naiomba mahakama hii itoe talaka ili mimi niweze kufunga ndoa na mwanaume niliyezaa naye,”alidai Magreth.

Kwa upande wake, Kulaya ameieleza mahakama kuwa aliishi na mke wake Magreth kwa miaka mitano na hawakujaliwa kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 yeye na Magreth walijadiliana na kukubaliana watengane kwa muda ndipo mke wake alipata mwanaume ambaye alizaa naye watoto wanne huku yeye akizaa na mwanamke mwingine watoto watatu.

“Yaani mimi nipo tayari hata leo hii mke wangu nirudiane naye na sina chuki naye na ninawakubali watoto wake nitawapokea, hivyo naiomba mahakama hii itakapotoa maamuzi yake itumie busara kwa hili,”alidai Kulaya. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 17, 2021 kwa ajili ya hukumu.
Hii duniaina maajabu sana, moyo wa mwanamke tayari upo sehemu nyingine ni ngumu kurudi kwa kulaya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom