Vipi kuishi na mume mkali kupitiliza?

Vipi kuishi na mume mkali kupitiliza?

Jee kishawahi kukupiga?? Chunguza mzazi wake yupi yupo mkali hio tabia atakuwa kairithi kutoka kwa mzee wake.

Ukishajua kama karithi kutoka kwa baba basi kaa na mama yake na muulize kawezaje kuishi na hio tabia. Na kama karithi kwa mama muulize Baba yake.

Lakini tabia hii kuna jamaa yangu anayo kuna siku aliniomba kitu sasa nikamuuliza unataka hicho kitu kwa nini?? Duh alikasirika hatareee na kuwa mkali, na mimi sikupenda alivyofanya basi nikamtolea ukali kama yeye, mwenyewe alikuja chini mpaka leo heshima kaiweka.

Ukiona mbwa anabweka sio kama mkali kuna wengine ni mbwa koko bali hujaribu kulinda territory zao tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukali ni tabia,
Ukali ni udhaifu.
Mimi mwenyewe ni mkali hadi najiogopa japo siyo rahisi kuniona nikifoka hovyo.
Lakini akiniudhi mtu kupitiliza naweza kumkemea na akimbie kuelekee kusikojulikana.
Nilipogundua mimi ni mkali na huumiza wengine, kwasasa nina mabadiliko makubwa sana.
Hii hali huwezi kuamua kuwa mkali bali ni udhaifu.
LAKINI USISAHAU WATU WAKALI wana huruma sana hasa ukimweleza tatizo huwa anaguswa haraka kukusaidia.
Tumia muda mnapokuwa na furaha mweleze kwa hisia za ndani kuonyesha jinsi anavyokuumiza.
Na hampendi kudanganywa, Putin njoo huku usome hapa
 
Ni tatizo la kisaikolojia hilo nadhani...tafuta hata ushauri kwa wataalam ujue jinsi ya kuishi na mumeo ili ufurahie ndoa yako..

Ndoa isiyo na amani haipendezi
 
Ni tatizo la kisaikolojia hilo nadhani...tafuta hata ushauri kwa wataalam ujue jinsi ya kuishi na mumeo ili ufurahie ndoa yako..

Ndoa isiyo na amani haipendezi
Fafanua tatizo kwa me au ke
Nawajua lkn tiba yenu hasa ni nini? Mkuu kuna best yangu ana ukali huo sasa mimi navyopenda utani dah hebu wadau watusaidie mkuu
Dawa ya mtu mkali ni upole..
Imeandikwa " jibu la upole huondoa hasira kifuani mwa mpumbavu, kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu"
Nikiwa mkali halafu ukanijibu kwa upole yaani ghafla hasira huisha na mara najiona mimi ni mjinga wa mwisho.
Hujikuta nakukumbatia na kukuomba msamaha..ni raha iliyoje hapo!
 
Na wewe mtolee ukali uone kama hatojirekebisha tabia ake
Sasa hapo unataka aambiwe anampanda kichwani... Tatizo halitatuliwi kwa njia iliyotumika kulitengeneza...Tit 4 Tat haifai mkuu
 
Fafanua tatizo kwa me au ke

Dawa ya mtu mkali ni upole..
Imeandikwa " jibu la upole huondoa hasira kifuani mwa mpumbavu, kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu"
Nikiwa mkali halafu ukanijibu kwa upole yaani ghafla hasira huisha na mara najiona mimi ni mjinga wa mwisho.
Hujikuta nakukumbatia na kukuomba msamaha..ni raha iliyoje hapo!
Dah [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] ndo naishi nae ivo na anakuwa mdogooo, lkn kwa wasiomjua sasa inakuwaje mfano unakuta ana girlfriend na huyo girl wake hajui tatizo la jamaa au jinsi ya kumuhandle muwe mnapunguza jazba basi mnatutisha somtym
 
Sasa hapo unataka aambiwe anampanda kichwani... Tatizo halitatuliwi kwa njia iliyotumika kulitengeneza...Tit 4 Tat haifai mkuu
Bora iwe hivo naamini ataacha ama atapunguza kumuonea mwenzie
 
Back
Top Bottom